Kikwete kwenye Tanuru: Kujaribiwa kwa Kiongozi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
kikwetembayuwayu.jpg

Pichani Rais Kikwete akiwakoromea wafanyakazi "mbayuwayu" mwaka 2010 na kuzuia mgomo wao

Leo tutashuhudia kujaribiwa kwa Rais Kikwete kama kiongozi. Naamini hakuna kipimo kizuri cha uwezo wake wa kuongoza na kulishawishi taifa kama atakavyojaribu kuonesha njia ya kushughulikia tatizo la mgomo wa madaktari nchini. Uchaguzi kwake ni mwepesi sana; kuwafanya madaktari waonekane maadui na kuwapa jina baya (demonize) ili kuhalalisha maamuzi dhidi yao ama yeye mwenyewe kuonesha kuwa anawajibika kwa serikali yake kushindwa kushughulikia matatizo ya mgogoro huu uliodumu kwa wiki kadhaa sasa.

Kuwa-demonize madaktari

Njia rahisi na uamuzi mwepesi kwa Rais Kikwete – na yawezekana maarufu kwa baadhi ya watu – ni kuamua kuwabebesha lawama madaktari. Kama tukitumia mfano wa jinsi alivyotumia kikao kama hicho Mei 2010 tunaweza kusema kwa uhakika mkubwa tu kuwa Rais Kikwete anaweza akawafanya duni madaktari na kuwatisha. Katika mkutano uliofanyika Diamond Jubilee wakati ule Rais Kikwete aliwaambia wafanyakazi waliokuwa wanajiandaa kugoma "Mie ndiye muajiri mkuu nisikilizeni mimi, msimsikilize Mgaya (Kaimu Katibu Mkuu TUCTA) mtafukuzwa kazi wala Mgaya hamtamuona! Mtapoteza haki zenu…akili ni nywele kila mtu ana zake mtu mzima dawa"

Akiamua kuchagua njia hii ya kuwa-demonize madaktari ili kujenga hoja ya kuwafukuza kazi atakuwa amechagua njia aliyoizoea –yaani njia ya kutokujaribu kushawishi. Njia hii hata hivyo inadhania (presume) kuwa serikali iko sahihi na haijakosea. Na ninaamini hapa ndipo mgongano ulipo – je serikali imekosea katika kushughulikia suala la madaktari toka mwanzo? Akichagua njia hii manake ni kuwa haamini serikali imekosea na hivyo lawama zote ziwaendee madaktari.

Kwa hiyo, kwa njia hii kuna uwezekano mkubwa wa kutumia muda mrefu kuelezea historia ya "mazungumzo" kama alivyofanya kwa wafanyakazi.

Kwenye kikao kile cha karibu miaka miwili iliyopita Rais Kikwete alisema kati ya mengi "Nimesikia wakiwashawishi kugoma wakitutuhumu sisi kuwa ni serikali isiyoambilika, huo ni uongo na hawa viongozi wa TUCTA ni waongo, wanafiki…nilieleza katika hotuba yangu ya mwezi Machi jinsi serikali ilivyochukua hatua kuboresha maslahi ya wafanyakazi, na dhamira ya kuendelea kuwajali." Akaongezea na kusema "Nikasema hata katika bajeti ijayo tumejiandaa kuongeza kima cha chini toka sh 60, 000 hadi kufikia 105,000…nikaeleza mambo mazuri toka katika sekta binafsi na umma lakini yote haya wenzetu hawayaoni hata walidiriki kusema kuwa Kikwete kaongeza shilingi 4,000 tu, ama kweli akutukanae hakuchaguli"

Kama huo ni mfano basi tutarajie Rais Kikwete kuwaita majina ya ajabu madaktari. Bado tunakumbuka jinsi Waziri Mkuu mara ya kwanza alipoamua kumuita jina baya (demonize) Dr. Ulimboka na kumdunisha mbele ya jamii. Safari hii kuna uwezekano wa madaktari wote kujaribiwa kufanywa duni na kuitwa "waongo, wanafiki" na kama tumesikia maneno ya karibuni basi "hawana utu, siyo wazalendo, na hawajali viapo vyao". Yote haya yatafanyika katika kuhalalisha hoja kuwa serikali haijafanya makosa na haipaswi kulaumiwa kwa yanayotokea.

Akichagua njia hiyo manake ni kuwa madaktari watatakiwa kurudi kazini "mara moja" na vitisho vingi – baada ya historia ndefu itakayokuwa inashangiliwa na wazee walioalikwa. Hapa atapata ushujaa wa muda na sifa za kitambo; tatizo la msingi litakuwa halijatatuliwa.

Yeye mwenyewe kukubali kuwajibika

Mojawapo ya vitu ambavyo tumevikosa kwa muda mrefu ni Rais Kikwete kukubali makosa na udhaifu wa serikali yake. Mojawapo ya vitu ambavyo tumejifunza katika historia ya taifa letu hasa wakati wa Mwalimu ni uwezo wa Baba wa Taifa kukubali makosa na kujaribu kusahihisha makosa. Kwa wanaokumbuka mojawapo ya nyaraka muhimu sana katika historia ya mwanzo ya taifa letu ni ile ya "TUJISAHIHISHE" kwani ilikuwa ni katika nyaraka ile ambapo Nyerere alijaribu kuangalia miaka kumi ya mwanzo ya uhuru na makosa yaliyofanyika na kuweka mkakati wa kuyasahihisha makosa. Kinyume na porojo nyingi kuwa Nyerere "hakuwahi kukubali kukosolewa" ukweli wa kihistoria ni kuwa alifanya hivyo mara nyingi. Siyo kwenye serikali tu hata kwenye chama chake. Kwa wana CCM wanaweza kufanya vizuri kujisomea "MWONGOZO WA 1981" ambao kwa kiwango kikubwa ilikuwa ni jitihada pia ya kujichunguza.

Kwa miaka hii mitano iliyopita ya utawala wa Rais Kikwete hakuna wakati wowote ambapo yeye kama Rais amewahi kukaa chini na kuonesha makosa ya serikali yake au hata kuanzisha program ya kujisafisha. Yawezekana Rais Kikwete hataki kuonekana dhaifu; kwa kukubali kuwa kuna makosa atakuwa anawapa maadui zake silaha ya kutumia dhidi yake.

Hata hivyo hapa ndio kipimo hasa cha uongozi. Suala la mgogoro wa madaktari katika nchi nzima lilipaswa kuingiliwa na kuangaliwa na Rais mara moja. Nilipoandika juu ya "tepidity" ya mwitikio wa Rais Kikwete nilimaanisha hili hasa. Kwamba, mgomo wa madaktari ulikuwa jambo kubwa sana kiasi kwamba Waziri Mkuu halimtisho. Walipokubali kurudi kazini na kutoa wiki tatu nilitarajia kuwa labda wakati huo Rais Kikwete angeonesha uongozi yeye mwenyewe kwa kujaribu kuingilia kati na kusikiliza uzito wa madai ya madaktari kutaka Waziri na Naibu wake wawajibishwe. Hakufanya hivyo.

Matokeo yake ni kuwa njia pekee iliyobakia – na sahihi- ni kwa rais Kikwete kukubali moja kwa moja kuwa anawajibika kwa makosa ya mawaziri wake na wale aliowateua na kuwa angepaswa kuingilia kati mapema zaidi. Wamarekani wanamsemo kuwa "the buck stops with the president" wakimaanisha kwamba mwisho wa siku ni Rais anayewajibika. Nitatumia mfano wa Rais Obama mwaka 2010. Kufuatia kumwagika kwa mafuta kwenye Ghuba ya Mexico watu wengi walilalamikia jinsi serikali ilivyoitikia hasa kwa kuacha kwa muda mrefu kampuni ya BP kuamua nini kinafanyika. Hatimaye Rais Obama akizungumza na waandishi wa habari alisimama na kusema kuwa kulikuwa na udhaifu wa mwitiko wa serikali yake – japo ilikuwa inafuatilia – na kuwa kama kulikuwa na mtu anataka kujua nani anawajibika Obama alisema kwa Kiingereza "In case you were wondering who's responsible, I take responsibility" yaani "kama mlikuwa mnajiuliza nani anawajibika kwa hili, mimi ndio nawajibika".

Obama hakuishia kukubali tu makosa na kukiri udhaifu wa vyombo mbalimbali vya serikali alienda mbali zaidi na kuongeza muda wa kuzuia utafutwaji mafuta kwa miezi sita na kuzuia makampuni 33 kufanya uchimbaji wowote kule; pamoja na hilo mkuu wa kitendo cha utawala wa mambo ya majini alikuwa amejiuzulu siku ile ile Obama alipozungumza na waandishi wa habari. Kwa ufupi, huu ni mfano wa mwitikio sahihi unaopaswa kuoneshwa na Rais Kikwete leo. Kwamba, suala la mgomo wa madaktari ni suala ambalo yeye alitumaini kuwa lingeweza kumalizwa mara moja na bila kuhatarisha maisha ya Watanzania lakini alikosea kufanya hivyo na anawajibika kwa yote yaliyotokea; siyo Mponda, siyo Nkya, siyo madaktari wala siyo Waziri Mkuu bali yeye.

Halafu Mponda na Nkya wajiuzulu?

Sasa hawezi kuwajibika na kuacha vitu vibakie vilivyo – itakuwa haina maana. Kuwajibika kwa Rais ni lazima kuwe na matokeo. Nyerere alipokuwa anazungumzia suala la kuwajibika kwa Waziri Mkuu Malecela kwenye sakata la "Hoja ya Tanganyika" alisema kanuni muhimu tu kuwa haiwezekani kila wakati kuna makosa basi Rais anawajibika lakini Rais anapowajibishwa Waziri wake lazima awajibike. Nyerere hakutaka Mwinyi aondolewe kwa udhaifu aliouonesha lakini Waziri Mkuu wake ilimpasa awajibike – hata kama ni kwa sababu ya udhaifu wa Rais. Katika hili linaloendelea ni lazima viongozi kadhaa wa serikali wawajibishwe permanently!

Hii ina maana – na nimatumaini yangu – kabla Rais Kikwete hajazungumza na wazee wa CCM jijini Dar na kupitia kwao kuzungumza na taifa Waziri Mponda na Naibu wake Nkya watakuwa wamekubaliwa kujiuzulu. Hili ni jambo muhimu sana kwa sababu hatua yoyote yenye kudhania kuwa wanaweza kuendelea madarakani baada ya madhara yote haya ya sifa, hadhi na heshima yao ni kuwadharau Watanzania.

Hoja ya "kubingirika" hawa wakiondolewa haina msingi

Kwa siku hizi chache nimewasoma wengi ambao wamekuwa wakirudia mojawapo ya makosa (fallacies) kubwa za hoja yaani ile ya kudai "kama tukikubali kwa huyo itakuwa ni mwanzo wa kukubali kwa wengine". Wenye kutoa hoja hoja hii wanataka watu waogope Rais kushinikizwa hadi kuwaondoa mawaziri kwani akifanya hivyo basi makundi mengine nayo yanaweza kuja na mashanikizo kama haya! Wanaotoa hoja hii wanafikiria wanasema kitu kizito kweli – wanaamini Mponda na Nkya wasiondolewa kwa shinikizo kwani kwa kufanya hivyo mawaziri na viongozi wengine wataondolewa kwa shinikizo! Ni hoja dhaifu sana kiakili.

Kwanza, kwa sababu hadi hivi sasa madai ya kuondolewa kwa Mponda na Nkya hayatolewa kiholela bali yanahusiana na utendaji wao na maamuzi yao kwenye wizara hii na si kwingine. Mawaziri na viongozi wengine watawajibika kwa mambo yao kwenye ofisi zao. Hakuna uhusiano wowote wa kuwashinikiza hawa na kuwashinikiza wengine. Uwezekano wa kutokea hili ni sifuri. Katika elimu ya ujengaji hoja ulaghai huu unafanana sana na kile kinachoitwa "fallacy of conjunction" yaani kama Wikipedia inavyotafsiri kuwa ni "logical fallacy that occurs when it is assumed that specific conditions are more probable than a single general one.

Pili, kama kutakuwepo na viongozi wengine wabovu au wasiotenda inavyopaswa wananchi wanayo haki ya kulalamika na kama wanaopaswa kuwawajibisha wakisuasua basi wananchi wanaweza kuweka shinikizo jingine. Kwa ufupi ni kuwa hakuna kosa kwa wananchi kushinikiza viongozi wabovu kuondolewa; kubwa linalotakiwa ni viongozi kuonesha uadilifu na weledi ili wananchi wasisukumize kuondolewa kwao.

Hivyo, leo ni siku ya majaribio; ni majaribio kwa mtu mmoja tu naye ni Kikwete. Leo ana uamuzi wa kulionesha taifa uongozi au anauamuzi wa kuonesha taifa kuwa bado hajabadilika na hajaelewa uzito wa kuwa Rais! Leo tutashuhudia Kikwete ni kiongozi wa namna gani; je anapenda kutumia ofisi yake kulazimisha mambo au anaweza kutumia nafasi yake kushawishi mazuri kufanyika? Leo tutashuhudia kama Kikwete kama kiongozi anaweza kuwajibika yeye mwenyewe – bila kisingizio – kwa yote yaliyotokea au leo atajitahidi kwa nguvu zake zote – kama alivyofanya mwaka 2010 – kuwademonize madaktari ili tu kutetea viongozi wabovu?

Leo tutapata jibu – je Kikwete anaweza kuonesha njia au kuongeza giza? Kwani kama baada ya kikao chake cha wazee wa CCM kutakuwepo na mgomo mkubwa zaidi basi jibu litakuwa wazi zaidi kwa kila Mtanzania kuwa Kikwete ameshindwa kuongoza. Kwani, endapo mgomo mkubwa zaidi utatokea nchini kwa sababu ya kutoamua sahihi leo hii basi tusije kushangaa tutakachoshuhudia leo hii itakuwa ni kwa Rais Kikwete kuanza kujichimbia shimo la kisiasa ambalo yeye mwenyewe atashindwa kujitoa. Asipofanya sahihi leo – Kikwete atawajibika kweli kweli yeye mwenyewe.
Kwa kujiuzulu.
 
Kweli umenena MM; tunategemea huyu kiongozi wetu kutoa lawama tu kwa madaktari, si vinginevyo. Lets wait and see!

Miye natarajia hivyo lakini pia naombea kuwa for once atakubali kuwajibika yeye mwenyewe na kulimaliza hili baada ya kuwalilia madaktari kwa kuwafukuza kina Nkya na Mponda. Njia nzuri ni kulia "madaktari wameshindwa kuonesha utu, ndugu zangu kwa kweli tumejitahidi sana, lakini madaktari hawataki. Sasa sisi tumefanya kila lililo ndani ya uwezo wetu kutatua mgogoro lakini wenzetu hawa wameamua kugoma. Imebidi hadi twende mahakamani, na sasa mahakama imeamuru warudi sasa na mimi nasema warudi; wasiporudi kwa kweli kabisa itabidi tuwafukuze na kama kuanza upya tutaanza upya. Wametaka mawaziri hawa waondoke miye nimekubali. Sasa basi warudi kazini".

Kitu kibaya anachoweza kufanya ni kuvunja baraza zima la mawaziri ili kuwaondoa hawa wawili tu. Atajiweka kwenye hali mbaya zaidi baadaye.
 
Kikwete haambiliki wala habadiliki.
Style ya kuongea ya kuongea na wazee maswala yanauohusu watu wengine ni dhahiri kwamba anachpkwenda kuongea ni majungu, fitna na uwongo ambao hawezi kuuongea mbele ya madaktari.

Huyo ndo Kikwete wa Lugoba.
 
Mzee Mwanakijiji nakukubali wewe ni guru kwenye kujenga hoja, thanks for this stuff!. Kwa vile ume explore all the posibilities ukaweka na variables na options zilizopo na mifano hai, its up to him to choose kusuka au kunyoa!

One thing for sure, ni whatever the path he may choose, Watanzania wata rally behind their beloved president!. Kwa avarage Tanzanians, uamuzi wowote wa rais wao ndio the right decision no matter what!.

Nyerere ni Nyerere, he was a realist ambaye hakupenda sifa ndio maana alikubali makosa!. Miongoni mwa madhaifu ya JK ni kupenda sifa, kwa hiyo usitegemee kukubali makosa wala kukubali kumwajibisha yoyote katika serikali yake!.

Lets wait and see!.
 
Kwa hulka na sirika ya Kikwete lazima aje na "tabasamu" kubwa na atakachofanya ni "kuwabeza" madaktari... jambo la kushangaza zaidi kuna idadi kubwa ya wapiga kura watasema "mh Raisi yupo sahihi.."

Kwa hiyo inaonekanaa watu wengi wanatarajia Kikwete atawa disparage madaktari na akiffanya kitu kingine chochote itakuwa ni "out of character" kwa kweli.
 
Unaposema wapiga kura una maana wepi? NEC au mimi na wewe? mimi nasema rais hayupo sahihi, limebaki tamko lako na la tume ya uchaguzi!! soon tutajua tu! kikwete hawezi kutuchonganisha na madaktari, tunajua ukifika wakati siri ya ugonjwa ni ya mgonjwa na daktari! haiwi ya ccm wala kikwata.
 
Mzee Mwanakijiji nakukubali wewe ni guru kwenye kujenga hoja, thanks for this stuff!. Kwa vile ume explore all the posibilities ukaweka na variables na options zilizopo na mifano hai, its up to him to choose kusuka au kunyoa!

One thing for sure, ni whatever the path he may chooses, Watanzania wata rally behind their beloved president!. Kweke na kwa avarage Tanzanians, uamuzi wowote wa rais wap ndio the right decision no matter what!. Nyerere ni Nyerere, he was a realist ambaye hakupenda sifa ndio maana alikubali makosa!. Miongoni mwa madhaifu ya JK ni kupenda sifa, kwa hiyo usitegemee kukubali makosa wala kukubali yoyote katika serikali yake kuwajibika!.

Lets wait and see!.

Mkuu ingekuwa heri kama salva angemwonyesha hii kitu ili apate ku-dessa, lakini kikwata atatinga ukumbini na kuvichukulia poa vizee vya watu. tutaisoma sura yake kuona kama nchi inatawalika au la! na haya ni makosa ya binadamu kutekeleza ushauri wa sokwe!!!!
 
Mwanakijiji hoja yako imetulia sana. Wasiwasi wangu hotuba na vielelezo atakuwa amepewa na kina Mponda kuwaponda madaktari.

Alipohojiwa na Tido Mhando 2005 alidai atajiwekea utaratibu wa kupata taarifa nje ya mfumo rasmi ili kuepuka taarifa zilizochujwa.

Sina hakika kama analifanya hili vinginevyo angechukua option ya pili....kuwajibika.
 
You have said it all mkuu,
Sijui huu utamaduni wa kusubiri mpaka maafa yatokee bila wahusika kuwajibishwa tumeutoa wapi. Kiukweli kabisa nina uhakika hata dr.mponda na nkya hawana hata hamu ya kurudi ofisini kwao mpaka sasa!
Turudi kwa jeykei yeye ni mgumu kukiri udhaifu na kuruhusu uwajibishwaji wa rafiki zake kitu ambacho kimeligharimu taifa mpaka sasa.Na huu mtindo wa kuongea na wazee ndio unamuharibia kabisa na anazidi kuonekana wa ajabu.Tutatoa assumptions nyingi sana kuhusu mkutano wake wa leo lakini its only a few hours to go lets wait and see what hes going to say this time
 
Mzee Mwanakijiji nakukubali wewe ni guru kwenye kujenga hoja, thanks for this stuff!. Kwa vile ume explore all the posibilities ukaweka na variables na options zilizopo na mifano hai, its up to him to choose kusuka au kunyoa!

One thing for sure, ni whatever the path he may choose, Watanzania wata rally behind their beloved president!. Kwa avarage Tanzanians, uamuzi wowote wa rais wao ndio the right decision no matter what!.

Nyerere ni Nyerere, he was a realist ambaye hakupenda sifa ndio maana alikubali makosa!. Miongoni mwa madhaifu ya JK ni kupenda sifa, kwa hiyo usitegemee kukubali makosa wala kukubali kumwajibisha yoyote katika serikali yake!.

Lets wait and see!.
Pasco tuombe radhi Watanzania kwa kutukejeri kwamba sisi ni wajinga wa viwango hivi, kwamba Mswahili yeyote anaweza akatulisha porojo za kikupumbavu!
Ungeeleweka kama ungesema wazee wa CCM wao ndio watamsupport Kikwete maana ile mishipa yao ya fahamu ilishakufa miaka mingi iliyopita.
 
Tanzania tanzania Nchi yenye mali nyingi watu wengi wa uluyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa wanaitamani sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kitendo cha JK kutaka kuongea na watanzania kupitia wazee wa dar leo siku ya tatu watu wakiwa wanakufa nakuteseka na magonjwa si cha kiungwana. Mimi nasema sio cha kiungwa kabisa.

Hii ni jeuri ya utawala kwasababu anadola!! Sitegemei cha tofauti zaidi ya kuwakejeli wadaktari na kuwalazimisha warudi kazini. Ila sijui kitakachotokea baada ya kuwadhiaki wadaktari na kutumia nguvu ya dola kuwalazimisha warudi kazini.

Namaswali mawili;
1. Je, madaktari watafanya kazi kwa ubora na kiwango baada ya kudhalilishwa na kulazimishwa?
2. Serikali ipo tayari kusimamia ubora wa kazi ya madaktari na kulinda afya ya mwananchi baada ya kuwalazimisha?

Nimeamua kujiaminisha kuwa baraza la mawaziri limekubaliana kwa pamoja atakachokisema JK leo na wapo tayari kwa umoja kubeba matokeo bila kutofautiana.
 
kikwetembayuwayu.jpg

Pichani Rais Kikwete akiwakoromea wafanyakazi "mbayuwayu" mwaka 2010 na kuzuia mgomo wao

Leo tutashuhudia kujaribiwa kwa Rais Kikwete kama kiongozi. Naamini hakuna kipimo kizuri cha uwezo wake wa kuongoza na kulishawishi taifa kama atakavyojaribu kuonesha njia ya kushughulikia tatizo la mgomo wa madaktari nchini. Uchaguzi kwake ni mwepesi sana; kuwafanya madaktari waonekane maadui na kuwapa jina baya (demonize) ili kuhalalisha maamuzi dhidi yao ama yeye mwenyewe kuonesha kuwa anawajibika kwa serikali yake kushindwa kushughulikia matatizo ya mgogoro huu uliodumu kwa wiki kadhaa sasa.

Kuwa-demonize madaktari

Njia rahisi na uamuzi mwepesi kwa Rais Kikwete – na yawezekana maarufu kwa baadhi ya watu – ni kuamua kuwabebesha lawama madaktari. Kama tukitumia mfano wa jinsi alivyotumia kikao kama hicho Mei 2010 tunaweza kusema kwa uhakika mkubwa tu kuwa Rais Kikwete anaweza akawafanya duni madaktari na kuwatisha. Katika mkutano uliofanyika Diamond Jubilee wakati ule Rais Kikwete aliwaambia wafanyakazi waliokuwa wanajiandaa kugoma "Mie ndiye muajiri mkuu nisikilizeni mimi, msimsikilize Mgaya (Kaimu Katibu Mkuu TUCTA) mtafukuzwa kazi wala Mgaya hamtamuona! Mtapoteza haki zenu…akili ni nywele kila mtu ana zake mtu mzima dawa"

Akiamua kuchagua njia hii ya kuwa-demonize madaktari ili kujenga hoja ya kuwafukuza kazi atakuwa amechagua njia aliyoizoea –yaani njia ya kutokujaribu kushawishi. Njia hii hata hivyo inadhania (presume) kuwa serikali iko sahihi na haijakosea. Na ninaamini hapa ndipo mgongano ulipo – je serikali imekosea katika kushughulikia suala la madaktari toka mwanzo? Akichagua njia hii manake ni kuwa haamini serikali imekosea na hivyo lawama zote ziwaendee madaktari.

Kwa hiyo, kwa njia hii kuna uwezekano mkubwa wa kutumia muda mrefu kuelezea historia ya "mazungumzo" kama alivyofanya kwa wafanyakazi.

Kwenye kikao kile cha karibu miaka miwili iliyopita Rais Kikwete alisema kati ya mengi "Nimesikia wakiwashawishi kugoma wakitutuhumu sisi kuwa ni serikali isiyoambilika, huo ni uongo na hawa viongozi wa TUCTA ni waongo, wanafiki…nilieleza katika hotuba yangu ya mwezi Machi jinsi serikali ilivyochukua hatua kuboresha maslahi ya wafanyakazi, na dhamira ya kuendelea kuwajali." Akaongezea na kusema "Nikasema hata katika bajeti ijayo tumejiandaa kuongeza kima cha chini toka sh 60, 000 hadi kufikia 105,000…nikaeleza mambo mazuri toka katika sekta binafsi na umma lakini yote haya wenzetu hawayaoni hata walidiriki kusema kuwa Kikwete kaongeza shilingi 4,000 tu, ama kweli akutukanae hakuchaguli"

Kama huo ni mfano basi tutarajie Rais Kikwete kuwaita majina ya ajabu madaktari. Bado tunakumbuka jinsi Waziri Mkuu mara ya kwanza alipoamua kumuita jina baya (demonize) Dr. Ulimboka na kumdunisha mbele ya jamii. Safari hii kuna uwezekano wa madaktari wote kujaribiwa kufanywa duni na kuitwa "waongo, wanafiki" na kama tumesikia maneno ya karibuni basi "hawana utu, siyo wazalendo, na hawajali viapo vyao". Yote haya yatafanyika katika kuhalalisha hoja kuwa serikali haijafanya makosa na haipaswi kulaumiwa kwa yanayotokea.

Akichagua njia hiyo manake ni kuwa madaktari watatakiwa kurudi kazini "mara moja" na vitisho vingi – baada ya historia ndefu itakayokuwa inashangiliwa na wazee walioalikwa. Hapa atapata ushujaa wa muda na sifa za kitambo; tatizo la msingi litakuwa halijatatuliwa.

Yeye mwenyewe kukubali kuwajibika

Mojawapo ya vitu ambavyo tumevikosa kwa muda mrefu ni Rais Kikwete kukubali makosa na udhaifu wa serikali yake. Mojawapo ya vitu ambavyo tumejifunza katika historia ya taifa letu hasa wakati wa Mwalimu ni uwezo wa Baba wa Taifa kukubali makosa na kujaribu kusahihisha makosa. Kwa wanaokumbuka mojawapo ya nyaraka muhimu sana katika historia ya mwanzo ya taifa letu ni ile ya "TUJISAHIHISHE" kwani ilikuwa ni katika nyaraka ile ambapo Nyerere alijaribu kuangalia miaka kumi ya mwanzo ya uhuru na makosa yaliyofanyika na kuweka mkakati wa kuyasahihisha makosa. Kinyume na porojo nyingi kuwa Nyerere "hakuwahi kukubali kukosolewa" ukweli wa kihistoria ni kuwa alifanya hivyo mara nyingi. Siyo kwenye serikali tu hata kwenye chama chake. Kwa wana CCM wanaweza kufanya vizuri kujisomea "MWONGOZO WA 1981" ambao kwa kiwango kikubwa ilikuwa ni jitihada pia ya kujichunguza.

Kwa miaka hii mitano iliyopita ya utawala wa Rais Kikwete hakuna wakati wowote ambapo yeye kama Rais amewahi kukaa chini na kuonesha makosa ya serikali yake au hata kuanzisha program ya kujisafisha. Yawezekana Rais Kikwete hataki kuonekana dhaifu; kwa kukubali kuwa kuna makosa atakuwa anawapa maadui zake silaha ya kutumia dhidi yake.

Hata hivyo hapa ndio kipimo hasa cha uongozi. Suala la mgogoro wa madaktari katika nchi nzima lilipaswa kuingiliwa na kuangaliwa na Rais mara moja. Nilipoandika juu ya "tepidity" ya mwitikio wa Rais Kikwete nilimaanisha hili hasa. Kwamba, mgomo wa madaktari ulikuwa jambo kubwa sana kiasi kwamba Waziri Mkuu halimtisho. Walipokubali kurudi kazini na kutoa wiki tatu nilitarajia kuwa labda wakati huo Rais Kikwete angeonesha uongozi yeye mwenyewe kwa kujaribu kuingilia kati na kusikiliza uzito wa madai ya madaktari kutaka Waziri na Naibu wake wawajibishwe. Hakufanya hivyo.

Matokeo yake ni kuwa njia pekee iliyobakia – na sahihi- ni kwa rais Kikwete kukubali moja kwa moja kuwa anawajibika kwa makosa ya mawaziri wake na wale aliowateua na kuwa angepaswa kuingilia kati mapema zaidi. Wamarekani wanamsemo kuwa "the buck stops with the president" wakimaanisha kwamba mwisho wa siku ni Rais anayewajibika. Nitatumia mfano wa Rais Obama mwaka 2010. Kufuatia kumwagika kwa mafuta kwenye Ghuba ya Mexico watu wengi walilalamikia jinsi serikali ilivyoitikia hasa kwa kuacha kwa muda mrefu kampuni ya BP kuamua nini kinafanyika. Hatimaye Rais Obama akizungumza na waandishi wa habari alisimama na kusema kuwa kulikuwa na udhaifu wa mwitiko wa serikali yake – japo ilikuwa inafuatilia – na kuwa kama kulikuwa na mtu anataka kujua nani anawajibika Obama alisema kwa Kiingereza "In case you were wondering who's responsible, I take responsibility" yaani "kama mlikuwa mnajiuliza nani anawajibika kwa hili, mimi ndio nawajibika".

Obama hakuishia kukubali tu makosa na kukiri udhaifu wa vyombo mbalimbali vya serikali alienda mbali zaidi na kuongeza muda wa kuzuia utafutwaji mafuta kwa miezi sita na kuzuia makampuni 33 kufanya uchimbaji wowote kule; pamoja na hilo mkuu wa kitendo cha utawala wa mambo ya majini alikuwa amejiuzulu siku ile ile Obama alipozungumza na waandishi wa habari. Kwa ufupi, huu ni mfano wa mwitikio sahihi unaopaswa kuoneshwa na Rais Kikwete leo. Kwamba, suala la mgomo wa madaktari ni suala ambalo yeye alitumaini kuwa lingeweza kumalizwa mara moja na bila kuhatarisha maisha ya Watanzania lakini alikosea kufanya hivyo na anawajibika kwa yote yaliyotokea; siyo Mponda, siyo Nkya, siyo madaktari wala siyo Waziri Mkuu bali yeye.

Halafu Mponda na Nkya wajiuzulu?

Sasa hawezi kuwajibika na kuacha vitu vibakie vilivyo – itakuwa haina maana. Kuwajibika kwa Rais ni lazima kuwe na matokeo. Nyerere alipokuwa anazungumzia suala la kuwajibika kwa Waziri Mkuu Malecela kwenye sakata la "Hoja ya Tanganyika" alisema kanuni muhimu tu kuwa haiwezekani kila wakati kuna makosa basi Rais anawajibika lakini Rais anapowajibishwa Waziri wake lazima awajibike. Nyerere hakutaka Mwinyi aondolewe kwa udhaifu aliouonesha lakini Waziri Mkuu wake ilimpasa awajibike – hata kama ni kwa sababu ya udhaifu wa Rais. Katika hili linaloendelea ni lazima viongozi kadhaa wa serikali wawajibishwe permanently!

Hii ina maana – na nimatumaini yangu – kabla Rais Kikwete hajazungumza na wazee wa CCM jijini Dar na kupitia kwao kuzungumza na taifa Waziri Mponda na Naibu wake Nkya watakuwa wamekubaliwa kujiuzulu. Hili ni jambo muhimu sana kwa sababu hatua yoyote yenye kudhania kuwa wanaweza kuendelea madarakani baada ya madhara yote haya ya sifa, hadhi na heshima yao ni kuwadharau Watanzania.

Hoja ya "kubingirika" hawa wakiondolewa haina msingi

Kwa siku hizi chache nimewasoma wengi ambao wamekuwa wakirudia mojawapo ya makosa (fallacies) kubwa za hoja yaani ile ya kudai "kama tukikubali kwa huyo itakuwa ni mwanzo wa kukubali kwa wengine". Wenye kutoa hoja hoja hii wanataka watu waogope Rais kushinikizwa hadi kuwaondoa mawaziri kwani akifanya hivyo basi makundi mengine nayo yanaweza kuja na mashanikizo kama haya! Wanaotoa hoja hii wanafikiria wanasema kitu kizito kweli – wanaamini Mponda na Nkya wasiondolewa kwa shinikizo kwani kwa kufanya hivyo mawaziri na viongozi wengine wataondolewa kwa shinikizo! Ni hoja dhaifu sana kiakili.

Kwanza, kwa sababu hadi hivi sasa madai ya kuondolewa kwa Mponda na Nkya hayatolewa kiholela bali yanahusiana na utendaji wao na maamuzi yao kwenye wizara hii na si kwingine. Mawaziri na viongozi wengine watawajibika kwa mambo yao kwenye ofisi zao. Hakuna uhusiano wowote wa kuwashinikiza hawa na kuwashinikiza wengine. Uwezekano wa kutokea hili ni sifuri. Katika elimu ya ujengaji hoja ulaghai huu unafanana sana na kile kinachoitwa "fallacy of conjunction" yaani kama Wikipedia inavyotafsiri kuwa ni "logical fallacy that occurs when it is assumed that specific conditions are more probable than a single general one.

Pili, kama kutakuwepo na viongozi wengine wabovu au wasiotenda inavyopaswa wananchi wanayo haki ya kulalamika na kama wanaopaswa kuwawajibisha wakisuasua basi wananchi wanaweza kuweka shinikizo jingine. Kwa ufupi ni kuwa hakuna kosa kwa wananchi kushinikiza viongozi wabovu kuondolewa; kubwa linalotakiwa ni viongozi kuonesha uadilifu na weledi ili wananchi wasisukumize kuondolewa kwao.

Hivyo, leo ni siku ya majaribio; ni majaribio kwa mtu mmoja tu naye ni Kikwete. Leo ana uamuzi wa kulionesha taifa uongozi au anauamuzi wa kuonesha taifa kuwa bado hajabadilika na hajaelewa uzito wa kuwa Rais! Leo tutashuhudia Kikwete ni kiongozi wa namna gani; je anapenda kutumia ofisi yake kulazimisha mambo au anaweza kutumia nafasi yake kushawishi mazuri kufanyika? Leo tutashuhudia kama Kikwete kama kiongozi anaweza kuwajibika yeye mwenyewe – bila kisingizio – kwa yote yaliyotokea au leo atajitahidi kwa nguvu zake zote – kama alivyofanya mwaka 2010 – kuwademonize madaktari ili tu kutetea viongozi wabovu?

Leo tutapata jibu – je Kikwete anaweza kuonesha njia au kuongeza giza? Kwani kama baada ya kikao chake cha wazee wa CCM kutakuwepo na mgomo mkubwa zaidi basi jibu litakuwa wazi zaidi kwa kila Mtanzania kuwa Kikwete ameshindwa kuongoza. Kwani, endapo mgomo mkubwa zaidi utatokea nchini kwa sababu ya kutoamua sahihi leo hii basi tusije kushangaa tutakachoshuhudia leo hii itakuwa ni kwa Rais Kikwete kuanza kujichimbia shimo la kisiasa ambalo yeye mwenyewe atashindwa kujitoa. Asipofanya sahihi leo – Kikwete atawajibika kweli kweli yeye mwenyewe.
Kwa kujiuzulu.

Umenena mkuu, Kikwete kama atawatumia washauri wake wa siku zote, leo unaweza ukawa mwanzo wa mwisho wa Utawala wake, ninaamini akiendeleza tabia za kuwakandamiza watu anao vutana nao itamuia vigumu kwa hili la madaktari tusubiri tuone. Ila wakati mwingine ninamuonea huruma Urais ni kazi ngumu sana kwa watu wa uwezo wake.
 
MM sina la kuongeza baba angu eee. Ujumbe umefi.....umefika kweli. Aamue kusu.....kusuka kweli au kunyo.....kunyoa kweli. Yetu ma....macho na ma.....masikio kweli.
 
Mzee Mwanakijiji nakukubali wewe ni guru kwenye kujenga hoja, thanks for this stuff!. Kwa vile ume explore all the posibilities ukaweka na variables na options zilizopo na mifano hai, its up to him to choose kusuka au kunyoa!

One thing for sure, ni whatever the path he may choose, Watanzania wata rally behind their beloved president!. Kwa avarage Tanzanians, uamuzi wowote wa rais wao ndio the right decision no matter what!.

Nyerere ni Nyerere, he was a realist ambaye hakupenda sifa ndio maana alikubali makosa!. Miongoni mwa madhaifu ya JK ni kupenda sifa, kwa hiyo usitegemee kukubali makosa wala kukubali kumwajibisha yoyote katika serikali yake!.

Lets wait and see!.

Beloved president!!!!!!!!!!!!
 
The biggest mistake is to keep people you personally like in the positions where they are incompetent
 
Umenena mkuu, Kikwete kama atawatumia washauri wake wa siku zote, leo unaweza ukawa mwanzo wa mwisho wa Utawala wake, ninaamini akiendeleza tabia za kuwakandamiza watu anao vutana nao itamuia vigumu kwa hili la madaktari tusubiri tuone. Ila wakati mwingine ninamuonea huruma Urais ni kazi ngumu sana kwa watu wa uwezo wake.
Madhara ya kusikiliza ushauri wa masokwe ni hatari sana......
 
Kwa hiyo inaonekanaa watu wengi wanatarajia Kikwete atawa disparage madaktari na akiffanya kitu kingine chochote itakuwa ni "out of character" kwa kweli.

Mkuu Mzee Mwanakijiji asante sana kwauchambuzi wako mikweli kabisa ninacho weza kusema Kikwete hawezi kuwajibika yeye kama rais kwani hana uchungu na watu wake anaowaongoza kwanza kungekuwa na hulka ya kuwajibika nchi isingekuwa hapa ilipo kwanza kila kukicha migogoro zuluma manyanyaso utafikiri nchi haina rais halafu vitu hivi vyote vinafanyika kukiwa na mawaziri wanao weza kulitatua juzi wazee kwa vijana kwa watoto waliandamana kupinga kunyanganywa mashamba yao na wanajeshi Arusha mbaka wananchi wanafanya hivyo hakuna waziri wa ardhi nyumba na makazi napata shida Kikwete anawapata wapi mawaziri wake? leo natarajia Kikwete kuimba taarabu mipasho na wazee wake wa ccm badala ya kutatua matatizo je Kikwete hawezi kuongea na madaktari wenyewe mbaka akaonge na wazee wa ccm???
 
Back
Top Bottom