Kikwete kutoa hotuba ya kishindo katika mkutano Mkuu wa CCM - DODOMA.

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Katika kuelekea siku ya mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi tarehe 23/07, ambao ni mkutano mkuu wa"UTAMADUNI" (maana haupo kikatiba), Mwenyekiti wa sasa Mheshimiwa Kikwete anatarjiwa kutoa hotuba ya kishindo.

Kwa maoni ya wana CCM wengi Mhesimiwa Kikwete atatoa hotuba nzito ambayo kwa vyovyote vile itajikita katika maeneo matatu yafuatayo:-

. Utejelezaji wa Ilani ya Chama kwa miaka mitano iliyopita pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka jana uliokuwa mgumu kwa CCM ambayo ilishinda kwa mizengwe.

. Uongozi wake ndani ya Chama na Serikalini ambao pamoja na mazuri kadhaa, umeacha tuhuma nyingi za matumizi mabaya ya rasilimali za taifa na nepotism. Hapa atatarajiwa kujitetea zaidi.

. Kama kawaida yake, atawarushia vijembe wana CCM walioamua kutoka ndani ya Chama haswa swahiba na adui yake mkuu kwa sasa Ndg Lowassa.

. Kubwa zaidi, kuna uwezekano mkubwa wa kutoa hotuba yenye lengo la kumfunga mdomo au speed gavana Magufuli anayetegemewa kufanya mapinduzi makubwa ndani ya Chama na hivyo kuhatarisha maslahi fulani fulani ya "Chama" na "wanachama", Kwa kisingizio cha utamaduni na desturi za Chama.

TUKUTANE DODOMA.
 
Back
Top Bottom