Kikwete kweli anawajali watoto na wazee? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kweli anawajali watoto na wazee?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Msongoru, Aug 31, 2010.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimeshangazwa na mabango mengi yenye picha za RAIS anayemaliza muda wake, akiwa na watoto wadogo na wazee. Picha hizi huwa zinaandikwa kwamba chama kinajali watoto na wazee na rika zote, hivyo wanatoa wito kwamba tuchague chama hicho. Swali langu ni hili je ni kweli kwamba kujali watoto wa TAIFA hili ni kwa kuwaweka baadhi yao kwenye mabango? Elimu wanayopewa, matibabu wanayopewa na mazingira mazima wanayoishi ni kweli kwamba WANAJALIWA?
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  WAZEE wa jumuia ya afrika ya mashariki wanalala nje ya ofisi za reli ya kati, mvua ni yao, jua ni lao, hadi sasa ni zaidi ya miaka 3 wako pale bila msaada wowote. Hakuna taifa duniani lisilojali wazee walioitumikia serikali kwa moyo wa uzalendo na kisha kunyanyaswa kama Tanzania chini ya chama tawala ccm.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mojawapo ya mabango ya kampeni za ccm, linamwonyesha JK akinong'onezwa jambo na mzee mmoja, likiwa na ujumbe

  "JK ANAWAJALI SANA WAZEE"
  .

  Picha hizi zinaonyesha jinsi JK anavyowajali wazee.


  [​IMG]

  Wazee wastaafu wa jumuiya ya Afrika ya mashariki wakiwa nje ya lango kuu la kuingilia ikulu, wakitegemea Rais Kikwete angewajali ili awasaidie walipwe mafao yao, lakini waliondolewa kwa virungu vya polisi

  [​IMG]

  Hapa siyo uani mwa nyumba ya mtu, la hasha, hapa ndiyo makazi ya wastaafu wa jumuia ya afrika ya mashariki nje ya ofisi za makao makuu ya shirika la reli kando kando ya barabara ya UHURU, wameishi hapo kwa zaidi ya miaka mitatu.

  [​IMG]

  Baada ya juhudi zao za kudai haki yao kugonga mwamba mgumu wa serikali ya chama cha mapinduzi, wastaafu waliamua kufunga barabara ya H.Mwinyi eneo la daraja la selender. Waliondolewa kwa nguvu za jeshi la polisi

  [​IMG]

  MAMA alishindwa kujizuia jinsi ZULUMA inavyozuia mafao yao. Analia kwa uchungu mkubwa akijigaragaza barabarani.

  [​IMG]

  Vikongwe wa Afrika ya mashariki wakila mkong'oto kutoka kwa askari polisi kuwaondoa barabarani


  [​IMG]

  [​IMG]

  Serikali ya JK ilitumia kila aina ya zana kuhakikisha hawa wazee wanazibitiwa. Hapa ni nje ya ofisi za shirika la reli.
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Na mkileta za kuleta nitawapa vichwa hadi muugue malaria:

  [​IMG]
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Au we bonge unasemaje?

  [​IMG]
   
 6. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 156
  Trophy Points: 160
  Mbona mnatisha sasa! Hivi CCM wamefikia kiasi cha kuwanyanyasa hata wastaafu!!!! Lol ! SAA YA UKOMBOZI IMEKARIBIA KWA HAWA WAZEE NI NANI AWAARIFU?
   
 7. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sio wazee tu, Kikwete anajali hata watoto, kawapatia maji safi ya kunywa:

  [​IMG]
   
 8. M

  Mutu JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani dogo ndio makamu mwenyekiti CCM AHAAAAAAAAAAAAAAAA na nyie vibaraka mnakubali utawala wa koo ,bado koo ya makamba katibu mkuu makamba naibu katibu mkuu January ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 9. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #9
  Sep 2, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jk jk jk jk! AN WARNING YOU
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanakuja humu kutetea kwa nguvu serikali dhalimu ya Kikwete bila kuangalia adhari kama hizi za wazee wetu kudhulumiwa haki yao kwa muda mrefu.
  [​IMG] [​IMG]
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Labda anajali wazazi wake na wa Salima tu!
   
 12. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  eti viongozi wa baadaye wa tanzania - kaaa!!
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Hawa wazee hawajui huu ndiyo wakati wa kudai haki zao, hii ni weak point nyingine ya JK na CCM mzee umetukumbusha.
   
 14. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Nichagueni nimwage Bajaji 400 kila wilaya kwa ajili ya kinamama wajawazito - tuone sasa CHADEMA nao watamwaga nini? hawana jeuri wale watani zangu tu teh teh teh
   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  anawajali sana.....mbona huwa anawaita mara kwa mara pale ikulu kuwalisha pilau na kujifanya kuongea na wananchi kupitia wazeee?????
  anawajali kwani wakienda wanaondoka na posho za maana wakiwa wamelishwa tupilau...jk bwana we acha tu...hao wengine ni wale wazee ambao uraia wao una mashaka kwa jk ndiyo maana wanalalamika sana..
   
 16. B

  Bobby JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Luteni thanks. Infact yapo mabango mengi tu nikiyaona huko barabarani nasikia kutapika naishia kujuta kwanini macho yangu yameona udhalimu huo. Moja liko pale njia panda ya kigogo, mgombea wa ccm anaonekana akimsikiliza mtoto albino ujumbe wake ni jk ni msikivu. I feel very sorry hivi kama huo ndio usikivu atawasikiliza wangapi kwa style hiyo? Haya msikivu wakati matendo yake ni kuwalinda mafisadi mwanzo mwisho? Rasilimali za nchi ameziacha zinaliwa na wachache huku akiacha maskini wakiishi maisha mabovu kuliko maelezo then tunamwita msikivu kipi hicho anachosikia? anawasikiliza nani zaidi ya mafisadi? Hatuwezi kununuliwa kirahisi namna hii.

  In my very honest opinion hakuna hata jambo moja alilofanya jk toka aingie madarakani kuonyesha anawajali masikini na kwamba wao ndio maboss wake wenye nchi-narudia HAKUNA kila kitu ni business as usual hakuna priorities basi tu tunaenda ili mradi. Maisha bora aliyoahidi 2005 imekuwa story no wonder kwa aibu kubwa sijamsikia akitamka huo upuuzi tena this time around.Pole baba na team yako!
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  huku mexico upuuzi huu huwezi kuuona
   
 18. b

  bobishimkali Member

  #18
  Sep 2, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kila mtanzania ana haki ya kudai haki zake kwa kufuata sheria na taratibu zilizoko.Tatizo lililojitokeza kwa hawa wazee wetu wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki ni kwamba walifanya maandamano bila ya kufuata sheria na taratibu za nchi.Kama wangefuata taratibu zote za kufanya maandamano, wasingezuiwa na vyombo husika.
   
 19. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Vile vizee ndio viganga vyake na pale vilikuwa vikimpa dawa na maagizo ya namna ya kuzitumia ndumba hizo
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Madai yao ni ya tangu mwaka 1977 jumuia ilipovunjika leo hii ni miaka 33 imepita hawajalipwa, bado huna haya kutamka kuwa wafuate "Sheria na taratibu" ?
   
Loading...