Kikwete kuzindua Tasaf kukomboa kaya maskini

Temporary01

JF-Expert Member
May 12, 2011
260
70




Waandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuzindua awamu ya tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), ambayo inalenga kutoa fedha moja kwa moja kwa kaya maskini nchini ili kujikwamua na uchumi duni.

Awali Tasaf ilikuwa ikitoa fedha kwa miradi mbalimbali ya jamii kama ujenzi wa shule, vituo vya afya, nyumba za walimu, ujenzi wa madaraja na miradi ya watu wenye mahitaji maalumu kama walemavu na watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga alisema Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa uzinduzi huo utafanyika kesho mjini Dodoma."Awamu ya pili imekuwa na mafanikio makubwa… madhumuni ya awamu ya tatu ni kuendeleza mafanikio yaliyopatikana awamu ya pili ili kuwezesha kaya maskini kuongeza kipato na fursa za kuinua kiwango cha matumizi yao," alisema Mwamanga.

Alisema awamu hii itaendeshwa kwa kipindi cha miaka 10 na itakuwa na awamu mbili za miaka mitanomitano.Ili kufanikisha mpango huo, Mwamanga alisema hadi jana wafandhili na Serikali, walikuwa wamechangia dola 272.9 milioni za Marekani takriban Sh436.64 bilioni.

Alisema fedha hizo zitatumika kwenye kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya awamu hiyo.
Kuhusu mpango huo wa kuzisaidia familia maskini moja kwa moja, Mwamanga alisema ulitokana na mradi wa majaribio uliofanyika wakati wa utekelezaji awamu ya pili na kuonyesha utaweza kuondoa umaskini unaozikumba kaya nyingi nchini.

Alisema mkakati huo utasaidia kaya hizo kutatua matatizo mbalimbali kama vile elimu, afya, maji na utawalenga wazee, watoto na miradi ya kuongeza kipato kwa wenye uwezo wa kufanya kazi.Akizungumzia uzinduzi huo, Mwamanga alisema baadhi ya kaya maskini zilizofaidika na mradi wa majaribio zitatoa ushuhuda.

Kuhusu awamu ya pili ya Tasaf, Mwamanga alisema licha ya kuonyesha mafanikio, changamoto kubwa ilikuwa ni uwezo mdogo wa fedha wa kutekeleza miradi yote iliyobuniwa na wananchi."Miradi iliyopangwa kutekelezwa ilikuwa 5,950 sawa na asilimia 10, wakati maombi kutoka kwa wananchi yalifikia 102,275," alisema Mwamanga.

Akizungumzia jinsi kaya maskini zitakavyopatikana kwa awamu ya tatu, Mtaalamu wa Utafiti na Ushirikishaji Mambo ya jamii wa Tasaf, Amedeus Kamagenge alisema watatumia mikutano mikuu ya kijiji na mitaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom