Kikwete,kutoa sh.5,000,000 kwa msichana yule ni kama tone baharini.

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Rais Kikwete alipo kuwa ziarani kule Tabora, alitoa Sh.5,000,000 kwa msichana maskini, ambaye si katai, kweli alihitaji msaada kufuatana na hali yake ilivyo.Ni sicho elewa mimi, ni kwa nini kwa msichana yule tu.Kwa vile wako maskini wengi Tanzania,ambao wanahitaji msaada.Utaniambia mbona alitoa mamilloni, ili watu wakope.Jibu lake ni rahisi,mamilioni ya Kikwete sio ya maskini.Ni ya walio nacho, na ndio waliokopa.Na hata hivyo, mkopo kwa maskini hautoi umaskini,unaongeza umaskini.Na hata kama mamilioni yale yangegawiwa vizuri, kila mtu angeishia kupata Sh.10,000 tu.Piga mahesabu uone.Sasa katika hali hii, nadhani jawabu sio kumkopesha maskini,na kumpa maskini yule Sh.5,000,OOO,basi iishie hapo.Jawabu ni pana zaidi.Serikali yetu ni vizuri ikachukua hatua za makusudi kabisa za kuboresha uchumi wa nchi yetu,ili wananchi wetu wawe na maisha bora, na hatimaye waweze kusaidiana wenyewe kwa wenyewe,ndugu kwa ndugu.Rais Kikwete akiwatosa mafisadi hawa, tutaamini kwamba ana nia ya kweli ya kusaidia maskini na nchi yake,kinyume cha hapo,hatumuelewi.
 
Back
Top Bottom