Kikwete Msahaulifu au Mzembe?, Anakumbuka Marafiki na kusahau ahadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Msahaulifu au Mzembe?, Anakumbuka Marafiki na kusahau ahadi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Sep 16, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Anakumbuka marafiki na kusahau ahadi

  NAWEZA kudai kumfahamu Kikwete kuliko wengi wa mashabiki wake wanaohudhuria mikutano yake ya kampeni. Nimefanya naye kazi jeshini na serikalini kidogo, lakini nimefanya naye kazi sana kwenye Chama. Nimekuwa naye kwa karibu kama rafiki (siyo swahiba) kwa mambo ya kawaida. Anaweza kuandika hotuba nzuri ya kunisifia siku ya mazishi yangu. Haya yanatoka moyoni.
  Mwaka 2005 yaliandikwa mengi ya kumsifia. Yakasemwa mengi ya kushadidia sifa zake – muungwana, mtu wa watu, mstaarabu, chaguo la Mungu, tumaini lililorejea, mkombozi wa Watanzania, Musa wa pili na chaguo la Watanzania.
  Akazoa kura nyingi zikiwamo za wapinzani, maaskofu, vijana, wasomi, wafanyakazi, wakulima, wachimbaji wadogo, wahamiaji haramu, wanajeshi, na wanafunzi. Naam, hata mama ntilie au kwa jina la utani Mama Lishe! Matumaini yalikuwa makubwa.
  Tuseme ukweli, walioonya wazi juu ya hatari ya huko mbele walikuwa wachache sana, na waliodiriki kufanya hivyo kwa uwazi, ilibidi usiku wawe wanahama vyumba vya kulala!
  Wapo wachache, hata nikidai mimi ni mmojawapo sitaaminiwa kwa maana hakuna ushahidi wa waliokataa ghiliba hii ndani ya chama chetu. Miaka mitano imekuwa ya mateso makubwa kwetu.
  Tumesutwa, tumetukanwa na wanaojifunza kutukana. Tumeitwa majina na tumefikia kuhudhuria vikao vya chama na kuandikwa kuwa hatukuhudhuria kwa sababu ya ukimya wetu.
  Kwenye vikao vya kahawa, tumetumiwa wajumbe wa kutuambia hatuwezi kumfufua aliyekwishakufa (Nyerere), hatuwezi kurudisha nyuma saa iliyokwishakwenda mbele, wakati umepita, tukae kimya. Nani atabishia simulizi yangu hii? Waliokuwa wachambuzi na wasemaji wa kuwatia moyo Watanzania wako wapi? Wote hao wamekwenda, zimebaki sifa zao!
  Nirudi kwenye hoja yangu ya leo. Hivi Rais Kikwete ni msahaulifu au mzembe? Mbona anakumbuka marafiki wake wa zamani na wa karibuni lakini anasahau ahadi zake na kauli zake?
  Walio karibu naye katika kampeni watakubaliana nami kuwa Kikwete ana kumbukumbu kali juu ya watu aliowahi kuwa nao zamani. Kila sehemu anayofika kwa mkutano atakuambia nani anazaliwa pale, atauliza yuko wapi siku hizi, ataagiza mwambie amtafute wazungumze au ataagiza apatiwe hiki au kile kama ameambiwa kuna shida.
  Akiambiwa alikwishakufa, atabadili ratiba akahani msiba au aitiwe mzazi au mjane ampe ubani. Atakumbuka hata dondoo ndogo sana za urafiki wake na mtu huyo.
  Hii inavutia wengi na waandishi wetu wameagizwa na kuamriwa kuhakikisha matukio kama hayo yanakuwa katika picha na kurasa za mbele za magazeti.
  Wakati huo huo, Kikwete ni msahaulifu wa ahadi zake kwa watu binafsi na hata kwa umma. Wapo wanaodai hili si tatizo lake, ni tatizo la watendaji wake ambao wanapaswa ama kuchukua kumbukumbu na kutekeleza au kumkumbusha. Mimi nadhani ni tatizo lake – nitaeleza sasa.
  Uaminifu wa kutekeleza ahadi huanza na kauli. Kikwete ni msahaulifu wa aliyoyasema. Ama hatunzi kumbukumbu za aliyosema, au hafikirii madhara ya kauli zake, au yote mawili kwa wakati mmoja.
  Alipoingia madarakani alisema “urais wake hauna ubia”. Alilenga kuwajibu waliokuwa wanamsakama kuwa ametekwa na marafiki. Juzi juzi wakati anachukua fomu ndani ya chama, pale Dodoma, akakausha macho na kusema; “Urais ni suala la kifamilia”.
  Alilenga kuwajibu waliokuwa wanahoji kitendo cha mtoto wake Ridhiwani kuzungusha fomu ya kutafuta wadhamini. Mpaka hapa inaonyesha Kikwete amesahau alisema nini 2006 au sehemu zote mbili hakufikiri kabla ya kusema. Urais ni taasisi. Urais ni utumishi wa umma. Rais ni mbia wa urais na wananchi wa Tanzania. Ndiyo maana mtu haamki asubuhi na kujitangaza kuwa yeye ni Rais. Anakwenda kuwaomba wananchi wamchague awe rais. Akishakuwa rais, haina maana urais ni mali yake na familia yake.
  Ni kituko kikubwa kwa rais kusema alivyosema Kikwete katika hafla hiyo ya Dodoma. Katika nchi zenye mifumo makini, serikali ingechukua hatua, au chama husika kingechukua hatua na kama vyote viwili vingeshindwa, basi, wananchi wangechukua hatua kupitia sanduku la kura.
  Siyo siri kuwa hivi sasa familia ya Rais Kikwete imeingia kwa nguvu za ajabu katika uendeshaji wa nchi na hakuna mtu ndani ya Chama wala serikali anayeweza kuthubutu kulikemea jambo hili. Uliokuwa ubia wa urais kati ya Kikwete na marafiki zake, sasa umegeuka ubia wa Kikwete na familia.
  Siku hizi si jambo la ajabu kumwona Mama Salma anaingia ndani ya vikao vya Kamati Kuu. Kamati ya maadili wananung’unikia kwenye korido, Kamati Kuu wanaongelea chini chini, wajumbe wa NEC hao ndiyo basi!
  Mama Salma sasa anafanya majukumu ya kichama bila kibali cha kikao chochote, na mbaya zaidi anaagiza, anakemea, anatishia, ananyang’anya na kugawa madaraka. Viongozi wa serikali mikoani na wilayani wako hoi. Hawajui wafanye nini na mama huyu.
  Mmoja wa wakuu wa mikoa ameniambia, safari hii, hata kwa risasi, hatakubali kuteuliwa kuendelea na ukuu wa mkoa kama mambo yanakuwa hivi. Anadai wiki hii unampokea Baba na madai yake, wiki inayofuata anakuja mtoto naye anataka uende uwanjani kumpokea, hujakaa sawa anakuja mama, unaambiwa uhame nyumba kumpisha, siku inayofuata anakuja yule mdogo wa chipukizi, unaambiwa umsindikize mpaka aondoke mkoani kwako.
  Mkuu huyo wa mkoa anakang’aka: “Tumeteuliwa kutumikia familia”? Polisi wanapiga saluti kwa mama, mtoto Ridhiwani anadai ripoti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa? Kamati za siasa na kamati za ulinzi wanachanganyikiwa hawajui wafanye nini?
  Mpaka hapa mtu unajiuliza: Kikwete aliposema hana ubia na mtu alimaanisha nini ikiwa watoto wake wawili na mkewe wanafanya kazi za Chama na serikali kwa gharama za serikali?
  Matokeo ya ubia huu wa Kikwete na familia yake ni kusitasita kwa Kikwete kuchukua hatua muhimu za kurekebisha hali ya nchi.
  Watu wamelia, vyombo vya habari vimelalamika na ripoti kadhaa zimeandikwa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi ya mafisadi, wala rushwa, wazembe serikalini, wakwepaji kodi wakubwa, wezi wa nyara za taifa, wauza madawa ya kulevya na majambazi.
  Kusitasita kwake kunatokana na hujuma iliyo ndani ya familia yake. Maadui wa ndani ya taifa letu ambao ni mafisadi ni wajanja.
  Walipoona kelele za watu zinaanza kumwingia Kikwete na kumnyima usingizi, wakamzunguka kupitia familia yake na wanajimu. Wanajua fika hapo hawezi kunasuka. Sasa baadhi yao wamezama katika ufisadi wa kutisha. Ni Mungu tu ajuaye hatima yao.
  Kabla ya kufika mwisho wa “fitina” zangu hizi (ndivyo JK anavyoziita makala hizi), nikumbushe na kusisitiza jambo la msingi. Pamoja na wema wake na misimamo yake tata isiyompa nafasi ya kuwa mtendaji mzuri serikalini na kwenye chama, hivi sasa Kikwete ajue yafuatayo yako ukutani.
  Nitataja bila kufafanua. Kwanza, pamoja na kusita kuwachukulia hatua mafisadi, hata wao hawamtaki na hawampendi kwa sababu wanamwona ni mdhaifu asiyeweza kuwahakikishia ulinzi mbele ya wanaolalamikia ufisadi.
  Wameniambia kuwa Kikwete ni mzigo kwao na kwa taifa. Pili, Kikwete hana risasi za kuwaua Watanzania wote wanaolalamika na kuteketea kwa umaskini mbele ya utajiri wa taifa letu. Hukumu yao kuna siku itatolewa, kama si mwaka huu, basi wakati mfupi ujao.
  Na wakati huo hata kama atakuwa hayupo duniani (sote twaenda huko), hata kutemea mate picha yake, kutampa mtu usingizi wa siku moja.
  Tatu, uongozi usio na maadili huzaa mamluki wengi. Hivi sasa siri nyingi za Ikulu zimezagaa mitaani kwa sababu tu Kikwete ameruhusu Ikulu pawe pango la mafisadi, wanajimu, wafanyabiashara na matapeli. Watu wasio na maadili hawawezi kutunza siri za nchi, ndo maana hata mikataba ya siri inavuja.
  Hawa siku moja watasimama kizimbani, si kama washtakiwa, bali kama mashahidi dhidi ya uongozi wa Kikwete uliokosa mwelekeo na kushindwa
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Haya ni maneno magumu sana.
   
 3. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  umenigusa sana kwa maneno haya nimetamani kumwaga chozi jinsi nchi yangu inavyoburuzwa na huyu mkwere, hakika watanzania tusipochukua hatua sasa,hali itakuwa mbaya na ya mashaka huko mbeleni.
   
 4. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeisoma hii kwenye Raia Mwema nikatafakari sana. Hasa hapa aliposema:

  "Wameniambia kuwa Kikwete ni mzigo kwao na kwa taifa. Pili, Kikwete hana risasi za kuwaua Watanzania wote wanaolalamika na kuteketea kwa umaskini mbele ya utajiri wa taifa letu. Hukumu yao kuna siku itatolewa, kama si mwaka huu, basi wakati mfupi ujao. Na wakati huo hata kama atakuwa hayupo duniani (sote twaenda huko), hata kutemea mate picha yake, kutampa mtu usingizi wa siku moja".
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Haya ni maneno makali, ni wenye hekima tu ndio wanaweza kuona ukubwa wa tatizo lililopo kama Kikwete atapewa miaka mingine mitano ya madaraka
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Imenigusa sana MOYONI hii hoja ya Agwambo.
  Mwanakijiji upo wapi uiweke hii kwenye kijarida chetu cha CHECHE?

  Natamani asilimia 50 ya watanzania wasome hii post.

  TUIKOPI na kutuma kwenye emails na tuzibandike kwenye noticeboards zenye kupitiwa na wasomaji.
  NIMELENGWA na machozi walah sio siri
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Natamani ujumbe huu uwafikie watanzania wapiga kura mwaka huu ili wafanya uamuzi ulio sahihi
   
 8. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kweli inauma sana sijui lini watanznia watafunguka vichwani mwao ili waweze kuona jambo hili, watanzania wengi ni bendera fuata upepo ( samahani kwa kuwakwaza but hii ndio hali halisi) wanashabikia hata visivyo shabikiwa, wanashangilia hata visivyo shangiliwa wanafuata mkumbo vitu vya ajabu. Huwa najiuliza mtu mzima na akili zake na timamu anasimama tena kwa kujiamini kutetea ujinga wa hii familia huku moyoni anajua kuwa anachimba kaburi la watanzania 1000 wasiojua nini maana ya ufisadi wa familia ya mkwere kwa kila kauli yake kisa amemsifia bwana mkubwa, kweli inatia uchungu sijui ni lini tuta amka tena tuamke kwa nguvu zote kuikomboa nchi yetu iliyotawaliwa na familia ya mtu mmoja, ikiwa tuliweza kumngoa mkoloni basi hatuna budi kuamka kuingoa hii familia inayo tunyonya bila kuwa na huruma kwa wamamawajawazito wanaojifungua kwenye zahanati duni, watoto wetu wanakaa chini sakafuni, watanzania wengi wanaishi kwa chini ya dola moja wao wanatanua na rasilimali za nchi yet bila huruma, ikiwa mtu anakodi ndege kwa $ 150000 kwa masaa 5 ukiongezea msururu wa magari atumiayo akitembea mikoa 10 ya Tanzania hiyo pesa haijatosha kununua dawa, madawati kulipa wauguzi, kuboresha miundombinu ya maji safi na salama kweli inauma.

  WATANZANIA TUAMKE KWA PAMOJA BILA KUJALI ITIKADI ZETU TUINGOE HII FAMILIA INAYOTUTAWALA KAMA TULIVYO UNGANA KUWANGOA WAKOLONI.

  KWANINI TUTAWALIWE NA WAKOLONI WEUSI??? TULIWAFUKUZA WAZUNGU NA WEUSI WANAO TUTAWALA NAO TUWAFUKUZE!!
   
 9. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
 10. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa aliyesoma natumai atachukua hatua kwa kutafakari hatma ya watoto na wajukuu zake hapo baadae,imenigusa sana kiasi kwamba imenibidi niisome mara mbili na kiprint na kuisambaza kwa wenzangu watano nao wamebaki kuumia tu.
  Natumai huko Lindi mkuu wa Mkoa anaumia tu moyoni kama mtu aliyekanyagwa na kushindwa kusema NAUMIA!!!!!!!!!!
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  @Agwambo,ahsante baba au Mama utajijua mwenyewe,niliisoma waraka wako ,kwenye Raia mwema nikabubujikwa na machozi,ni kweli kabisa unavyosema Kikwete ametengeneza bomu la ajabu, lisipodhibitiwa wote sisi tutaangamia,mimi nafanya shughuli fulani ya jamii, tulimualika salma kikwete aje azindue mkanda ili tutunishe mfuko wa elimu kwa wasichana, kwa bahati mbaya hiyo shughuli ilifanyika naye alikuja lakini watu wenye majina makubwa tuliowaalika hawakuja, masaa matatu yote aliyokaa kwenye shughuli hiyo alikuwa anatukana kwamba tumempotezea muda na kama kulikuwa hakuna watu kwa nini tulimualika alivyo mswahili, alikuwa anaandika vikaratasi vya umbea vinapita kichwani kwangu kwenda kwa Regina Lowassa kwa sababu tulimualika pia, akipata jibu alikuwa anacheka kicheko cha wanawake wale wambeya
  Nilifadhaika sana moyoni mwangu kwa tabia yake hiyo mwisho aliahidi kwamba atatoa shilingi milioni moja kwa niaba ya mwanae alimtaja jina ( lakini sitataja jina lake hapa )
  Regina pia aliahiidi milioni moja baada ya siku mbili tatu hivi Regina aliuliza akaunti yetu akaandika cheki pesa ikaja,Salma hakujishughulisha tena tulipomtuma mtu wetu kufuatilia kwenye ofisi zake za WAMA kwa sababu ni ahadi aliitoa mbele ya Kadamnasi, huyo mtu alirudi ofisini kwetu akilia jinsi alivyotukanwa na msaidizi wake aliyewahi kuwa mwandishi na mtangazaji maarufu wa vyombo mbalimbali hapa nchini
  ninachotaka kusema Agwambo ni kuwa kweli huyo mama ni mkatili na asiyefaa kabisa,na anamajidai sana,kuna siku tulikutana Kwa balozi wa uingereza watu wote aliwapa mikono kuwapa salamu mimi aliruka mkono wangu,dada mmoja akaniambia limbukeni kapata amekalia ****** mbwata,anajidai kwa kuwa amevaa cheo cha mumewe
  tulienda Ikulu siku moja kwenye shughuli fulani wafanyakazi wake wa sasa wamekosa heshima sio kama wakati ule wa Raisi Mkapa ,wakati Raisi anaongea wasaidizi wake walikiuwa wanaongea wanatubughudhi mpaka sisi wasikilizaji,Kipaza sauti cha kusimama kilikuwa kinaanguka na kilikuwa kimoja Raisi akauliza kama hakuna kipaza sauti kingine kikaja kile cha wireless ,na hata mkutano ulivyoisha ni Raisi aliiuliza kama kulikuwa na kitu chochote vinywanji vilitolewa soda na juice bila vitafunwa,sio kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa kulikuwa na nidhamu pale Ikulu
  Mungu ibariki Tanzania,tuendako kugumu sana ,Wananchi wangelijua wangempumzisha Raisi Kikwete sasa
   
 12. Kiwi

  Kiwi JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 1,009
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Asante sana kwa ujumbe unaochoma. Kibinafsi nimeguswa sana na ujumbe wako. Ninamfahamu kwa karibu sana mtu mmoja aliyekuwa muasisi wa TANU na CCM. Aliwahi kuwa kwenye NEC na CC ya CCM enzi za Mwalimu. Alikuwa mmoja wa waliotembea Butiama mpaka Mwanza pamoja na Mwalimu kuunga mkono Azimio la Arusha. Na yeye pia alinieleza kwa maneno yake mwenyewe wasiwasi wake wakati JK anaingia madarakani 2005. Sikumwamini wakati ule. Leo hii anasikitika sana na ninapoongea naye majibu yake ni 'sisi tulifahamu, lakini tulinyamazishwa'.
  Inatia moyo kuona watu kama ninyi mpo, na mko tayari kusema hadharani. Hali inatisha, lakini ndiyo hali halisi. Tusinyamaze, lazima tuueleze ulimwengu. Tusipofanya hivyo vizazi vijavyo vitatuhukumu.
  Mungu Ibariki Tanzania!
   
 13. l

  liganga4 Member

  #13
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  tatizo kubwa tulilonalo wengi wetu tumefundishwa kuto fikiri wapiga kura wengi wanasoma udaku. kutokana nahilo ccm wametumia maisha ya slaa badala ya kujibu hoja. cc ambao angalau tunaona twa fungue na wengine.
  leo nilikuwa naongea na mkenya mmoja nilijsikia vibaya kwajinsi wenzetu wanvyo tuonea huruma juu ya viongozi wazembe tulionao. kenya wantoa elimu bure mpaka chuo cc raisi nakundi lake wanasema haiwezekani. mashudu yanatoka tz maya ynatoka kenya.
  :confused2:
   
Loading...