Kikwete kwa hili sikubaliani na wewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kwa hili sikubaliani na wewe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kichenchele, Sep 30, 2010.

 1. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  nimekuwa nikisikia ahadi nyingi sana zinazoendelea kutolewa na wagombea urais wa vyama mbalimbali vilivyosimamisha wagombea, hali hii inanifanya nijiulize hawa wagombea wamekuwa wakiishi nchi gani maana kama ni matatizo ya watanzania wameshayaona muda mwingi na si kusubiri mpaka kipindi hiki cha uchaguzi kifike, kilichonitia kichefuchefu ni ahadi iliyotolewa na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, ya kwamba kama atachaguliwa atajenga reli kutoka dar-es-salaam hadi mikoa yote ya kanda ya ziwa, mimi ningemuona mwenye hoja kama angesema atahakikisha reli yetu iliyopo inaboreshwa kwa kiwango cha juu, sasa hii iliyopo ni taabani unasema utajenga nyingine, huku ni kuwaongopea watanzania, toweni hoja zenye mantiki na si kutoa verse ambazo haziimbiki,

  MUNGU IBARIKI,TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU WABARIKI WAAFRIKA,
   
 2. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  The believer is happy, the doubter wise.
   
 3. MANI

  MANI Platinum Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,872
  Trophy Points: 280
  Kichenchele umesahau kutokomeza jembe la mkono na kuweka matrekta?
   
 4. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Hotuba za JK zinafaa zikusanywe na iwe kama moja ya vitabu vya vichekesho kama vile HEKAYA ZA ABUNUWASI
   
 5. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,185
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  Mbona hiyo ni chamtoto?. Kasema mkimchagua mtasahau watanzania kutumia jembe la mkono. WAKATI SASAHIVI YEYE NI RAIS NA WAKULIMA WANAOTUMIA JEMBE LA MKONO NI KAMA ASILIMIA 90%- HUYU MUUNGWANA anajua anachoongea!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!![​IMG]
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu, hapa umeongea. Na bila shaka kitabu hicho kitapendwa sana.
   
 7. e

  emalau JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  ha ha ha ha ha na uwanja wa ndege misenyi !
   
 8. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu hilo ni kweli hasa tukiweka chapter moto moto kama vile
  1. Kauli tata za Jk- wanao pata ukimwi ni kiherehere chao
  -wanaopata mimba shuleni ni kiherehere chao
  -wezi waliorudisha hela zetu hatuna haja ya kuwajua
  - kelele za mwenye nyumba... chitalilo we dunda na elimu feki!
  2. wAFANYAKAZI - SIHITAJI KURA ZENU
  - Mkigoma ffu watawachapa mfungwe plasta kwenda kazini
  - Hata myaka 8 ijayo mishahara haingezwi ngo!
  3. Afya mgogor - raisi anaye dondoka ovyoovyo mbele ya hadhara
  4. Vascodgama wa kizazi cha dot.com
  5. Uraisi wa nchi kuwa swala la kifamilia.. (baba mama na wana)
  6. Raisi aliye wahi kudaganywa kuliko wote duniani mfano
  - Kijana Bashe si raia
  -

  oh... the list is so long.. nahisi kitabu kitakuwa kikubwa kama encyclopedia volume '16'
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  acha utani veve, alisema hii kitu? Hivi hana historians kwenye team yake ya kampeni?

  mimi nitachora cover yake na illustrations za ndani mkuu.

  nimeshawaambia kuwa YES HE CAN! kwani kuna ugumu gani kutandaza reli ya plastiki tanzania nzima kwa ajili ya treni ya mabua? Tatizo la JK anadhani tupo ktk zile zama za kukubaliana na ule utabiri elekezi wa REDET kuwa anakubalika saaana na ni maarufu kuliko baraza lake la mawaziri. hakujua kuwa alipowatuma akina mkandala and the gang waliacha maswali mazito akilini kwetu kuwa sisi hatukumchagulia hilo baraza, kama mawaziri hawafai basi aliyewachagua ndiye zaidi ya hapo.
  Rais mstaafu mtarajiwa since october 31, 2010 JK, nakutakia maisha marefu na afya njema baada ya safari ndefu kujaribu kuiongoza tanzania. Sheria ya pensheni mliyojiwekea naamini itakulinda hutolala njaa na maisha yatakuwa mswano tu.
   
 10. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  aiseee huyu mwana jf aliyeleta hoja ya kutunga kitabu/vitabu vya ahadi za Jk ameongea la maana kama kuna uwezekano jamani wekeni mkazo ktk hoja hii ili iwezekane tunao wataalamu waliobobea ktk utunzi na uandishi wa vitabu, mawazo na michango ya hoja itatoka humuhumu JF
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,950
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Kitatumika pia kufundishia watoto wetu shuleni kwenye somo la uraia, civics, na general studies au English literature jinsi gani utapeli unavyofanyika kwenye siasa za Tanzania kama wenzetu wa Nigeria na kile cha kwao kinaitwa "A Man of the people". Tofauti ni kwamba cha kwetu kitakuwa 'non-fictional' na kile ni 'fictional'.
   
 12. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Akili za huyu jamaa Jk nadhani anayezielewa ni mama SALMA tu, na ndio maana hadi leo wanaishi pamoja. lakini watu wengine wanamsupport ili CCM ishinde.
   
 13. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 60
  Naunga mkono hoja 100%
   
Loading...