Kikwete mbona siku hizi kifua kikubwa na unazungukwa na walinzi kibao unaogopa nini?

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
401
Namshangaa sana kikwete tangu ashike madaraka kifua chake kimetuna as if ni mnyanyua vyuma. Kana kwamba hiyo haitoshi, siku anazungukwa na walinzi wengi waliovaa kiraia. Hivi anachoogopa ni nini kama yeye ni MAN OF THE PEOPLE. Kuna wakati makamba alisema kikwete ni kipenzi cha watanzania. Kama ndivyo, sasa kwa nini anakuwa mwoga kiasi hicho?
 
hata papa benedict xvi analindwa, itakuwa rais wa tanzania bwana anayeandamwa na kashfa serikalini mwake?
 
ukiwa mwizi lazima ujilinde..we si umeona waziri mkuu wa UK anakata mitaa tu spain wala hana wasiwasi..sasa wa kwetu huyu kila saa anakumbuka kura alizoiba anaona kama kuna watu wanamnyemelea wampige ngeta
 
Hahahahahaa, ni ulaji tu wa walinzi ndo wanalazimisha kujipa ajira. Akitembea mitaani hakuna hata mtu atakaye pay attention, sana sana mitaa fulani atazomewa
 
Hahahahahaa, ni ulaji tu wa walinzi ndo wanalazimisha kujipa ajira. Akitembea mitaani hakuna hata mtu atakaye pay attention, sana sana mitaa fulani atazomewa

Nakubaliana nanyi wote kwamba ni mwizi wa kura kwa hiyo anaogopa atapigwa kama kibaka kwa kuiba kura za kitanzania.
 
hata papa benedict xvi analindwa, itakuwa rais wa tanzania bwana anayeandamwa na kashfa serikalini mwake?

Uasi uko palepale maana Marais wengi waliouliwa waliuliwa na Walinzi wao! Kama haohao ndio wanaotoa siri zake watashindwaje kummaliza? Tutaona wacha mambo yawe tight, kamba aliyoiandaa itamtundika mwenyewe na shimo alilochimba atatumbukia mwenyewe!
 
MWANANCHI UKITAKA KUJUA KAMA NCHI YETU INAIBIWA AU LAA WEWE ANGALIA TU KAMA RAIS WAKO ANA-COMPLICATE MAISHA VISIVYO KAWAIDA AU HAPANA

Ni kawaida sana tu kugongana mitaani na Mzee Ruksa sawa tu na Watanzania wa kawaida tu.

Hili la Ufalme wa rais Kikwete nchini mpaka mtu hata kupaki tu gari pale Chuo Cha Serikali Magogoni si ruksa wenzenu sote tumewazwa huu utamaduni mpya Tanzania na gamba la kuvimbisha kifua muda wote kama Anold Swezzineger wa Marekani muda wote na misafara mirefu ajabu haijawahi kutokea nchini!!!!!!!!!!!

Hata hivyo mie nimepata kitu kujifunza hapo kwa ukitaka kujua kama nchi yako inaibiwa kwa ushirikiano wa karibu toka ikuluni kwetu wala mtu usijisumbue kuunda tume; wewe angalia tu jinsi rais wako anavyo-complicate maisha na mazingira jirani yake.

Wengine hutuambia kwamba BMW kila mara alikua anajiendea tu mwenyewe hivi hivi kushinda kwa kaka yake pale Kinondoni Komakoma wakipiga gumzo mambo ya nyumba kwao tu.

Naye Mwalimu Nyerere ndio hivo tumepata kusikia kwamba likua ni wa kawaida kabisa hata kupanga foleni kama Mtanzania yeyote yule pindi anapoenda kutafuta huduma mahala. Kwa mtaji wa tabia za kujishusha sana kwa Mwalimu, Prof Achebe kamuandika vizuri sana katika kitabu chake cha hivi karibuni tu hasa pale alipoenda kuomba shuleni wanakosoma wanaye ili uongozi wa shule umruhusu kulipa karo ilikua ikidaiwa walau kwa kidogo kidogo kwa kuwa watoto walikua ni wengi kidogo na mshahara wake mdogo.

Kweli huu usultani uliokithiri kwa huyu mwenzetu, mhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Hivi papa atakua na ufuasi mkubwa kiasi gani vile ukilinganishwa na rais wa hapa kwetu Bongo??????????????

hata papa benedict xvi analindwa, itakuwa rais wa tanzania bwana anayeandamwa na kashfa serikalini mwake?
 
KAKAAAA KUNA KITU KINAITWAAAA...."PROTOCAL'' HATA KAMA NI MKEO... UTAPEWA SIKU ZA KULALA NAE....!!!!!! ONLY IF SHE LEADS THE STATE n YOU ARE THE 1ST MAN............ RAIS LAZIMA ALINDWE
 
Huo mtuno, mhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bullet proof Vest!! ..uraisi mtamu na maisha matamu...jinsi wale walinzi walivyo wazembe ameamua kujilinda
Remember alivamiwa jukwaani huko usukumani
Huwa akidondoka hawawahi kumdaka
Hata Mzee Ruksa aliwahi kupigwa kibao high table
 
KAKAAAA KUNA KITU KINAITWAAAA...."PROTOCAL'' HATA KAMA NI MKEO... UTAPEWA SIKU ZA KULALA NAE....!!!!!! ONLY IF SHE LEADS THE STATE n YOU ARE THE 1ST MAN............ RAIS LAZIMA ALINDWE

Tafadhali.,mke wangu afu wanipangie....,ndo maana yule wa mume wa VP wa UG walishindwana...
 
Tutajieni Rais gani Duniani asielindwa?? kama kulindwa ni kigezo cha kuchakachua Kura basi Obama ndo mchakachuaji mkuu!!! JK ni Rais mbovu but nasi tusiruhusu kuwa wabovu kwa kumpima kwa vigezo vibovu,Ulinzi wa Rais has nothing to do with our life, thread za kijinga kama hizo pelekeni kwenye blog za kina shigongo hapa ni makazi ya Great thinkers, muwe na adabu japo ya maigizo kwa muda!!!!
 
That's news to me~hivi Obama aliiba kura?.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom