Kikwete: Mapinduzi ya kilimo ni muhimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete: Mapinduzi ya kilimo ni muhimu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mzeewabusara, Jun 10, 2006.

 1. m

  mzeewabusara Member

  #1
  Jun 10, 2006
  Joined: Jun 7, 2006
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakati Mheshimiwa Mkapa anamaliza uongozi wake alikiri kuwa eneo mojawapo ambalo halikupewa umuhimu katika uongozi wake ni KILIMO. Kutokana na jinsi Mheshimiwa Raisi Kikwete alivyoanza katika kasi yake bado sijaona kama kweli suala la kilimo limo sana katika ajenda. Hivyo napenda kutoa ushauri ufuatao.
  1. Mabadiliko makubwa ya uongozi wa wizara ya kilimo yanatakiwa ili kupata viongozi watakaoweza kubuni na kuanzisha mikakati mipya ya kilimo. Nasikia waziri aliyepo sasa hakufanya vizuri katika wizara ya elimu aliyoongoza kabla ya hii. Kama ni hivyo Mheshimiwa Kikwete ni vema ukaliona hili na kufanya mabadiliko mapema.

  2. Wizara ya kilimo iandae sera na mikakati ya umwagiliaji wa maji

  3. Wizara ikaribishe wawekezaji wakubwa wa kilimo kama wale waliokuwa wakilima Zimbabwe na tuwatie moyo matajiri wa Tanzania kuwekeza katika kilimo.

  4. Serikali ianzishe programme ambazo zitahamasisha vijana kupenda kilimo badala ya kuuza karanga na korosho pale chalinze. Hii inawezekana mfano kwa kuwa na mashamba makubwa ambayo yataajiri vijana kwa kazi mbalimbali za kilimo. Hii inawezekana .

  5. Mwisho Tanzania kama tunataka kupiga hatua at least ya kuhakikisha tuna chakula chetu wenyewe suala la kilimo NI MUHIMU SANA. Mtazamo wangu hadi sasa naona serikali bado haijaupa mkazo kilimo.

  Wana bodi naomba tujadili na kutoa mawazo yetu ili nchi yetu yenye mito maziwa isiwe tena ni nchi ya njaa na ombaomba. Inatia aibu jamani.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jun 11, 2006
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  MzeewaBusara,
  Hakuna sehemu hata moja Mkapa alifanya la maana!...
  Ukimyima mtu chakula atapata wapi nguvu ya kujenga nchi?... Labda tuseme kuwanyima watu kula kumetajirisha wengine na ndio mafanikio aliyokuwa akiyataka yeye!.
  Unajuwa kuna mshikaji wangu mmoja alinunua kiwanja Mbezi miaka ya 80's tulimwona kafanya la maana sana lakini mshikaji huyohuyo hakuwa na plan ya kujenga kabisa. Leo hii kiwanja hichoi kimesimama nyumba ya mtu mwingine na kibali chake kinaonekana kuwa ndicho feki...
  Hii ni mifano ya Mkapa na mikataba yake.... tunashindwa kuchukua IPTL na tutakuja shindwa Netgroup, Songo, Barricks na kwingineko kote kwa sababu wananchi walikubali mikataba hiyo kutokana na njaa!
   
 3. s

  sumar Member

  #3
  Jul 6, 2008
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni serikali kujifanya wajuwaji. Mkulima ndio mwenye kuijuwa adha ya kazi yake. Lazima ahusishwe moja kwa moja. Tatizo kubwa la mkulima ni soko lenye kulipa vizuri kwa tija muafaka. Kwanza iko haja ya kuanzisha 'serious enterprices' zitakazo tumia mazao ya wakulima kwa wingi. Lazima kuwe na 'balance' ya uzalishaji na matumizi. Jaribu kupanda 'tomato' uione adha. Nenda Kariako kaone wachuzi wanavyo ya kimbia mafuso kwa kushindwa kuwalipa malipo ya uchukuzi wao kwa sababu ya kukosa bei muafaka yenye angalau kuweza kulipa nauli na gharama nyengine ndogo ndogo.

  Jembe la mkono nalo limepitwa na wakati. Kila kijiji lazima wawe na tractor kubwa au dogo na elimu ya kilimo cha kisasa. Kusanya haya mawili pamoja na soko la uhakika njaa-umaskini kwaheri.
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa katika kilimo Tanzania sio uzalishaji bali ni storage facilities.Ndio maana kuna lugha kama "msimu wa maembe" etc. Kipau mbele kitolewe kwenye kuboresha storage facilities, serikali ishirikiane na SUA kuwaelimisha wananchi juu ya njia affordable za kuhifadhi chakula, that way mkulima hatalazimika kuuza kwa farm-gate price na atakuwa na uwezo wa kununua pembejeo bora na hapo ndipo kilimo kitakapopata heshima na kuendelea.
   
 5. m

  miminimkulimaakachekasana Senior Member

  #5
  Jun 29, 2017
  Joined: May 29, 2017
  Messages: 196
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 80
  da ni kweli haisee
   
Loading...