Uchaguzi 2020 Kikwete, Mizengo Pinda na Kassim Majaliwa hamna ushawishi wowote kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, huko kwenye kampeni mlikojiingiza mnachorwa tu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,377
217,438
Nikianza na Kikwete, huyu mambo yote yalimvurugikia mwaka 2015 kutokana na kutokujiamini na uoga wake dhidi ya Lowassa, akaboronga na kupeleka nchi kushoto kwa kucheza kamari ya hatari sana na kumpa nchi mtu asiyestahili, katili na mwenye visasi vya hovyo sana ambavyo havijawahi kutokea kwenye nchi hii. Matokeo yake nchi yetu imerudi utumwani huku watu wakitekwa na kupotea katika mazingira ya hovyo sana yenye kuiletea nchi aibu duniani.

Hata hivyo Kikwete hajawahi kukemea unyama huu wa kishamba, na tangu hapo wananchi wamemdharau sana, japo ameonekana Lindi kwenye mkutano wa kampeni wa CCM, wengi hawakuguswa na uwepo wake na wanaamini alikuja mahususi kumpigia kampeni mkewe, ambaye alifikia kuwa first lady lakini sasa anaomba tena ubunge. Maajabu! Kwa kifupi Kikwete ndio aliyesababisha nchi hii kuwa hivi, wananchi hawatamsamehe.

Mizengo Pinda, huyu hana uwezo wa kumshawishi yeyote kuhusu siasa za Tanzania , hana uwezo na wala hajawahi kukemea maovu popote Tanzania, wananchi siyo Wajinga na wanazo kumbukumbu na akili timamu. Pinda alipokuwa Waziri Mkuu alimzuia Magufuli aliyekuwa Waziri wa Ujenzi kubomoa jengo la Tanesco Ubungo kwa kisingizio kwamba liko kwenye hifadhi ya barabara. Hata hivyo, baada ya Magufuli kuwa Rais akarudi tena Ubungo na kulibomoa jengo lile kiroho mbaya bila huruma na wala bila faida yoyote, Pinda aliona lakini akaufyata, mtu kama huyu anaweza kumshawishi mwananchi gani kuichagua CCM?

Kasimu Majaliwa, huyu ndio funga kazi kabisa! Hana ubunifu na wala hajawahi kuwa nao. Katika kipindi chake chote cha miaka mitano alichofanya ni kupandisha ligi kuu kimagumashi timu ya kwao inayoitwa Namungo na kutumia pesa ya umma kujenga uwanja wa soka kwao. Hana alilolifanya zaidi ya kusoma hotuba za kufunga ama kufungua bunge. Aliufyata alipoambiwa mashangazi zake watatandikwa makofi kwenye sakata la korosho, ndugu zake wakazama kwenye mafuriko huku yeye akijificha DSM.

Kwa kumbukumbu zangu huyu ndio Waziri Mkuu wa kiwango cha chini kabisa kuwahi kuwepo nchi hii, hana ubunifu wowote na kuna taarifa kwamba kwao hatakiwi kabisa na wananchi. Hii ndio sababu ya Wagombea ubunge Ruangwa wa vyama vingine kutekwa na kunyimwa fomu ili apitishwe bila kupingwa. Huyu hana uwezo wa kumshawishi mtu yeyote kuichagua CCM. Kampeni anazozifanya ni sawa na kupoteza muda tu.

Itaendelea...
 
Back
Top Bottom