Kikwete kwenye Tanuru: Kujaribiwa kwa Kiongozi

Najaribu kutafakari haya maneno yalioandikwa na Mtoto wa Chami.....
"I must say, you will never be known as the man who changed Tanzania. You will be known as the man who was too much of a coward to face the liars, the corrupt and the exploiters who ruin this country. No one will remember you when you are gone".
 
Ingawa najua JK ataongea yale yale yanayotegemewa na ambayo baadhi ya agents wa dola wameshayasema. Hawa ni pamoja na Mzindakaya na Kasesela kwenye TBC jana usiku na baadhi ya watu waliokuwa kwenye Star TV leo asubuhi....

Hata hivyo, natamani angechungulia path ya Pinda...

Mwanzo alitoa vitisho vya kuwafukuza madaktari, next akawaangukia na kuwaomba warudi kazini na kwamba serikali imakubali kushughulikia madai yao...recently amegeuka na kueleza uongo kuwa wana madai mapya na kukwamisha mjadala....Kwa ufupi, amepoteza opportunity ya kumaliza mgogoro.

JK naye atakubali kuitumia nafasi ya leo kutatua tatizo au ndo atawasha moto zaidi?
 
Bila saha washauri wake wameshayasoma haya pia. Sasa msikosee kumshauri tena. Leo ndiyo karata ya mwisho kwa wananchi kuendelea kuwa na imani na serikali yetu.

Lyimo: Ili kuepuka pressure kupanda watanzania ni bora tutarajie taarifa mbaya leo.

Kama kuna rais amekuwa akipata bahati za kucheza nafasi ya "super hero" ni JK lakini mara zote hazitumii fursa hizo kujijenga.
Lakini pia kina Mponda kujiuzuru ni mpaka rais akubali????
 
mimi siwezi kutibiwa na mtu aliyelazimishwa kurudi kazini...hata siku moja maana anaweza kunichoma sindano anayotumia kuchoma mbwa wenye vichaa....kikwete hili la madaktari limemshinda.....
 
Kwa hulka na sirika ya Kikwete lazima aje na "tabasamu" kubwa na atakachofanya ni "kuwabeza" madaktari... jambo la kushangaza zaidi kuna idadi kubwa ya wapiga kura watasema "mh Raisi yupo sahihi.."

Shida wengi wanasikia habari za magazetini na hawaujui ukweli.
Na ndio kete kubwa ya CCM: propaganda.
 
Mzee Mwanakijiji nakukubali wewe ni guru kwenye kujenga hoja, thanks for this stuff!. Kwa vile ume explore all the posibilities ukaweka na variables na options zilizopo na mifano hai, its up to him to choose kusuka au kunyoa!

One thing for sure, ni whatever the path he may choose, Watanzania wata rally behind their beloved president!. Kwa avarage Tanzanians, uamuzi wowote wa rais wao ndio the right decision no matter what!.

Nyerere ni Nyerere, he was a realist ambaye hakupenda sifa ndio maana alikubali makosa!. Miongoni mwa madhaifu ya JK ni kupenda sifa, kwa hiyo usitegemee kukubali makosa wala kukubali kumwajibisha yoyote katika serikali yake!.

Lets wait and see!.

Pasco, Mbona ushawachagulia Watanzania side watakayokuwa no matter what the President willcome up with?? Kwa kuanagalia haraka haraka tu humu ndani ya forum, Madoctor wanasympathizers wengi kuliko serikali. Vilevile, wananchi kuwa upande wa Serikaliinawezekana haitakuwa suruhisho la mgogoro iwapo Madoctor wataamua kuendelea namgomo wao. Kama ikitokea madoctor wakafukuzwa au wakaendelea na mgomo wao,beleave me two weeks down the road wananchi watahamia upande wa madoctors nahilo litakuwa ni pigo kwa serikali.

Kwa mtu kama wewe nilitegemea uanalyse mambo na kuja na options au constructiveideas kama MMKJJ badala ya kuleta ushabiki kama vile siyo professional person,tena Mwanahabari!! You are rather letting yourself down, if I may say that!!

 
Kila mchangiaji ana shauku na maongezi ya jk na wazee wake hasa tamko kuhusu madaktari ni saa kumi jioni kumwaga mboga na ugali.MM angukuwa jk angalau na jk haongei na wazee tana.
 
mimi ni mpumbavu zaidi na zuzu wa kwanza ninaye iaminisha nafsi yangu kwamba Lowasa atakuja kuwa Rais wa nchi hii!! Mimi ni mjinga kabisa tena nanaishi katika pepo ya mabwege kwenye nchi ya kusadikika. JB Wiser!!!
Ni kweli kabisa Mkuu JB Wiser nimekukubali!. Kumbe majina mengine ya busara kama wise man ni majina tuu!. When you get a bit wiser utanielewa!.

Naunga mkono asilimia 100% EL asimamishwe kuwa mgombea wa CCM tupate raisi toka Kaskazini na ukombozi wa pili na wa kweli wa Mtanzania!.
Wale tunaoelewana, tuendelee kuelewana, wale wengine waacheni waingie chaka!. Kuna watu humu wanadhani neno "The home of great thinkers" ni jina tuu!. Ili kuwa great thinkers lazima uwe na hiyo capacity to think great!. Thanks boy/girl!.
 
Ni kweli kabisa Mkuu JB Wiser nimekukubali!. Kumbe majina mengine ya busara kama wise man ni majina tuu!. When you get a bit wiser utanielewa!.

Naunga mkono asilimia 100% EL asimamishwe kuwa mgombea wa CCM tupate raisi toka Kaskazini na ukombozi wa pili na wa kweli wa Mtanzania!.
Wale tunaoelewana, tuendelee kuelewana, wale wengine waacheni waingie chaka!. Kuna watu humu wanadhani neno "The home of great thinkers" ni jina tuu!. Ili kuwa great thinkers lazima uwe na hiyo capacity to think great!. Thanks boy/girl!.

Pasco wa JF hapo kwenye wekundu sijakuelewa vizuri. Kwani tunatafuta raisi wa kanda flani ndo ukombozi upatikane? au tunahitaji sera na uadilifu na uwajibikaji uliotukuka ili tupate ukombozi.
 
Mzee Mwanakijiji nakukubali wewe ni guru kwenye kujenga hoja, thanks for this stuff!. Kwa vile ume explore all the posibilities ukaweka na variables na options zilizopo na mifano hai, its up to him to choose kusuka au kunyoa!

One thing for sure, ni whatever the path he may choose, Watanzania wata rally behind their beloved president!. Kwa avarage Tanzanians, uamuzi wowote wa rais wao ndio the right decision no matter what!.

Nyerere ni Nyerere, he was a realist ambaye hakupenda sifa ndio maana alikubali makosa!. Miongoni mwa madhaifu ya JK ni kupenda sifa, kwa hiyo usitegemee kukubali makosa wala kukubali kumwajibisha yoyote katika serikali yake!.

Lets wait and see!.
Katika utamaduni wetu kuna hii kanuni kuwa mkubwa hakosei, na ni kanuni hii ambayo imo ndani yetu sisi wote. Hata hivyo kanuni hii imetumiwa vibaya na viongozi ambao katika uongozi huo wamepewa 'ukubwa'. Kitu ambacho viongozi wengi walichosahau ni kuwa ukubwa unakwenda na uwajibikaji. Ukiwa baba kwenye nyumba unatakiwa utimize wajibu wako kama baba, vilevile kwa mama pia na hata watoto vilevile wana wajibu wao. Pindi uwajibikaji usipokuwepo, hata huo 'ukubwa' unakosa uhalali.

Wengi wetu tumeshindwa kutambua kukosekana kwa uhalali wa wakubwa zetu wasipotimiza wajibu wao. Badala yake tunaugua ugonjwa wa 'ndio bwana' (kwa Kiingereza -ndio bwana syndrome). Ndio maana hata kudai haki zetu za msingi inakuwa ni kosa na anayethubutu kudai hubambikiziwa alama kuwa hana adabu ni mtovu wa nidhamu. Kutokana na hali hiyo sitashangaa watu wengine wakishangilia madaktari wakiambiwa ni watovu wa nidhamu.
 
Kwa hulka na sirika ya Kikwete lazima aje na "tabasamu" kubwa na atakachofanya ni "kuwabeza" madaktari... jambo la kushangaza zaidi kuna idadi kubwa ya wapiga kura watasema "mh Raisi yupo sahihi.."

Wasiwasi ni kuwa anaweza kuchochea chuki kati ya madaktari na wazee ambao wengi wao ni clients wa karibu kila mwezi wa madaktari. Madaktari wanaweza rudi kazini lakini wasiwe committed na kutoa huduma kwa 'Ultruism'. Watakaoumia ni wazee na wananchi wanaotegemea hospitali zetu kwa 100% tofauti na viongozi wanategemea kutibiwa nje.
 
Usitafute majibu ya Kikwere Sorry ya Kikwete kwa madaktari. Zingatia mawazo yake, haya hapa.

Madaktari wanataka hela, sisi tunaangalia uchaguzi wa Arumeru

TRA hawakusanyi mapato ya kutosha

Kitilya ameniambia wale watoa hela za kampeni ya CCM , wanajiandaa kutoa hela Arumeru.

Rostam yuko wapi angenisaidia, labda kusamehe kupokea malipo ya Dowans, lakini tumemkorofisha.

Mhh. Lowasa ndio anaumwa Ujerumani, ameshasema asisumbulie kwa lolote, baada ya Sioi Sumari kupitishwa mgombea wa CCM yeye anapumzika.

Mkapa naye haeleweki !!! - tunamtegemea uchaguzi Arumeru analeta za kuleta, hivi tuibue ANBEM kumshikisha adabu au tutulie kwa sasa?


Mwakyembe, Mwandosya wagonjwa- Halafu Sita kang'ang'ania kuna mkono wa mtu. Nifanyeje sasa.

Angalia yule Manumba naye, tumemtuma vingine, kakurupuka kujibu sijui utumbo ule kautoa wapi.

Haya unaona sasa, Membe na wenzake , eti wanataka Mponda na Nkya watemeshwe mzigo, mbona hakuna anayenisaidia?


Nimepata jibu, ngoja nikaongee na wazee wa Dar es Salaam watanipa cha kufanya, nitawakandia madaktari ile mbaya.
 



Yeye mwenyewe kukubali kuwajibika


Mojawapo ya vitu ambavyo tumevikosa kwa muda mrefu ni Rais Kikwete kukubali makosa na udhaifu wa serikali yake. Mojawapo ya vitu ambavyo tumejifunza katika historia ya taifa letu hasa wakati wa Mwalimu ni uwezo wa Baba wa Taifa kukubali makosa na kujaribu kusahihisha makosa. Kwa wanaokumbuka mojawapo ya nyaraka muhimu sana katika historia ya mwanzo ya taifa letu ni ile ya “TUJISAHIHISHE” kwani ilikuwa ni katika nyaraka ile ambapo Nyerere alijaribu kuangalia miaka kumi ya mwanzo ya uhuru na makosa yaliyofanyika na kuweka mkakati wa kuyasahihisha makosa. Kinyume na porojo nyingi kuwa Nyerere “hakuwahi kukubali kukosolewa” ukweli wa kihistoria ni kuwa alifanya hivyo mara nyingi. Siyo kwenye serikali tu hata kwenye chama chake. Kwa wana CCM wanaweza kufanya vizuri kujisomea “MWONGOZO WA 1981” ambao kwa kiwango kikubwa ilikuwa ni jitihada pia ya kujichunguza.
mwanakijiji you are talking two different things here. Think wisely.
 
Kila mara watu hapa JF wanatyumia mfano wa Mwinyi kuwajibika. Mwinyi akiwa waziri wa ndani aliwajibika kwa sababu Polisi waliua wazee waliokisiwa kuwa wachawi. NI kitendo kibaya kilichofanywa na Polisi dhidi ya wananchi. Sasa kwa mfano huo, ikiwa Mponda atatakiwa kuwajibika ni kwa sababu madaktari wamesababisha vifo vya wananchi sio kwa sababu hakubaliani na madai ya madaktari. Haikuwa hivyo, sasa kwa nini watu mnataka kufananisha vitu hivi...Ni vizuri tufahamu kwa nini serikali haikubaliani na madai ya madaktari kuliko kutafuta bangusilo.

Katika masuluhisho yoyote yale baina ya pande mbili lazima kila upande usimamie kile wanacho amini. Madaktari wanaweza kabisa kuwa ma madai yenye maana na lazima lakini huwezi kuweka madai ukiwa na majibu tayari - My way or the highway!. Toka mgogoro huu uanze nimeona jeuri kubwa ya madaktari, sasa ukikutana na mtu jeuri pia ndio matokeo kama haya hutokea.

Meza ya makubaliano upande wa serikali haiwezi kuchaguliwa na madaktari... Hii sielewi madaktari wameipata wapi!.. hata hayo mazungumzo ya baina ya Nato na Iran hawawezi kusema hatumtaki Ahmadinajad au mwakilishi fulani wa Iran kwa sababu tu msimamo wake hawaupendi.
 
kikwetembayuwayu.jpg


Pichani Rais Kikwete akiwakoromea wafanyakazi "mbayuwayu" mwaka 2010 na kuzuia mgomo wao

Leo tutashuhudia kujaribiwa kwa Rais Kikwete kama kiongozi. Naamini hakuna kipimo kizuri cha uwezo wake wa kuongoza na kulishawishi taifa kama atakavyojaribu kuonesha njia ya kushughulikia tatizo la mgomo wa madaktari nchini. Uchaguzi kwake ni mwepesi sana; kuwafanya madaktari waonekane maadui na kuwapa jina baya (demonize) ili kuhalalisha maamuzi dhidi yao ama yeye mwenyewe kuonesha kuwa anawajibika kwa serikali yake kushindwa kushughulikia matatizo ya mgogoro huu uliodumu kwa wiki kadhaa sasa.


Kuwa-demonize madaktari


Njia rahisi na uamuzi mwepesi kwa Rais Kikwete – na yawezekana maarufu kwa baadhi ya watu – ni kuamua kuwabebesha lawama madaktari. Kama tukitumia mfano wa jinsi alivyotumia kikao kama hicho Mei 2010 tunaweza kusema kwa uhakika mkubwa tu kuwa Rais Kikwete anaweza akawafanya duni madaktari na kuwatisha. Katika mkutano uliofanyika Diamond Jubilee wakati ule Rais Kikwete aliwaambia wafanyakazi waliokuwa wanajiandaa kugoma “Mie ndiye muajiri mkuu nisikilizeni mimi, msimsikilize Mgaya (Kaimu Katibu Mkuu TUCTA) mtafukuzwa kazi wala Mgaya hamtamuona! Mtapoteza haki zenu…akili ni nywele kila mtu ana zake mtu mzima dawa”


Akiamua kuchagua njia hii ya kuwa-demonize madaktari ili kujenga hoja ya kuwafukuza kazi atakuwa amechagua njia aliyoizoea –yaani njia ya kutokujaribu kushawishi. Njia hii hata hivyo inadhania (presume) kuwa serikali iko sahihi na haijakosea. Na ninaamini hapa ndipo mgongano ulipo – je serikali imekosea katika kushughulikia suala la madaktari toka mwanzo? Akichagua njia hii manake ni kuwa haamini serikali imekosea na hivyo lawama zote ziwaendee madaktari.

Kwa hiyo, kwa njia hii kuna uwezekano mkubwa wa kutumia muda mrefu kuelezea historia ya “mazungumzo” kama alivyofanya kwa wafanyakazi.

Kwenye kikao kile cha karibu miaka miwili iliyopita Rais Kikwete alisema kati ya mengi “Nimesikia wakiwashawishi kugoma wakitutuhumu sisi kuwa ni serikali isiyoambilika, huo ni uongo na hawa viongozi wa TUCTA ni waongo, wanafiki…nilieleza katika hotuba yangu ya mwezi Machi jinsi serikali ilivyochukua hatua kuboresha maslahi ya wafanyakazi, na dhamira ya kuendelea kuwajali.” Akaongezea na kusema “Nikasema hata katika bajeti ijayo tumejiandaa kuongeza kima cha chini toka sh 60, 000 hadi kufikia 105,000…nikaeleza mambo mazuri toka katika sekta binafsi na umma lakini yote haya wenzetu hawayaoni hata walidiriki kusema kuwa Kikwete kaongeza shilingi 4,000 tu, ama kweli akutukanae hakuchaguli”


Kama huo ni mfano basi tutarajie Rais Kikwete kuwaita majina ya ajabu madaktari. Bado tunakumbuka jinsi Waziri Mkuu mara ya kwanza alipoamua kumuita jina baya (demonize) Dr. Ulimboka na kumdunisha mbele ya jamii. Safari hii kuna uwezekano wa madaktari wote kujaribiwa kufanywa duni na kuitwa “waongo, wanafiki” na kama tumesikia maneno ya karibuni basi “hawana utu, siyo wazalendo, na hawajali viapo vyao”. Yote haya yatafanyika katika kuhalalisha hoja kuwa serikali haijafanya makosa na haipaswi kulaumiwa kwa yanayotokea.


Akichagua njia hiyo manake ni kuwa madaktari watatakiwa kurudi kazini “mara moja” na vitisho vingi – baada ya historia ndefu itakayokuwa inashangiliwa na wazee walioalikwa. Hapa atapata ushujaa wa muda na sifa za kitambo; tatizo la msingi litakuwa halijatatuliwa.


Yeye mwenyewe kukubali kuwajibika


Mojawapo ya vitu ambavyo tumevikosa kwa muda mrefu ni Rais Kikwete kukubali makosa na udhaifu wa serikali yake. Mojawapo ya vitu ambavyo tumejifunza katika historia ya taifa letu hasa wakati wa Mwalimu ni uwezo wa Baba wa Taifa kukubali makosa na kujaribu kusahihisha makosa. Kwa wanaokumbuka mojawapo ya nyaraka muhimu sana katika historia ya mwanzo ya taifa letu ni ile ya “TUJISAHIHISHE” kwani ilikuwa ni katika nyaraka ile ambapo Nyerere alijaribu kuangalia miaka kumi ya mwanzo ya uhuru na makosa yaliyofanyika na kuweka mkakati wa kuyasahihisha makosa. Kinyume na porojo nyingi kuwa Nyerere “hakuwahi kukubali kukosolewa” ukweli wa kihistoria ni kuwa alifanya hivyo mara nyingi. Siyo kwenye serikali tu hata kwenye chama chake. Kwa wana CCM wanaweza kufanya vizuri kujisomea “MWONGOZO WA 1981” ambao kwa kiwango kikubwa ilikuwa ni jitihada pia ya kujichunguza.


Kwa miaka hii mitano iliyopita ya utawala wa Rais Kikwete hakuna wakati wowote ambapo yeye kama Rais amewahi kukaa chini na kuonesha makosa ya serikali yake au hata kuanzisha program ya kujisafisha. Yawezekana Rais Kikwete hataki kuonekana dhaifu; kwa kukubali kuwa kuna makosa atakuwa anawapa maadui zake silaha ya kutumia dhidi yake.


Hata hivyo hapa ndio kipimo hasa cha uongozi. Suala la mgogoro wa madaktari katika nchi nzima lilipaswa kuingiliwa na kuangaliwa na Rais mara moja. Nilipoandika juu ya “tepidity” ya mwitikio wa Rais Kikwete nilimaanisha hili hasa. Kwamba, mgomo wa madaktari ulikuwa jambo kubwa sana kiasi kwamba Waziri Mkuu halimtisho. Walipokubali kurudi kazini na kutoa wiki tatu nilitarajia kuwa labda wakati huo Rais Kikwete angeonesha uongozi yeye mwenyewe kwa kujaribu kuingilia kati na kusikiliza uzito wa madai ya madaktari kutaka Waziri na Naibu wake wawajibishwe. Hakufanya hivyo.


Matokeo yake ni kuwa njia pekee iliyobakia – na sahihi- ni kwa rais Kikwete kukubali moja kwa moja kuwa anawajibika kwa makosa ya mawaziri wake na wale aliowateua na kuwa angepaswa kuingilia kati mapema zaidi. Wamarekani wanamsemo kuwa “the buck stops with the president” wakimaanisha kwamba mwisho wa siku ni Rais anayewajibika. Nitatumia mfano wa Rais Obama mwaka 2010. Kufuatia kumwagika kwa mafuta kwenye Ghuba ya Mexico watu wengi walilalamikia jinsi serikali ilivyoitikia hasa kwa kuacha kwa muda mrefu kampuni ya BP kuamua nini kinafanyika. Hatimaye Rais Obama akizungumza na waandishi wa habari alisimama na kusema kuwa kulikuwa na udhaifu wa mwitiko wa serikali yake – japo ilikuwa inafuatilia – na kuwa kama kulikuwa na mtu anataka kujua nani anawajibika Obama alisema kwa Kiingereza “In case you were wondering who’s responsible, I take responsibility” yaani “kama mlikuwa mnajiuliza nani anawajibika kwa hili, mimi ndio nawajibika”.


Obama hakuishia kukubali tu makosa na kukiri udhaifu wa vyombo mbalimbali vya serikali alienda mbali zaidi na kuongeza muda wa kuzuia utafutwaji mafuta kwa miezi sita na kuzuia makampuni 33 kufanya uchimbaji wowote kule; pamoja na hilo mkuu wa kitendo cha utawala wa mambo ya majini alikuwa amejiuzulu siku ile ile Obama alipozungumza na waandishi wa habari. Kwa ufupi, huu ni mfano wa mwitikio sahihi unaopaswa kuoneshwa na Rais Kikwete leo. Kwamba, suala la mgomo wa madaktari ni suala ambalo yeye alitumaini kuwa lingeweza kumalizwa mara moja na bila kuhatarisha maisha ya Watanzania lakini alikosea kufanya hivyo na anawajibika kwa yote yaliyotokea; siyo Mponda, siyo Nkya, siyo madaktari wala siyo Waziri Mkuu bali yeye.


Halafu Mponda na Nkya wajiuzulu?


Sasa hawezi kuwajibika na kuacha vitu vibakie vilivyo – itakuwa haina maana. Kuwajibika kwa Rais ni lazima kuwe na matokeo. Nyerere alipokuwa anazungumzia suala la kuwajibika kwa Waziri Mkuu Malecela kwenye sakata la “Hoja ya Tanganyika” alisema kanuni muhimu tu kuwa haiwezekani kila wakati kuna makosa basi Rais anawajibika lakini Rais anapowajibishwa Waziri wake lazima awajibike. Nyerere hakutaka Mwinyi aondolewe kwa udhaifu aliouonesha lakini Waziri Mkuu wake ilimpasa awajibike – hata kama ni kwa sababu ya udhaifu wa Rais. Katika hili linaloendelea ni lazima viongozi kadhaa wa serikali wawajibishwe permanently!



Hii ina maana – na nimatumaini yangu – kabla Rais Kikwete hajazungumza na wazee wa CCM jijini Dar na kupitia kwao kuzungumza na taifa Waziri Mponda na Naibu wake Nkya watakuwa wamekubaliwa kujiuzulu. Hili ni jambo muhimu sana kwa sababu hatua yoyote yenye kudhania kuwa wanaweza kuendelea madarakani baada ya madhara yote haya ya sifa, hadhi na heshima yao ni kuwadharau Watanzania.


Hoja ya “kubingirika” hawa wakiondolewa haina msingi


Kwa siku hizi chache nimewasoma wengi ambao wamekuwa wakirudia mojawapo ya makosa (fallacies) kubwa za hoja yaani ile ya kudai “kama tukikubali kwa huyo itakuwa ni mwanzo wa kukubali kwa wengine”. Wenye kutoa hoja hoja hii wanataka watu waogope Rais kushinikizwa hadi kuwaondoa mawaziri kwani akifanya hivyo basi makundi mengine nayo yanaweza kuja na mashanikizo kama haya! Wanaotoa hoja hii wanafikiria wanasema kitu kizito kweli – wanaamini Mponda na Nkya wasiondolewa kwa shinikizo kwani kwa kufanya hivyo mawaziri na viongozi wengine wataondolewa kwa shinikizo! Ni hoja dhaifu sana kiakili.


Kwanza, kwa sababu hadi hivi sasa madai ya kuondolewa kwa Mponda na Nkya hayatolewa kiholela bali yanahusiana na utendaji wao na maamuzi yao kwenye wizara hii na si kwingine. Mawaziri na viongozi wengine watawajibika kwa mambo yao kwenye ofisi zao. Hakuna uhusiano wowote wa kuwashinikiza hawa na kuwashinikiza wengine. Uwezekano wa kutokea hili ni sifuri. Katika elimu ya ujengaji hoja ulaghai huu unafanana sana na kile kinachoitwa “fallacy of conjunction” yaani kama Wikipedia inavyotafsiri kuwa ni “logical fallacy that occurs when it is assumed that specific conditions are more probable than a single general one.


Pili, kama kutakuwepo na viongozi wengine wabovu au wasiotenda inavyopaswa wananchi wanayo haki ya kulalamika na kama wanaopaswa kuwawajibisha wakisuasua basi wananchi wanaweza kuweka shinikizo jingine. Kwa ufupi ni kuwa hakuna kosa kwa wananchi kushinikiza viongozi wabovu kuondolewa; kubwa linalotakiwa ni viongozi kuonesha uadilifu na weledi ili wananchi wasisukumize kuondolewa kwao.


Hivyo, leo ni siku ya majaribio; ni majaribio kwa mtu mmoja tu naye ni Kikwete. Leo ana uamuzi wa kulionesha taifa uongozi au anauamuzi wa kuonesha taifa kuwa bado hajabadilika na hajaelewa uzito wa kuwa Rais! Leo tutashuhudia Kikwete ni kiongozi wa namna gani; je anapenda kutumia ofisi yake kulazimisha mambo au anaweza kutumia nafasi yake kushawishi mazuri kufanyika? Leo tutashuhudia kama Kikwete kama kiongozi anaweza kuwajibika yeye mwenyewe – bila kisingizio – kwa yote yaliyotokea au leo atajitahidi kwa nguvu zake zote – kama alivyofanya mwaka 2010 – kuwademonize madaktari ili tu kutetea viongozi wabovu?


Leo tutapata jibu – je Kikwete anaweza kuonesha njia au kuongeza giza? Kwani kama baada ya kikao chake cha wazee wa CCM kutakuwepo na mgomo mkubwa zaidi basi jibu litakuwa wazi zaidi kwa kila Mtanzania kuwa Kikwete ameshindwa kuongoza. Kwani, endapo mgomo mkubwa zaidi utatokea nchini kwa sababu ya kutoamua sahihi leo hii basi tusije kushangaa tutakachoshuhudia leo hii itakuwa ni kwa Rais Kikwete kuanza kujichimbia shimo la kisiasa ambalo yeye mwenyewe atashindwa kujitoa. Asipofanya sahihi leo – Kikwete atawajibika kweli kweli yeye mwenyewe.
Kwa kujiuzulu.
Mzee mwanakijiji umenena na nafikiri mwenye kuelewa atakuwa ameelewa na kama alipitia hapa basi atakuwa amepata msaada wa hali halisi kwenye jamii
 
1. Ni jambo lisilokubalika kuwa na utendaji wenye ubabaishaji uliokithiri Serikalini katika Wizara zetu juu ya viwango na hata ulipwaji wa mishahara na mafao ya Watumishi wa kada mbalimbali (wasio wizarani) ikiwa ni pamoja na mafao ya kuacha kazi na kustaafu (pensionable & non pensionable).

2. Ni jambo lisilokubalika eti Wanasiasa (hata kama hawana elimu wala ujuzi mkubwa) kulipwa mafao ya juu kuliko Wasomi wengi waliobobea na wenye ujuzi hadhimu unaotakiwa katika kuleta maendeleo nchini.


3. Ni jambo lisilokubalika Serikali kuendelea kukumbatia viongozi wa juu (Mawaziri, Manaibu wao, Wakurugenzi, Makamishina, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makamanda wa Polisi, Wabunge, Majaji / Mahakimu & Maafisa mbalimbali hasa wa Halmshauri zetu n.k) ambao wengi wao eti ndio wenye sifa za: WIZI, UONGO, UBABAISHAJI KAZINI NA KUMILIKI ELIMU AU VYETI / STASHAHADA / SHAHADA FEKI. YAANI WENYE SIFA KINYUME NA HAO ETI NDIO HAWATAKIWI!!!!

KWA MWENDO HUU, HATA MUNGU KAMWE HATAWEZA KUTUBARIKI NA TUTAANDAMWA NA MATUKIO YA UKINZANI YASIYOISHA. MFANO NDANI YA SIKU MOJA, MGOMO WA MADAKTARI, MAANDAMANO YA WANDISHI WA HABARI, MAANDAMANO YA WANANCHI DHIDI YA ENEO LIMECHUKULIWA NA JWTZ BILA MAELEZO, WANAFUNZI WA MUHIMBILI KUKOSA CHAKULA N.K
 
Back
Top Bottom