Elections 2010 Kikwete, mgombea binafsi kwa staili ya BMW?

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kikwete, mgombea binafsi kwa staili ya BMW?

?

Sarwed Dawalo

*

NYAKATI zimepita na majira ya uchaguzi kwa mara nyingine yamewadia hapa nchini. Uchaguzi Mkuu wa safari hii utakuwa wanne tangu siasa za vyama vingi zirejeshwe mwaka 1992.

Kwa wanasiasa, wagombea na wapiga debe, ni wakati wa vituko na kuropoka hovyo kwenye majukwaa. Na kwa wananchi wapiga kura, huu ni wakati wa kusikiliza ndoto na kughilibiwa kwa uongo usiokuwa na mashiko; kwa wenye akili kuchambua, kutafakari na mwishowe kujikusanya kifikra kwa kuchukua maamuzi yanayokidhi utashi binafsi.

Kampeni hizi zimekuwa zikiendelea kwa takriban miezi miwili sasa. Katika hali ya kawaida si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kukumbuka kila kilichoahidiwa na wagombea tofauti.

Hata hivyo, itoshe tu kusema kuwa yale yote waliosikiliza, kuona na hata kusoma magazetini hadi sasa yameshawasaidia kuunda uamuzi mioyoni mwao, sera au ahadi ipi imewakuna na mwelekeo upi maamuzi yao yatachukua.

Ni vyema tukatambua kuwa uchaguzi mkuu au mwingine wowote ni hatua ndogo katika ujenzi na kuimarisha demokrasi katika nchi. Kwa kuwa uchaguzi hutokea mara moja katika kila miaka mitano, ni vigumu kusema demokrasia ni uchaguzi pekee.

Katika hali ya kawaida na kwa wakati wote, ujenzi wa demokrasia kwenye jamii lazima ijumuishe ufahamu, uelewa, mwamko, ushiriki, ukereketwa nk. raia katika kila uamuzi ama wa pamoja au binafsi katika mambo yahusuyo maisha kwa ujumla, mtaa hadi taifa. Katika hali hiyo, demokrasia inageuka kuwa ni uhai wa kila siku wa taifa lililonawiri.

Wakati kampeni za kila chama ziko kwenye kasi ya juu, tumeweza kuona namna chama tawala, Chama Cha Mapinduzi kilivyojikita katika harakati hizo na staili ambayo wamechagua kufuata katika uchaguzi huu.

Kwa mara ya kwanza tumeona mgombea wa CCM ambaye anatetea kiti chake akipita huku na huko ‘akijinadi’ mwenyewe kama ‘mtoto mkiwa’. Jambo la kustaajabisha, wazee na viongozi wengine wastaafu wa Serikali zilizopita ambao wanavikwa heshima kubwa na Watanzania hawashiriki kampeni hizi za CCM. Mojawapo linawezekana, ama wamewekwa kando kwa makusudi au wamejiweka pembeni wenyewe.

Marais wastaafu Mwinyi na Mkapa hawapo pichani, makamu wenyeviti wa CCM, Karume na Msekwa halikadhalika. Mawaziri Wakuu wastaafu Warioba, Msuya, Sumaye na Salim gizani. Makamba, Kingunge na wengi wengineo hawajaonekana hata mara moja kwenye majukwaa ya CCM.

Amebakia hapa Dar es Salaam Abdulrahman Kinana akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM (wengi wametilia shaka kama kamati hiyo ipo kweli) kujibu hoja kwa waandishi wa habari kila inapotokea Dakta Slaa (mgombea wa CHADEMA) amerusha kombora.

Kwa ufupi, CCM safari hii imeacha kuiongoza kampeni na badala yake wamekuwa wakijibu mapigo ya Dk. Slaa tu.

Wamekuwa wakitumia muda mwingi kujitetea au kumkashifu Dakta Slaa na viongozi wengine wa upinzani. Kwa chama kilicho kubuhu kama CCM hatua hii ni ya kushangaza mno na ni ishara ya kupoteza umakini hususan kwenye ngazi ya juu ya uongozi wake.

Kwa mara ya kwanza, mgombea urais Jakaya Kikwete ameamua kuchukua hatamu za kampeni yake na kuongoza mwenyewe takriban kila idara. Tathmini nyepesi tu inaonyesha kuwa katika uchaguzi huu wa 2010, CCM imekosa mkakati madhubuti wa kushinda. Badala yake Kikwete amekuwa akipita kote na kumwaga ahadi za ajabu ajabu na ambazo uwezekano wa kuzitekeleza haupo.

Ni dhahiri kuwa hata kama nchi hii ingekuwa na utajiri wa nchi kama Marekani bado ahadi za Kikwete zingekuwa ngumu kutekelezeka. Hata hivyo, ukweli huu haujamzuia Kikwete kuendelea na ahadi zake. “Nitajenga hiki, nitafuta deni lile, nitakamilisha yale, nitawaleteeni hili nk. nk.” Kama vile kateremka leo kutoka sayari nyingine.

Kwa maono mengine, kwenye uchaguzi wa 2010 kwa kiti cha urais, CCM imesimamisha ‘mgombea binafsi’. Dalili zote zinaonyesha kuwa katika kinyang’anyiro cha urais CCM kama chama hakishiriki, ila Kikwete kama mwanachama wa CCM anagombea urais akiwa kama ‘Private Candidate’.

Kwa kuthibitisha upweke wake, Kikwete amewakabidhi kazi hiyo familia yake. Mama Salma Kikwete, mkewe, hajapumzika karibuni miezi miwili sasa. Wanawe nao akina Ridhwan wanazurura nchi nzima kumfanyia kampeni mkuu wao wa kaya.

Staili hii imekuja kujulikana kama ‘BMW’ au Baba, Mama na Watoto. Mikiki ya aina hii huioni kwenye ngazi ya chama. Ni kama vile viongozi wengine wa CCM wametulia huku wakisema ‘tuone litafika wapi’ nae Kikwete akisema ‘nitawaonyesha kuwa ninaweza na sitowahitaji’.

Ukiondoa mkakati huu wa mgombea binafsi wa CCM wenye mtazamo wa kifamilia pamoja na ahadi zisizo na mwisho, mbinu ingine ni kuongeza mabango yenye picha ya Kikwete nchi nzima. Watanzania wana ufahamu wa kuweza kumtambua Kikwete kama wakikutana naye hata usiku.

Mabango haya na hasa wingi wake unawafanya Watanzania wajinga na wasahaulifu wakubwa kiasi cha kushindwa kumtambua Rais aliewatawala kwa miaka mitano iliyopita. Aidha mabilioni yaliyotumika kuweka mabango hayo na waliofaidika na fedha hizo inawaachia maswali mengi wananchi wetu.

Hivi Kikwete (na si CCM) anaamini kweli kuwa wingi wa mabango ni hakika ya ushindi? Wanasaikolojia wamethibitisha kuwa kitu chochote ambacho umekizoea machoni kupita kiasi unakichoka na pengine hata kukichukia.

CCM ya sasa imeonyesha udhaifu wa hali ya juu kiasi kuwa hata viongozi wastaafu kadhaa wamekuwa wakilalamika hadharani kuhusu jambo hili.

Chama hiki kwa sasa kinajiendesha kimazoea na hadaa. Hadaa hii ni kwa wananchi wa kawaida wanaovaa mashati ya kijani na kucheza rhumba la TOT, huku wakiaminishwa kuwa wameegemea mbuyu hali kuwa ni kuti kavu ambalo litaanguka wakati wowote.

CCM imeingia kwenye uchaguzi huku ikinadi Ilani na sera zake, wakati kila mmoja akiionea haya katiba inayotamka kuwa Sera ya CCM ni ‘Ujamaa na Kujitegemea’. Mkengeuko mkubwa!!!

Kwa wale wachunguzi wa mambo, mashaka makubwa yamejidhihirisha kuhusiana na ufadhili wa CCM kwenye uchaguzi huu. Nikitafsiri methali ya Kiingereza ‘they are spending money like they have no hands’ yaani ‘wanamwaga fedha utafikiri hawana mikono ya kuzishika hizo fedha’.

Sasa haya ndiyo mambo yaliyo dhahiri. Ukweli kuhusu nani kapenyeza nini CCM kitajulikana muda si mrefu tangu sasa.

Matumizi mabaya ya mali za umma anayofanya Salma pamoja na kujivika uongozi wa CCM nayo pia yatakuwa bayana.

Inasemekana Salma siku hizi ana uwezo hata wa kuita viongozi wa kitaifa na wakaitika. Wanahistoria, mtujuvye ufalme huwa unaanza vipi na nini viashiria vyake?

Miezi michache iliyopita, serikali ya CCM iliweza kushinda kesi mahakamani dhidi ya mwanaharakati Christopher Mtikila, ambaye alikuwa akipigania kubadilishwa kwa sheria ili iruhusu ‘mgombea binafsi’ kwenye chaguzi zetu. Siku zote CCM wamekuwa na msimamo wa wazi kuhusu jambo hili, wanaliogopa na kulipinga kwa nguvu zote.

Kinyume chake, CCM katika uchaguzi huu imeamua kusimamisha mwanachama wake, Jakaya Kikwete, kama ‘mgombea binafsi’. Wapiga kura wamechanganyikiwa, ikitokea Kikwete kaibuka mshindi, Tanzania itatawaliwa na nani? Chama kwa maana ya CCM au mtu binafsi kwa maana ya Kikwete na familia?
?

sdawalo@yahoo.com
Source: Tanzania Daima Jumatano Oktoba 13, 2010
 
huenda huu ndio mtindo wa ccm. kama kumbukumbu zangu hazinitupi
hata mkapa alikuwa kama amesusiwa na chama wakati wa kampeni yake
kipindi cha pili, tofauti na sasa ni kwamba mkapa hakutumia mke na watoto
japokuwa kinana alikuwemo kwenye timu yake.
 
Hii nayo

"Ee KIKWETE Uliye tufilisi, Jina lako USANII
MTUPU, utakalo lifanyike BAGAMOYO TU,
utupe leo mabilioni yetu ya EPA, uwapeleke
MAFISADI wote Mahakamani, uwape
WASTAAFU pesa zao, uwasamehe wafungwa
hasa BABU SEYA kama ulivyomsamehe
LOWASA, Usitutie katika mikataba FEKI, kwa
kuwa UFISADI ni fani yako na uwongo hata
milele, na Uanguke kwenye uchaguzi ujao
kama unavyoanguka hovyo jukwaani…"
 
wazee wa kuspin bana .... haya bana umesomeka
 
Hii nayo

"Ee KIKWETE Uliye tufilisi, Jina lako USANII
MTUPU, utakalo lifanyike BAGAMOYO TU,
utupe leo mabilioni yetu ya EPA, uwapeleke
MAFISADI wote Mahakamani, uwape
WASTAAFU pesa zao, uwasamehe wafungwa
hasa BABU SEYA kama ulivyomsamehe
LOWASA, Usitutie katika mikataba FEKI, kwa
kuwa UFISADI ni fani yako na uwongo hata
milele, na Uanguke kwenye uchaguzi ujao
kama unavyoanguka hovyo jukwaani…"

STOP!!!!!!
UMEVUNJA MASHARTI YA USHAIRI, HUNA HAKI KUTUWEKEA SHAIRI LISILO NA MUELEKEO! SHAIRI LAKO NI BOMU TUPU MAANA HALINA BETI, VINA WALA MIZANI.

KAMA MARA NYINGINE UTATAKA KUTUWEKEA SHAIRI LAKO HAPA JF HUNA BUDI KUZINGATIA MASHARTI YA KUANDIKA SHAIRI!!
UNAWEZA KUJIFUNZA NAMNA YA KUANDIKA SHAIRI KWA KUPITIA SHULE HII HAPA: http://gskool.com/n/node/140
 
ANGALIA MFANO WA SHAIRI MURUWA:

Nakuombea kwa Mungu, akupege afya njema,
Akulipe lako fungu, leo na kesho kiama,
Asije kupa machungu, duniani kulalama,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Hongera kwa kuchukua, bila mtu kukukera,
Fomu ya chama sikia, hivyo ndiyo barabara,
Na sisi tunakwambia, kwa hakika unang‘ara,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Hongera twakupa heko, kukubali kugombea,
Kwetu sisi ni kicheko, daima twakuombea,
Na hatuna mshituko, ushindi tajibebea,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Kikwete baba sikia, twakuombea Rabuka,
Hilo tunakuambia, usijekuwa na shaka,
Kura tutakutilia, Ikulu tutakuweka,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Ikulu utarejea, kwa hilo tuna hakika,
Dua tunaitikia, usijeingia shaka,
Ubaki huko kwa nia, Slaa asije fika,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Na sera za chama chako, ni nzuri twakuambia,
Shule nyingi zikiwemo, wanyonge twafurahia,
Tutakuwa na kicheko, katika hii dunia,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Umaskini kwaheri, hapa kwetu Tanzania,
Amani ilishafika, wote tunafurahia,
Taishi kwa uhakika, mazao tajivunia,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Ukabila utaisha, kwa wananchi sikia,
Kwa furaha na bashasha, mashambani taingia,
Nasi tutaimarisha, uchumi taendelea,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Wewe mkombozi wetu, wanyonge tatutetea,
Wewe ndiye ngao yetu, hapa petu Tanzania,
Wewe ndo kioo chetu, tunachojiangalia,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Naweka kalamu chini, hapa ninaishilia,
Imeningia huzuni, tungo hizi kuishia,
Sijui nifanye nini, hamu haijanishia,

Nimelipenda zaidi la Invicible.
 
Ile ilikuwa sala sio shairi!!!
 
Mmmh! hamna lolote!
 
kikwete, mgombea binafsi kwa staili ya bmw?

?

Sarwed dawalo

*

nyakati zimepita na majira ya uchaguzi kwa mara nyingine yamewadia hapa nchini. Uchaguzi mkuu wa safari hii utakuwa wanne tangu siasa za vyama vingi zirejeshwe mwaka 1992.

Kwa wanasiasa, wagombea na wapiga debe, ni wakati wa vituko na kuropoka hovyo kwenye majukwaa. Na kwa wananchi wapiga kura, huu ni wakati wa kusikiliza ndoto na kughilibiwa kwa uongo usiokuwa na mashiko; kwa wenye akili kuchambua, kutafakari na mwishowe kujikusanya kifikra kwa kuchukua maamuzi yanayokidhi utashi binafsi.

Kampeni hizi zimekuwa zikiendelea kwa takriban miezi miwili sasa. Katika hali ya kawaida si rahisi kwa mwananchi wa kawaida kukumbuka kila kilichoahidiwa na wagombea tofauti.

Hata hivyo, itoshe tu kusema kuwa yale yote waliosikiliza, kuona na hata kusoma magazetini hadi sasa yameshawasaidia kuunda uamuzi mioyoni mwao, sera au ahadi ipi imewakuna na mwelekeo upi maamuzi yao yatachukua.

Ni vyema tukatambua kuwa uchaguzi mkuu au mwingine wowote ni hatua ndogo katika ujenzi na kuimarisha demokrasi katika nchi. Kwa kuwa uchaguzi hutokea mara moja katika kila miaka mitano, ni vigumu kusema demokrasia ni uchaguzi pekee.

Katika hali ya kawaida na kwa wakati wote, ujenzi wa demokrasia kwenye jamii lazima ijumuishe ufahamu, uelewa, mwamko, ushiriki, ukereketwa nk. Raia katika kila uamuzi ama wa pamoja au binafsi katika mambo yahusuyo maisha kwa ujumla, mtaa hadi taifa. Katika hali hiyo, demokrasia inageuka kuwa ni uhai wa kila siku wa taifa lililonawiri.

Wakati kampeni za kila chama ziko kwenye kasi ya juu, tumeweza kuona namna chama tawala, chama cha mapinduzi kilivyojikita katika harakati hizo na staili ambayo wamechagua kufuata katika uchaguzi huu.

Kwa mara ya kwanza tumeona mgombea wa ccm ambaye anatetea kiti chake akipita huku na huko ‘akijinadi' mwenyewe kama ‘mtoto mkiwa'. Jambo la kustaajabisha, wazee na viongozi wengine wastaafu wa serikali zilizopita ambao wanavikwa heshima kubwa na watanzania hawashiriki kampeni hizi za ccm. Mojawapo linawezekana, ama wamewekwa kando kwa makusudi au wamejiweka pembeni wenyewe.

Marais wastaafu mwinyi na mkapa hawapo pichani, makamu wenyeviti wa ccm, karume na msekwa halikadhalika. Mawaziri wakuu wastaafu warioba, msuya, sumaye na salim gizani. Makamba, kingunge na wengi wengineo hawajaonekana hata mara moja kwenye majukwaa ya ccm.

Amebakia hapa dar es salaam abdulrahman kinana akiwa kama mwenyekiti wa kamati ya kampeni ya ccm (wengi wametilia shaka kama kamati hiyo ipo kweli) kujibu hoja kwa waandishi wa habari kila inapotokea dakta slaa (mgombea wa chadema) amerusha kombora.

Kwa ufupi, ccm safari hii imeacha kuiongoza kampeni na badala yake wamekuwa wakijibu mapigo ya dk. Slaa tu.

Wamekuwa wakitumia muda mwingi kujitetea au kumkashifu dakta slaa na viongozi wengine wa upinzani. Kwa chama kilicho kubuhu kama ccm hatua hii ni ya kushangaza mno na ni ishara ya kupoteza umakini hususan kwenye ngazi ya juu ya uongozi wake.

Kwa mara ya kwanza, mgombea urais jakaya kikwete ameamua kuchukua hatamu za kampeni yake na kuongoza mwenyewe takriban kila idara. Tathmini nyepesi tu inaonyesha kuwa katika uchaguzi huu wa 2010, ccm imekosa mkakati madhubuti wa kushinda. Badala yake kikwete amekuwa akipita kote na kumwaga ahadi za ajabu ajabu na ambazo uwezekano wa kuzitekeleza haupo.

Ni dhahiri kuwa hata kama nchi hii ingekuwa na utajiri wa nchi kama marekani bado ahadi za kikwete zingekuwa ngumu kutekelezeka. Hata hivyo, ukweli huu haujamzuia kikwete kuendelea na ahadi zake. "nitajenga hiki, nitafuta deni lile, nitakamilisha yale, nitawaleteeni hili nk. Nk." kama vile kateremka leo kutoka sayari nyingine.

Kwa maono mengine, kwenye uchaguzi wa 2010 kwa kiti cha urais, ccm imesimamisha ‘mgombea binafsi'. Dalili zote zinaonyesha kuwa katika kinyang'anyiro cha urais ccm kama chama hakishiriki, ila kikwete kama mwanachama wa ccm anagombea urais akiwa kama ‘private candidate'.

Kwa kuthibitisha upweke wake, kikwete amewakabidhi kazi hiyo familia yake. Mama salma kikwete, mkewe, hajapumzika karibuni miezi miwili sasa. Wanawe nao akina ridhwan wanazurura nchi nzima kumfanyia kampeni mkuu wao wa kaya.

Staili hii imekuja kujulikana kama ‘bmw' au baba, mama na watoto. Mikiki ya aina hii huioni kwenye ngazi ya chama. Ni kama vile viongozi wengine wa ccm wametulia huku wakisema ‘tuone litafika wapi' nae kikwete akisema ‘nitawaonyesha kuwa ninaweza na sitowahitaji'.

Ukiondoa mkakati huu wa mgombea binafsi wa ccm wenye mtazamo wa kifamilia pamoja na ahadi zisizo na mwisho, mbinu ingine ni kuongeza mabango yenye picha ya kikwete nchi nzima. Watanzania wana ufahamu wa kuweza kumtambua kikwete kama wakikutana naye hata usiku.

Mabango haya na hasa wingi wake unawafanya watanzania wajinga na wasahaulifu wakubwa kiasi cha kushindwa kumtambua rais aliewatawala kwa miaka mitano iliyopita. Aidha mabilioni yaliyotumika kuweka mabango hayo na waliofaidika na fedha hizo inawaachia maswali mengi wananchi wetu.

Hivi kikwete (na si ccm) anaamini kweli kuwa wingi wa mabango ni hakika ya ushindi? Wanasaikolojia wamethibitisha kuwa kitu chochote ambacho umekizoea machoni kupita kiasi unakichoka na pengine hata kukichukia.

Ccm ya sasa imeonyesha udhaifu wa hali ya juu kiasi kuwa hata viongozi wastaafu kadhaa wamekuwa wakilalamika hadharani kuhusu jambo hili.

Chama hiki kwa sasa kinajiendesha kimazoea na hadaa. Hadaa hii ni kwa wananchi wa kawaida wanaovaa mashati ya kijani na kucheza rhumba la tot, huku wakiaminishwa kuwa wameegemea mbuyu hali kuwa ni kuti kavu ambalo litaanguka wakati wowote.

Ccm imeingia kwenye uchaguzi huku ikinadi ilani na sera zake, wakati kila mmoja akiionea haya katiba inayotamka kuwa sera ya ccm ni ‘ujamaa na kujitegemea'. Mkengeuko mkubwa!!!

Kwa wale wachunguzi wa mambo, mashaka makubwa yamejidhihirisha kuhusiana na ufadhili wa ccm kwenye uchaguzi huu. Nikitafsiri methali ya kiingereza ‘they are spending money like they have no hands' yaani ‘wanamwaga fedha utafikiri hawana mikono ya kuzishika hizo fedha'.

Sasa haya ndiyo mambo yaliyo dhahiri. Ukweli kuhusu nani kapenyeza nini ccm kitajulikana muda si mrefu tangu sasa.

Matumizi mabaya ya mali za umma anayofanya salma pamoja na kujivika uongozi wa ccm nayo pia yatakuwa bayana.

Inasemekana salma siku hizi ana uwezo hata wa kuita viongozi wa kitaifa na wakaitika. Wanahistoria, mtujuvye ufalme huwa unaanza vipi na nini viashiria vyake?

Miezi michache iliyopita, serikali ya ccm iliweza kushinda kesi mahakamani dhidi ya mwanaharakati christopher mtikila, ambaye alikuwa akipigania kubadilishwa kwa sheria ili iruhusu ‘mgombea binafsi' kwenye chaguzi zetu. Siku zote ccm wamekuwa na msimamo wa wazi kuhusu jambo hili, wanaliogopa na kulipinga kwa nguvu zote.

Kinyume chake, ccm katika uchaguzi huu imeamua kusimamisha mwanachama wake, jakaya kikwete, kama ‘mgombea binafsi'. Wapiga kura wamechanganyikiwa, ikitokea kikwete kaibuka mshindi, tanzania itatawaliwa na nani? chama kwa maana ya ccm au mtu binafsi kwa maana ya kikwete na familia?
?

sdawalo@yahoo.com
source: Tanzania daima jumatano oktoba 13, 2010

ccm kama chama kilishakufa miaka mingi iliyopita, ndio maana ya hali hiyo. Kama ni mikutano imebaka katika ngazi ya taifa tena ikifanyika ikulu ikiashiria kuwa ni cham dola.. Yetu macho!!!!
 
kwa maono mengine, kwenye uchaguzi wa 2010 kwa kiti cha urais, ccm imesimamisha ‘mgombea binafsi'. Dalili zote zinaonyesha kuwa katika kinyang'anyiro cha urais ccm kama chama hakishiriki, ila kikwete kama mwanachama wa ccm anagombea urais akiwa kama ‘private candidate'.

Kwa kuthibitisha upweke wake, kikwete amewakabidhi kazi hiyo familia yake. Mama salma kikwete, mkewe, hajapumzika karibuni miezi miwili sasa. Wanawe nao akina ridhwan wanazurura nchi nzima kumfanyia kampeni mkuu wao wa kaya.

Staili hii imekuja kujulikana kama ‘bmw' au baba, mama na watoto. Mikiki ya aina hii huioni kwenye ngazi ya chama. Ni kama vile viongozi wengine wa ccm wametulia huku wakisema ‘tuone litafika wapi' nae kikwete akisema ‘nitawaonyesha kuwa ninaweza na sitowahitaji'.

chema cha dr. Slaa chajiuza na kibaya cha jk chajitembezaaaaaaaaaaaaaaa
 
ANGALIA MFANO WA SHAIRI MURUWA:

Nakuombea kwa Mungu, akupege afya njema,
Akulipe lako fungu, leo na kesho kiama,
Asije kupa machungu, duniani kulalama,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Naweka kalamu chini, hapa ninaishilia,
Imeningia huzuni, tungo hizi kuishia,
Sijui nifanye nini, hamu haijanishia,
Hongera baba hongera, kikwete twakuombea.

Siyo tu vina na mizani umekosea, lakini sikuona MAUDHUI ya utumbo huu
 
Watanzania wakati umefika kwa maendeleo ya ukweli na hakuna chama kingine kitakachokuja kuleta maendeleo zaidi ya CCM, maneno siku zote hayavunji mfupa, tushikamane kwa maendeleo ya Taifa letu na CCM ndio chaguo la watanzania, acha matendo yachukue nafasi yake, CCM hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom