Kikwete mgombea pekee?

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
Kumezuka wimbi la baadhi ya viongozi wa CCM na jumuia zake kutaka Kikwete awe mgombea pekee wa urais kupitia CCM......hivi kuna tatizo gani kumpambanisha na wana-CCM wengine wenye nia ya kugombea urais? Je, kwa mtindo huu, tunakuza au kudumaza demokrasia ndani ya CCM?
 
Kaka,

Kwa maoni yangu, kila nchi inao utamaduni wake wa kisiasa (political culture) ambao ndio unaathiri mwelekeo na mwenendo wa nchi hiyo. Hapa kwetu, utamaduni wetu ni wa awamu mbili, akijitokeza mgombea hatakatazwa lakini atapandikiza utamaduni mpya ambao ni mgeni na hivyo utaleta uamsho mpya. Sote tunafahamu si kila wakati uamsho mpya ni kitu chema, wakati mwingine huleta mtikisiko wenye athari za kitaasisi na nchi, haswa pale ambapo jamii haijaandaliwa kukubali mabadiliko hayo. Aidha, mgombea mwingine atafanya gharama za uchaguzi kuwa kubwa kwa kulazimu kufanyika duru ya kampeni ndani ya chama ya wagombea urais ambayo haitakuwa na tija zaidi ya kugawa wanachama na kukibebesha mzigo wa gharama chama na wanachama. Hii ni kutokana na hali halisi kuwa nafasi ya mgombea mwingine kumshinda mgombea urais ambaye ni Rais na Mwenyekiti wa Chama (incumbent) ni finyu mno.Demokrasia sio lengo (an end) ni matokeo (byproduct).........
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom