Kikwete: Kutokana na utoaji hafifu wa Elimu nchini, kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050

Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.

My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.

Shida yao wampoteze mh rais Samia kwa kujifanya washauri kumbe Wana lao Jambo

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.
Kuzeeka kuna mengi keshaanza kupoteza kumbukumbu

Kwa hiyo ikifika hiyo miaka serikalini na mahakamani tutaajiri wazungu kufanya kila kazi ya ajira iliyoko serikalini na kwenye mahakama zetu?
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.

My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.

====

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu nchini kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 wakati akizindua kongamano la elimu linalojadili ufadhili wa elimu lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet) jijini Dar es Salaam.

Akieleza utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, amesema elimu inayotolewa barani Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea.

"Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets. Tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika. Kwa waliopo shule wengi hawamalizi shule. Wengi wanaishia njiani. Asilimia 67 wamemaliza shule, asilimia 33 ni idadi kubwa," amesema Kikwete.

Amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu na maendeleo ya teknolojia kuna janga la ukosefu wa ajira linakuja.

"Ifikapo 2050 asilimia 50 ya kazi zitafutika, kwa sababu ya matumizi ya mashine. Kutakuwa na magari yasiyotumia dereva. Unataka usafiri, unaita Uba, unatumia simu yako inakuja inakupeleka sehemu husika labda Ubungo Plaza au Millennium Tower," amesema.

Advertisement

Amesema mbali na ukosefu wa ajira, idadi ya watu barani Afrika itafikia watu bilioni mbili, “kama watu hao hawana ujuzi unafanya nini? Sijui itakuwaje. Kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii."

Akisisitiza matumizi ya teknolojia, Kikwete ameshauri kuwepo na uwekezaji katika elimu ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji, wawe washiriki wa uchumi.

"Kunatakiwa kuwepo na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ufundishaji. Kila shule inatakiwa kuunganishwa na intaneti," amesema.

Huku akitoa mfano wa janga la corona, Kikwete amesema limethibitisha jinsi ukosefu wa teknolojia unavyoathiri ufundishaji.

"Tumeona wakati wa corona, moja hatua zilizochukuliwa ni kufunga shule. Wanafunzi wetu hawakusoma, wanacheza rede, lakini nchi zilizoendelea shule zilifungwa na watoto wakaendelea kusoma.”

"Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.

Kuhusu Elimu jumuishi ameitaka Serikali na wadau kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa kukosa elimu.

"Wengine wanadhani msichana ni wa kubaki jikoni. Wengine wameachwa nyuma kutokana sababu za kisiasa.

Tunatakiwa kuhusisha mashirika yasiyo ya kiserikali kuchangia elimu," amesema.

Awali akimkaribisha Kikwete mwenyekiti wa Tenmet, Dk John Kalage ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya HaliElimu amesema kongamano hilo litajadili kwa kina njia za ufadhili wa elimu nchini.

Ni kwamba tatizo la ajira litakuwa limekwisha..?
 
Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology

Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine

Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market

So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa

Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
Najaribu kufikiri by 2050 zile boma za Masai zimejaa maroboti yanakamua maziwa na kuchunga ng'ombe.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo ikifika huo mwaka majeshi yetyu yote iwe polisi au JWTZ watakuwa wanaajiriwa wazungu wenye elimu bora?
 
Ukweli mchungu by 2050 kila kitu kitabaki kwenye technology

Hivyo wanaitajika watu ambao wapo tayari kujiajiri, Machine na operators wa machine

Maroobot vile vile yatakuwa yakifanya kazi sehemu kama shelli na super market

So kazi zitakuwa chache au kutokuwepo kabisa

Kikwete ana hoja tuchukue hatua.
Kwa hiyo mahakimu na majaji watakuwa ni hayo maroboti ,mapolisi watakuwa ni hayo maroboti,Leseni za biashara zitakuwa zinatolewa na hayo maroboti,madaktari na manesi watakuwa ni hayo maroboti,WAtoto mashuleni na vyuoni watafundishwa na hayo maroboti au?
 
"Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.
Kumbe Mzee Kikwete ulishaanza kuminya ajira kitambo, je ulipanga kuwatumia kwa lipi walimu waliobakia
 
Anamaanisha kwamba ifikapo 2050 baadhi ya ajira zitakuwa zinafanywa na mashine na marobot. Kwa mfano kiwanda kinachoajiri watu 200 kwa sasa kitakuwa kinaajiri watu 25 tuu yaani 175 wanaobaki watakuwa hawana kazi.
Population itakuwaje mwaka huo? Population ikiongezeka ajira zinaongezeka pia haziwezi kushuka zaweza shuka eneo moja zikaongezeka eneo lingine mfano population ikiwa itaongezeka ajira za madaktari na manesi lazima ziongezeke,pia za walimu,Maaskari na watendaji wengine.Huwezi tu kusema tu kwa sababu kiwandani zitashuka haina maana sekta nyingine kuwa nako zitashuka

Kuongelea kushuka au kutoweka kwa ajira unatakiwa kuangalia vitu vingi kimojawapo ni population je itakuwaje kipindi hicho na itahitaji nini kutoka soko la ajira wa kuwahudumia?
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.

My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.

====

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu nchini kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 wakati akizindua kongamano la elimu linalojadili ufadhili wa elimu lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet) jijini Dar es Salaam.

Akieleza utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, amesema elimu inayotolewa barani Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea.

"Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets. Tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika. Kwa waliopo shule wengi hawamalizi shule. Wengi wanaishia njiani. Asilimia 67 wamemaliza shule, asilimia 33 ni idadi kubwa," amesema Kikwete.

Amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu na maendeleo ya teknolojia kuna janga la ukosefu wa ajira linakuja.

"Ifikapo 2050 asilimia 50 ya kazi zitafutika, kwa sababu ya matumizi ya mashine. Kutakuwa na magari yasiyotumia dereva. Unataka usafiri, unaita Uba, unatumia simu yako inakuja inakupeleka sehemu husika labda Ubungo Plaza au Millennium Tower," amesema.

Amesema mbali na ukosefu wa ajira, idadi ya watu barani Afrika itafikia watu bilioni mbili, “kama watu hao hawana ujuzi unafanya nini? Sijui itakuwaje. Kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii."

Akisisitiza matumizi ya teknolojia, Kikwete ameshauri kuwepo na uwekezaji katika elimu ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji, wawe washiriki wa uchumi.

"Kunatakiwa kuwepo na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ufundishaji. Kila shule inatakiwa kuunganishwa na intaneti," amesema.

Huku akitoa mfano wa janga la corona, Kikwete amesema limethibitisha jinsi ukosefu wa teknolojia unavyoathiri ufundishaji.

"Tumeona wakati wa corona, moja hatua zilizochukuliwa ni kufunga shule. Wanafunzi wetu hawakusoma, wanacheza rede, lakini nchi zilizoendelea shule zilifungwa na watoto wakaendelea kusoma.”

"Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.

Kuhusu Elimu jumuishi ameitaka Serikali na wadau kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa kukosa elimu.

"Wengine wanadhani msichana ni wa kubaki jikoni. Wengine wameachwa nyuma kutokana sababu za kisiasa.

Tunatakiwa kuhusisha mashirika yasiyo ya kiserikali kuchangia elimu," amesema.

Awali akimkaribisha Kikwete mwenyekiti wa Tenmet, Dk John Kalage ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya HaliElimu amesema kongamano hilo litajadili kwa kina njia za ufadhili wa elimu nchini.

Chanzo: Mwananchi
Kwa hiyo wewe unataka Chadema wafanye nini? Yaani sula ni elimu ya Tanzania, wewe mwenzetu unaitaja Chadema. mmmmm! kazi tunayo.
 
2050 ni keshokutwa tu mkuu, Ajira ngumu za mikono zitaendelea kuwepo nyingi. Huu utabiri wa JK ni hewa au baada ya miaka 150 ambapo hatujui hata kama Tz itaendelea kuwepo jinsi ilivyo.

Sasa Chadema na madudu yanayofanywa na ccm na Serikali yao,wapi na wapi?Chadema inahusika vipi kila mradi ccm inachemka,hata kama Chadema wanacheka,na kufurahia,nyie ccm mna vyombo vya habari,watumishi wote wanafata amri Zenu,sasa mnashindwa Nini kupangua hoja,na kubadirisha "narative"?kama mnashindwa,basi ni waumbavu msio na weredi.
Jiwe alipotaka asikike,badala ya kupangua hoja kwa hoja,anafungia vyombo vingine,wanaomkosoa anaua!!!!
Kama midege yenu inafaida acheni uchumi uongee wenyewe,tatizo ni kwamba hakuna mnachojua,hamjui mnapotaka kwenda,njia hamuijuhi,lakini bado mnataka muendelee kushika usukani.
 
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameonya tusipobadilika namna tunavyofundisha watoto wetu basi ajira zote zitatoweka ifikapo mwaka 2050.

My take.
Hii elimu yetu ya kuwafanya chadema washangilie kila baya linaloipata nchi yetu ikiwemo kukamatwa ndege, miradi kukwama , tutashitakiwa MIGA etc bora ifutwe kabisa tuanzishe elimu mpya itakayowafanya chadema wajitambue.

====

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu nchini kuna hatari ya nusu ya ajira zilizopo kutoweka ifikapo mwaka 2050.

Ameyasema hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 wakati akizindua kongamano la elimu linalojadili ufadhili wa elimu lililoandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet) jijini Dar es Salaam.

Akieleza utafiti uliofanywa na tume ya kimataifa ya elimu ambayo yeye ni mjumbe, amesema elimu inayotolewa barani Afrika ilitolewa miaka 50 hadi 70 iliyopita kwa nchi zilizoendelea.

"Sisi bado tunatumia chaki, wakati wenzetu wanatumia tablets. Tuliona kuwa kuna watu zaidi ya milioni 263 waliotakiwa kuwa shule lakini hawapo, kati yao milioni 100 wapo Afrika. Kwa waliopo shule wengi hawamalizi shule. Wengi wanaishia njiani. Asilimia 67 wamemaliza shule, asilimia 33 ni idadi kubwa," amesema Kikwete.

Amesema kutokana na utoaji hafifu wa elimu na maendeleo ya teknolojia kuna janga la ukosefu wa ajira linakuja.

"Ifikapo 2050 asilimia 50 ya kazi zitafutika, kwa sababu ya matumizi ya mashine. Kutakuwa na magari yasiyotumia dereva. Unataka usafiri, unaita Uba, unatumia simu yako inakuja inakupeleka sehemu husika labda Ubungo Plaza au Millennium Tower," amesema.

Amesema mbali na ukosefu wa ajira, idadi ya watu barani Afrika itafikia watu bilioni mbili, “kama watu hao hawana ujuzi unafanya nini? Sijui itakuwaje. Kutakuwa na athari kubwa za kiuchumi na kijamii."

Akisisitiza matumizi ya teknolojia, Kikwete ameshauri kuwepo na uwekezaji katika elimu ili vijana wa Afrika wasiwe watazamaji, wawe washiriki wa uchumi.

"Kunatakiwa kuwepo na matumizi ya sayansi na teknolojia katika ufundishaji. Kila shule inatakiwa kuunganishwa na intaneti," amesema.

Huku akitoa mfano wa janga la corona, Kikwete amesema limethibitisha jinsi ukosefu wa teknolojia unavyoathiri ufundishaji.

"Tumeona wakati wa corona, moja hatua zilizochukuliwa ni kufunga shule. Wanafunzi wetu hawakusoma, wanacheza rede, lakini nchi zilizoendelea shule zilifungwa na watoto wakaendelea kusoma.”

"Nilipokuwa Rais tulianzisha matumizi ya intaneti katika ufundishaji, tuliwekeza sana kwenye mkongo wa Taifa. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha kila shule, hospitali ziunganishwe na intaneti. Mwalimu mmoja wa hisabati afundishe nchi nzima,” amesema.

Kuhusu Elimu jumuishi ameitaka Serikali na wadau kuhakikisha hakuna mtoto anayebaki nyuma kwa kukosa elimu.

"Wengine wanadhani msichana ni wa kubaki jikoni. Wengine wameachwa nyuma kutokana sababu za kisiasa.

Tunatakiwa kuhusisha mashirika yasiyo ya kiserikali kuchangia elimu," amesema.

Awali akimkaribisha Kikwete mwenyekiti wa Tenmet, Dk John Kalage ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi ya HaliElimu amesema kongamano hilo litajadili kwa kina njia za ufadhili wa elimu nchini.

Chanzo: Mwananchi
Hizo ni siasa tu! Hakuna uhalisia wowote kwa kile alichokizungumza mbele ya waandishi wa habari.

Kwa sababu, yeye pia aliwahi kuwa kiongozi serikalini kwa kushika nafasi mbalimbali na hata kuwa kiongozi wa nchi, yaani rais.

Kwa kipindi chote cha uongozi wake, alilifanyia nini taifa kwa upande wa sekta ya elimu? Jibu ni hakuna!

Kipindi cha uongozi wa Mrisho Khalufani Kikwete tumeshuhudia uozo mwingi mno kwenye sekta ya elimu.

Uozo huo uliambatana na upishi wa matokeo ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari yaani "Repression and Falsification of Pupils and Students Academic Results".

Hivyo kupelekea kuzorota kwa mfumo mzima wa elimu kwa kuzalisha wahitimu wasiokuwa na sifa za kuajiriwa au kujiajiri wenyewe kwa kutokukidhi matakwa ya soko la ajira.
 
Duh
 
Back
Top Bottom