Kikwete mpaka leo hajajua kuwa yeye ndio Rais wa Tanzania, anasubiri nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete mpaka leo hajajua kuwa yeye ndio Rais wa Tanzania, anasubiri nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Arafat, Feb 5, 2011.

 1. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Nimesikitika sana kuona kuwa Kikwete mpaka leo hajui kuwa yeye ndio Rais watanzania, anajua makosa ya watendaji lakini hamna hatua zilizokwisha chukuliwa, anajua Richmond ilikuwa hewa lakini walioileta Richmond bado wapo huru na wanakula fedha za Umma wengine kama Mawaziri wengine kama Waziri Mkuu Mstaafu!!! Nani ataweza kuwachukulia hatua hawa watu kama Kikwete aliyepigiwa Mizinga 21 na kukabidhiwa Dola hawezi!! tumkimbilie nani?? kwanini hasiondoke mwenyewe kistaarabu maana kashindwa kuongoza, anajua Richmond ilikuwa hewa lakini Hoseah na PCCB waliodanganya Umma juu ya uhalali wa Richmond bado wapo wanalipwa na Umma uliodanganywa!!!, Kikwete hamjui Mmiliki wa Dowans hadi leo hii ingawa TISS ipo na DCI wanfanya ukachero gani hawa jamaa hadi leo hawajafikisha jina la Mmiliki wa Dowans mezani kwa Rais, au Ruhanjo anahujumu taarifa za kikachero?? Kikwete anakubaliana na hoja ya Dowans hisilipwe katika hotuba yake leo wakati aliitisha kikao cha CC-CCM wakaazimia Dowans ilipwe, au Rais anahujumiwa wakati wa kujadili hilo alikuwa kalala, lakini kama alikuwa amelala mbona hakumchukulia hatua Bwana Chiligati kutangaza jambo hambalo yeye halitaki??!!

  Jamani hivi kikwete yupo kweli!? Je anajua yeye ndio Rais wa Tanzania kweli!!, Kama kikwete akiendelea hivi CDM wasiwe na shaka 2015 watachukua kilaini sana. Hivi kushindwa kwa Rais siyo kushindwa kwa watendaji na vyombo vyake vikuu?? haya yote hayaonyeshi kuwa TISS imeshindwa pia?, sio kuwa Mawaziri na Makatibu wakuu pia wameshindwa??!!
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mi naona jamaa ni kama kachanganyikiwa vile!
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nadhani hayupo sawa, lakini hotuba haziandaliwi na wataalam na Makachero wapo wapi??
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  tuna rais wa mfukoni that is all
   
 5. N

  Nyang'oma Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli huyu bwana kachanganyikiwa. mwacheni avae suti suti na kula chakula cha bure kwa mara ya mwisho. Watanzania tujutie makosa ya kuwa na hawa ccm kwa muda wote huo. Hakuna political will na hata leadership miongoni mwao. Hadi inatia hasira kusikia kiongozi wa nchi anajisifia utendaji wake kwa kipimo cha misaada ya nje. Hukai na kusikia ni namna gani ya kuboresha huduma na mazingira ya hospitali zetu!!
   
 6. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  JF tuache kutafuna maneno, mmiliki wa Dowans ni Rostam, mbunge wa Igunga na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM. JK amtaje ama asimtaje sisi hapa JF tukiongelea DOWANS tunamaanisha ROSTAM
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hapo sasa wewe, umejuaje na Rais wako kashindwa kujua!!!!
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
 9. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Unataka ajitie kitanzi mwenyewe?Mengi uliyoyataja hapo nae yumo ndani,yapaswa kujua kashfa kubwa zimepewa baraka kutoka juu.
   
 10. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Siku hizi najisikia mapigo ya moyo yanaenda mbio kila nikimsikia huyu bwana akiongea, iwe kwenye tv au redio. Hana mvuto.
   
 11. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Malaria ya kichwani imempanda huyu kiongozi wetu manake hata hajielewi
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Yuko mfukoni mwake yeye mwenyewe au mfukoni mwaaaaa, Rich'mondu au mfukoni mwani mwa dowans!!! yuko mfuko upi??
   
 13. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo Tume ya uchaguzi ya CCM haiwezi kumtangaza mshindi kutoka chama kingine hata kama ameshinda. Kwa tume hiyo hata Rostam Aziz akigombea urais ataibuka na ushindi wa kishindo. Cha msingi ni kushughulikia katiba ili tupate tume huru ya uchaguzi. JK anajua kuwa yeye ndiye rais si unakumbuka siku ile wabunge wa CHADEMA walivyotoka nje alisema, hata kama hamkunichagua lakini mimi ndiyo rais wenu hakuna mwingine! Ila jamaa anafanya masihara kwenye issues za msingi. Haiingii akilini kusema hawajui wamiliki wa Dowans wakati yeye ndio mkuu wa nchi anaye miliki vyombo vyote vya usalama na intellijensia ya Mwema! Ki msingi JK ni fisadi, asiye na dhamira ya kuwaletea maendeleo watanzania zaidi ya kujinufaisha yeye, familia yake na mafisadi wenzake akina Rostam Azizi, Edward Lowassa na Mkono!
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ye alifikiri urais ni kuchekacheka tu
   
 15. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Namfahamu sana kinyonga na hasa huwa nafurahi ile tabia yake ya kubadilika badilika kulingana na mazingira. Hii humsadia sana kujificha adui.
  Zamani nilimsikia mzee mmoja akiwambia mwenzake 'usiwe kama kinyonga'. Sikumwelewa kwa maana sikuamini kuwa kuna mtu anaweza kuwa kama kinyonga; lakini sasa nimeamini kuwa mtu naweza kuwa kama kinyonga:
  Kwenye kamati kuu (JK ndiye mwenyekiti) anasema Dowans ilipwe
  Kwenye serikali - baraza la mawaziri (JK ndiye mwenyekiti) anasema Dowans ilipwe
  Kwenye jukwaa la CCM (JK ndiye mwenyekiti) anasema Dowans isilipwe
  Akibanwa kwa masuali JK anasema Dowans haijui!
  Je si 'kinyonga' huyu?
   
 16. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mtu hatari sana huyu sijui ataishi wapi baada ya hiyo miaka mitano ya kuwanyanyasa watanzania
   
 17. Mwalimu Mkuu

  Mwalimu Mkuu Member

  #17
  Feb 7, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  inauma sana, mi naona kama sisi ndo wajinga kwa kuendelea kumsikiliza huku akiwa hana lolote la maana la kutuambia!
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  nahisi alipokua anagombea aliomba nafas asiyojua kazi iliyoko mbele yake
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  tujifunze kutokana na makosa 2015
   
 20. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwani rais lazima atoke ccm? TZ bila ccm inawezekana
   
Loading...