Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,437
- 113,445
Wanabodi,
Uchaguzi umemalizika, japo ni kwa mtindo wa sadakalawe, mwenye kupata, kupata hata kama ni kwa kuiba, bado kapata tuu na mwenye kukosa, kakosa hata kama ni kwa kuibiwa, kudhulumiwa, kuonewa na kunyanyaswa, the bottom line ni kakosa.
Japo ni muhimu sana kukaa chini na kutafakari historia ya tulikotoka, tulipo ili tuone tunapokwenda, pia ni muhimu zaidi kutokumbatia yaliyopita ni ndwele, tungange yajayo for 2015, hivyo sasa macho yetu yote tuyaelekeze Dodoma.
Wabunge wanakusanyika rasmi Dodoma kuanzia kesho, kwanza watasajiliwa. Baada ya hapo, wataaungana na wenzao wa viti maalum. Siku ya Ijumaa asubuhi, Watamchagua Spika na naibu spika na zoezi la kuwaapisha litaanza rasmi. Watapumzika wikiendi hii kujilia kuku zao na wengi wao kutambulishwa rasmi eneo la Mnadani.
Update:
Rais, ameshaitisha tangazo la kuitisha bunge kuanzia leo.
Wabunge walioko Dar, wanajisajili pale ofisi ya Bunge, wengine watajisajilia Dodoma.
KAikao cha kwanza cha Bunge, kitaanza Alhamisi kwa vikao vya kamati za siasa za vyama kupendekeza majina ya wagombea uspika.
Saa 10:00 jioni ya Alhamisi ndipo bunge litapokea majina ya wagombea uspika.
Mkutano wa kwanza wa Bunge, utaITISHWA Ijumaa asubuhi kwa kusomwa tangazo la rais kuitisha Bunge kikifuatiwa na uchaguzi wa spika atakayeapishwa na Katibu wa Bunge, wimbo wa Taifa utapiogwa ukifuatiwa na dua na kiapo cha utii kwa wabunge wote.
Jumamosi, Jumatatu kuapishwashwa kutaendelea.
Jumanne ndio jina la waziri mkuu litafichuliwa, Waziri Mkuu atatoa hotuba ya shukrani, na utafuatia uchaguzi wa naibu spika.
Jumatano asubuhi, Waziri Mkuu mpya (wa zamani kama alivyo rais mpya) ataapishwa rasmi Ikulu ya Chamwino, saa 10:00 jioni ndipo rais atalihutubia Bunge kwa hotuba ya malengo mfano wa 'State of Nation Address' ambapo litaahirishwa rasmi mpaka kikao cha Januari, 2011 na kumalizia kwa tukio la kugonganisha glasi usiku pale katika viwanja vya bunge.
Alhamisi atatangaza baraza jipya la mawaziri. Jumamosi asubuhi, baraza hili litaapishwa rasmi katika viwanja vya Ikulu. Jumatatu inayofuatia, mawaziri wa zamani, watakabidhi ofisi kwa mawaziri wapya, serikali mpya ndio itaingia kazini rasmi.