Kikwete, Magufuli na mtu huyu wa tatu...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,226
116,839
Tunasahau haraka tu.

Hata wakati wa mwanzo wa Kikwete bunge lilimtimua Zitto Kabwe sababu ya kuhoji tu Buzwagi imejirudia tu...

Wakati wa Kikwete pia matamko ya kuzuia maandamano na siasa za upinzani yalikuwepo tele, Wakati huu wa Magufuli ni kama marudio tu na kuzidisha kidogo

Ukichunguza utagundua kuna 'mtu wa tatu' ambaye haonekani kwa macho ambaye ndo kama 'mshauri mkuu wa marais wetu'
au 'de facto power behind power'....ambae kila rais lazima 'amsikilize'.

Hata wakati wa Mkapa yalitokea haya hasa la Bunge kubanwa banwa hotuba za wapinzani kufunikwa na media na kadhalika.

Mtu aliewapa wapinzani sauti wala hakuwa Kikwete....alikuwa Samuel Sitta...

na wote tunajua 'alipoishia'.

Tujiulize mbona watu wanabadilika..... mawaziri na marais lakini 'huu mfumo' haubadiliki?

Kila Rais atautetea muungano kwa nguvu zote hata kwa gharama za maisha ya watu.

Kila Rais hataki kabisa demokrasia ya vyama vingi istawi vya kutosha. kila Rais atajaribu kulibana bunge ....tusisahau hawa marais ni watu tofauti wenye utashi tofauti....lakini kuna vitu 'havibadiliki'....

Huyu mtu wa tatu ni nani? au ni kina nani?
 
Kwa Kikwete kumbukumbu zangu hazioneshi kawa upinzani ulibanwa ndiyo kipindi ambacho upinzani umepata nguvu hata wenyewe wanajua

Umesahau tu...
Hata kutolewa Samuel Sitta akawekwa Makinda ni sababu Sitta 'aliwapa' wapinzani sauti..

Makinda alibadili mambo mengi tu hata namna ya kuunda kamati za bunge

Makinda kuna kamati alimteua tu Chenge
 
Serikali nyingi zinaendeshwa kishetani so mtu wa tatu wanamjua wao tu.

We si ulimsikia Obama kuwa nikiingia tu nafunga Guantanamo but now anaondoka bado ipo!!

Watu wanasemaga kuwa all the presidents are puppets of someone"..."

Wanakuwaga pale kama mapazia na nivitu vichache ndio wanaweza kuvisemea.
Kwani Magu ameishiaje na wafanyabiashara wa SUKARI?? Hivi iligaiwa ile?? Elekezi ikatoka 1800 mpk 2200.

Kuna watu ni zaidi ya Rais they r just there to control stuff.

Kama ambavyo Kennedy hawakukubaliana na mambo yake jinsi anavyoongoza wakamtungua..

So I dnt think ni mtu Bali ni kundi LA watu.
 
Tunasahau haraka tu..
hata wakati wa mwanzo wa Kikwete bunge lilimtimua Zitto Kabwe
sababu ya kuhoji tu Buzwagi...
imejirudia tu....

Wakati wa Kikwete pia matamko ya kuzuia maandamano na siasa za upinzani
yalikuwepo tele....Wakati huu wa Magufuli ni kama marudio tu na kuzidisha kidogo

Ukichunguza utagundua kuna 'mtu wa tatu' ambae haonekani kwa macho
ambae ndo kama 'mshauri mkuu wa marais wetu'
au 'de facto power behind power'....ambae kila rais lazima 'amsikilize'....

Hata wakati wa Mkapa yalitokea haya hasa la Bunge kubanwa banwa
hotuba za wapinzani kufunikwa na media na kadhalika......

Mtu aliewapa wapinzani sauti wala hakuwa Kikwete....alikuwa Samuel Sitta.....

na wote tunajua 'alipoishia'........

Tujiulize mbona watu wanabadilika.....mawaziri na marais lakini 'huu mfumo' haubadiliki?

Kila Rais atautetea muungano kwa nguvu zote hata kwa gharama za maisha ya watu
kila Rais hataki kabisa demokrasia ya vyama vingi istawi vya kutosha
kila Rais atajaribu kulibana bunge ....tusisahau hawa marais ni watu tofauti
wenye utashi tofauti....lakini kuna vitu 'havibadiliki'....

Huyu mtu wa tatu ni nani? au ni kina nani?
The boss, the analyst, the intelligent.
 
Kwa bahati mbaya Marais wetu wote hawakuwa wamejiandaa au kuamini kuwa watakuja kuzipata hizo nafasi, somehow wakaamini ile si kazi kubwa sana. Na bila shaka wakaamini aliyepo madarakani ni Kiongozi mbovu.

Kwa mazingira kama hayo unapopata madaraka mwanzoni unafanya mambo mengi, unapata sifa nyingi lakini baadaye unagundua kumbe kazi ni ngumu zaidi, unaweza kupoteza hata kile kidogo ulichonacho. Hapo ndipo ruling class wanapoingia "kumwonyesha" Mkuu namna ya kuzima wapiga kelele wasiharibu mambo.
 
There is "the president and "the presidency".

Presidents change with time but the presidency is always the same. In African countries the presidency are the self chosen few that hold the strings and call the shots, they have been in existence ever since any country becomes a republic.

These are the smiling faces we see with so much respect but in reality they are the working hands behind the president and all that goes on.

Sadly these few are operating in a hereditary manner in the sense that their policies and mode of operation is passed through heirs and heirs like a monarchy.

The fact that they are unknown it makes it rather difficult to break them so the bitter truth is no matter who rules this nation the mode of ruling will for a very very very long time be the same.
 
Mtu huyo tumekuwa nae, miaka ya nyuma alifanya kazi nzuri ya kiushauri, wakati ule ushauri wake kisiasa ulikuwa sahihi sana,kwa sasa analinda yale yaliyojengwa miaka ya nyuma, ila ameshindwa kuyasoma mabadiiko au anaona akiyakubali ataondolewa heshima/nguvu yake, anafanana na watu wa mashariki, pengine ufahamu wake ulitokana na ulaya mashariki ya zamani.

kwakuwa yuko gizani huwa halaumiwi,ila mwenendo wake kwa miaka ya sasa unaondoa uwazi na demokrasia, zama zake za kilele demokrasia hakikuwa kitu cha msingi, ana uzalendo ila kwa wachache. The Boss hii mada yako imenitoa nje ya mstari!! ngoja nisubiri wajuzi
 
Back
Top Bottom