Kikwete kuwa makini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kuwa makini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Vin Diesel, May 7, 2011.

 1. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Siku hizi imekuwa kama desturi, kila kukicha utasikia kuwa Waziri Mkuu 'aliyejiuzuru' kasema hili mara kafanya lile na yote ayafanyayo au kuyasema hayana tija kwa mustakabali wa nchi yetu.

  Hapa namzungumzia Waziri Mkuu aliyejiuzuru terehe 7 mwezi Februari mwaka 2008 mbele ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa KASHFA ya RICHMOND. Vyombo vya habari vimeandika sana na watu mbali mbali wamesema na kuchambua kwa kina juu ya KASHFA hii ya RICHMOND. Sihitaji kurudia kuandika juu ya sakata hili.

  Kinachotokea kwa “Kiongozi” huyu si ajali, bali ni mavuno ya mbegu alizopanda. Watanzania wanakumbuka wazi kuwa mwaka 1995 “Kiongozi’ huyu alitupa karata yake ya kuomba kuliongoza Taifa hili ktk nafasi ya juu kabisa ya Urais kupitia Chama chake, lakini kwa msaada mkubwa wa Mwenyezi Mungu kupitia Hayati Baba wa Taifa Mwenyeheri Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere, jaribio hilo lilizimwa. Mwenyeheri Mwl.

  Nyerere alisema wazi kuwa “Bwana Huyu” HAFAI KUWA KIONGOZI WA NCHI kwani ni mtu mwenye TAMAA kubwa sana ya MALI na MADARAKA.

  Lakini kwa kutumia nguvu ya fedha “alizoziiba” alipokuwa Serikalini, na ujanja mwingine 'Waziri Mkuu' huyu mwenye weledi wa sanaa akafanikiwa kurudi madarakani na kupanda ngazi za uongozi na hamadi akaukwaa u waziri mkuu.

  Waswahili wanasema jasiri haachi asili kwani ndani ya muda mfupi akapiga dili ya mamilioni ya shilingi, akakwama kwenye dili ya umeme ya RICHMOND hadi akalazimika kuachia ngazi.

  Leo hii 'MSTAAFU' huyu anafanya kila jitihada kujisafisha ili aingie “patakatifu” mwaka 2015, japo haoni kwamba kwa jaribio la yeye kuingia Ikulu ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano.

  Baadhi ya washirika wake muhimu ktk kambi yake wameona ugumu huo, na sasa wameamua kutafuta njia mbadala ya kuwasogeza mahala “patakatifu”.

  Jitihada anazozifanya za kujisafisha ili afikiriwe kuliongoza Taifa hili zinamgharimu kiasi kikubwa sana cha fedha, na mbinu anazozitumia zina hatari kubwa kwa usalama wan chi yetu.

  Pamoja na mambo mengine, amekuwa akitumia baadhi ya vyombo vya habari kumsafisha, lakini baya zaidi, ni pale anapomchafua Rais Kikwete na familia yake.

  Ameleta mfarakano mkubwa ndani ya Chama chake, na sasa tunashuhudia, baadhi ya wenyeviti wa Chama chake wanapita sehemu mbali mbali kuhubiri “uasi” dhidi ya maazimio yaliyofikiwa hivi karibuni ktk vikao halali mkoani Dodoma.

  Hakika, kwa haya anayoyafanya “mstaafu” huyu yasingeweza kuvumilika kwa ma-Rais waliopita, kwani ana kila hatia ya kujibu.

  Rais Kikwete anatakiwa kujua kuwa yeye ni Rais wa wengi, na hivyo anatakiwa kusikiliza na kutekeleza ya wengi, hata Ponsio Pirato lilipomshinda kwa Nabii Issa (Yesu Kristo) alisema “VOX POPULI, VOX DEYI”, maana yake “SAUTI YA WENGI, SAUTI YA MUNGU”.


  Nchi hii ni masikini saaana, umasikini huu unatokana na kuwa na viongozi wasiokuwa na mipango mizuri ya kututoa ktk dimbwi hili la umasikini. Maendeleo ktk nchi yeyote duniani huhitaji vitu vifuatavyo: ARDHI, WATU, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA.

  Mheshimiwa Kikwete, nakushauri uchukue hatua madhubuti sasa, kwani si muda mrefu watanzania wataanza kuhoji ufanisi wako kwa kigezo cha marafiki zako “wanaonuka” machoni pa wananchi.

  Ponsio Pilato alimtoa Yesu kwa wayahudi ili asulubiwe japo yeye hakuona kosa lolote juu yake na sie twamtaka 'mstaafu' huyu ahukumiwe na kama ni msafi basi damu yake na iwe juu yangu na kizazi changu chote.

  Inasikitisha sana kuona wezi wa kuku wamefungwa jela wakati wezi wa mabilioni wanatanua na Rais anapata wasaa wa kuonana nao, kama anaonekana msafi basi namuomba umlete Kariakoo aone wenye nchi yao watakavyo mlaki kwa hoi hoi, nderemo na vifijo.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA….
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  siyo kikwete kuwa makini, bali watanzania wawe makini na serikali ya kikwete
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kikwete asipokuwa muangalifu hawa mapacha watatu kwa mambo wanavyoyafanya wakati huu , watamuwahi na by the time anastuka itakuwa HAMAD!! It will be too late to recover!! As he might as well know timing in politics is very importatnt.
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sio kwa mapacha 3 tu, hata kwa vyama vinavyo endeleza udini na ukabila kama CDM
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  May 7, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hoja yako ni nzuri lakini haina mashiko! Unapomjadili huyu mwizi Edward N.Lowasa yakupasa usimwache Jakaya M.Kikwete mtu mtanashati mwenye tambo na tabasamu la kudumu! Mtu aliyewekwa Magogoni kwa maslahi ya Lowasa, Rostam na Chenge!!
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hv mnatuhakikishia kuwa ccm ni yawaislam tuihame!??? mimi mbona sielewi vizuri mtangaze kabisa basi tutoke huku!
   
 7. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hii ni banana republic ndiyo maana kila mmoja anaweza kujisemea anachotaka
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa mkuu... lakini uzuri ni kuwa kuna uwezekano mkubwa njama zao za kutaka kumpiku JK na kupata nomination ya CCM itakuwa ni kuandaa ushindi wa upinzani kwa sababu watanzania wengi wameshaamka na wanajua kinachotokea. Waache tu wajisafishe kwa maji taka waone shughuli yake
   
 9. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #9
  May 7, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Huu ni wakati wa Rais kuchukua hatua
  ngoja ngoja hii itatibua mambo.
   
 10. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mi nilishasema kazi tunayo fufuka mwenye heri JK halisi.
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Rais yupi achukue hatua?, mbona kwenye orodha ya awali ya "List of shame" huyu RAHISI wako yumo na ndo unataka achukue hatua?!, mbona updated"List of shame" hata mwanaye yumo- unataka achukue hatua gani?, amchukulie nani?.
   
 12. K

  Kivia JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ACHA UNAFIKI WEWE, NANI KAKUTUMA ? Nani kakwambia lowasa sio mtu safi ? Si chama chake kilishasema kujiuzulu kwake ni ajali ya kisiasa ? Tumwache mzee wa watu apumzike salaama na ale pensheni yake.
   
 13. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Rais hawezi kuchukua hatua kwa sababu they have sailed in the same boat from 1992 to 2008 na hawakukutana barabarani
   
 14. S

  Stany JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 278
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  dah! Kaz ipo!!
   
Loading...