Kikwete Mshukuru Mola

IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
140
Rais kikwete umetakiwa umshukuru mola kwa jinsi mungu wako anavyokutetea, kwani yale yaliyokuwa yakikutatiza ktk uongozi wako sasa yameanza kupata majibu, Kikwete tunaukumbuka usemi wako ulioutoa siku ile unatangaza baraza lako la mawaziri, uliosema "Tusije tukalaumiana huko mbele ya safari" kweli nimeamini maneno yako sasa, kweli Chenge atakulaumu wapi? Karamagi au Lowasa hatakulaumu, kwa ndugu yako Dito, MUOMBEE KWA MOLA WETU YEYE NDIYE MWENYE KUREHEMU. Najua ulikuwa na mzigo mzito sana baba, hawa jamaa walikuwa wanakuchanganya ila mungu anaendelea kuwapembua kama mchele.

Mzee Kikwete napenda ujua kuwa ulichaguliwa kwa asilimia 80% na sisi wote watanzania tulikuwa na imani na wewe na wala si serikali ya ccm, tuliamini kuwa ukiingia madarakani utaibadilisha serikali hiyo ilioachwa na Mkapa serikali iliyozoea kuwaibia watanzania.

Rais Kikwete kilio cha Watanzania ni maisha bora kwa kila mtanzania ile ahadi uliyoitoa ukiingia madarakani, watanzania wanakuuliza mbona gharama za maisha zinaendelea kupanda huku maisha yao yakiendelea kuwa mabaya?

Rais Kikwete KATIBA MPYA ni kilio cha watanzania wote, hauoni kuwa kuna kila sababu kama mwenyekiti wa Afrika una sababu za kuionyesha afrika wewe unafuata demokrasia iliyobora? hii itawasaidia kupata viongozi waliobora.Lakini pia utakumbukwa na vizazi vyote hapa Tanzania kama mfano bora kuleta katiba mpya? iweje tuongozwe na katiba tulioachiwa na mkoloni yenye kutizama maslahi ya huyo mtawala kwa siku zile? na kila kukicha inaendelea kuzibwa virakaviraka?

Rais Kikwete uzuri wako unatusikiliza sana sisi wajoli wako, tulisema upunguze baraza ukapunguza, tumesema mafisadi wajiuzuru na imekuwa hivyo, Sasa tunakuomba pia mafisadi washitakiwe na serikali, na kama haitakuwa hivyo basi sisi watanzania tutawashitaki sisi raia, tunajua hili nalo utalisikiliza na utalifanyia kazi.

Rais Kikwete tunajua wewe ni rafiki wa watanzania siku zote, damu yako iko mioyoni mwetu sisi watanzania japo kuna dalili za kutusaliti, sote twajua uliingia hapo ikulu ukisaidiwa na wana mtandao, ila kwa sasa waambie kuwa sisi watanzania tumeanza kuwa na uelewa tena si wajingawajinga kama kale, tumekwenda shule japo ni kwa asilimia chache ila chachu kidogo huchachusha donge zima.

Rais Kikwete tunajua chama chetu cha mapinduzi tumejisahau,tumekosa dira hatujui tuendako tumegawanyika makundimakundi ndani ya chama hii inatoa mwanya kutugawa, Tusishangae siku moja tukasikia lile kundi la wasomi wakitusaliti na kwenda CHADEMA, wasomi hao wamechoka kuburuzwa ndani ya chama sasa naomba kama wewe mwenyekiti ulitazame hilo

Rais Kikwete ujue mwalimu alishatoa baraka kwa chama hiki cha CHADEMA, na watanzania wanapenda mabadiliko, hata kuchaguliwa kwako watu walitegemea mabadiliko, sasa kama serikali yako itawatosa fikiria sana si unakumbuka uchaguzi wa 1995

ama mnaonaje JF KWA HILI?
 
Rais Kikwete KATIBA MPYA ni kilio cha watanzania wote, hauoni kuwa kuna kila sababu kama mwenyekiti wa Afrika una sababu za kuionyesha afrika wewe unafuata demokrasia iliyobora? hii itawasaidia kupata viongozi waliobora.Lakini pia utakumbukwa na vizazi vyote hapa Tanzania kama mfano bora kuleta katiba mpya? iweje tuongozwe na katiba tulioachiwa na mkoloni yenye kutizama maslahi ya huyo mtawala kwa siku zile? na kila kukicha inaendelea kuzibwa virakaviraka?

Isaya Mwita,

Je wewe kwa kuanza unaona ni sehemu gani ya katiba ambayo ina matatizo,isije ikawa uansikia maneno ya watu katiba ibadilshwe tu kwa ajili ya matakwa yao binafisi ila hawajua ni wapi kuna makosa.

Kwa kuanzaia mie ningependa wewe utuambie ni wapi katiba ina matatizo na sio kulalama tu.kwa taarifa yako tu katika ilishabadilisha na sio ambyo tulkiachiwa na mkoloni. Ni katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wapi katika katiba imeandika kwamba nchi itafuata melekezo ya mkoloni.??

hoja yako itakuwa nzuri ukija na vipengele vipi vibadilishwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom