Sn2139
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 834
- 250
Ina maana tume ya Mwakyembe wote ni wapumbavu na kazi waliyoifanya ni kazi bure?. Sasa kama Lowasa ni msafi kwanini JK alikubali na kubariki kujiuzulu kwa Lowasa?.
Ndugu zangu watanzania, nchi si yetu sote bali ni mali ya watu wachache sana. Wanafanya wapendacho na wako juu ya sheria.
Ni ukweli usiofichika kwamba watanzania wenye mapenzi ya kweli ya nchi yao wameshangazwa na kauli hii ya Jakaya (Lowasa ni MSAFI).
Tunakokwenda ni kubaya, itafika wakati watanzania wataanza kuvaa mabomu na kujilipua ama kulipua mali za mafisadi na familia zao.
Kwanini nilizaliwa mtanzania?
Hii ni kudharau bunge lote la jamhuri lililokubaliana kwa pamoja ELowasa ajiuzuru kwa sababu ya kuhusishwa katika kashfa ya Ricmond. Rais asiyeheshimu bunge ni hatari sana...ni rais asiyeweza kufuata utawala wa sheria.
Kwakweli Wa-Tz wenzangu huenda kwa maneno yetu makali na yanayoonesha chuki dhidi ya ufisadi hayatasaidia sana katika harakati za kuinasua nchi yetu kutoka mikono ya mafisadi. Nimeona na kusikia watu wengi ama kwa kujua au kutofahamu wanapenda kabisa kikwete ashinde. Yaani hawaoni kama Dr Slaa ni mkombozi wa nchi yetu kama tunavomuona siye.
Kutokana na hali hiyo nadhani itakuwa vizuri kama tukimshirikisha Mungu.
Chuki peke yake dhidi ya ufisadi inaweza kupandisha BP yako na ukafia ndani ya chumba chako peke yako. Na mtu akifa kwa sababu ya hasira dhidi ya ufisadi haina msaada sana katika harakati za kuikomboa nchi yetu kutoka kwa wezi wachache. Nawashauri watu waombe kwa Mungu, kila mtu kwa imani yake. Mungu anaweza kuleta mageuzi tunayotamani. Yeye huwainuwa wafalme na kuwashusha chini waovu. Nina imani kabisa kwamba Kikwete hakubaliki, hata mbele za Mungu, kama ilivyo kwa wanadamu hivi sasa. Mungu asipoingilia kati, pesa ina nguvu kuweza kununua kitu chochote hapa duniani kasoro uzima. Kumbukeni zile bilioni 50 .... lakini, mafisadi wapo tayari ku-spend hata mara tatu ya hiyo pesa ili kunusuru hatima yao. Hii kwa mafisadi ni struggle for survival. Ukweli ndio huo...