Kikwete kutoa chanjo za saratani kwa wanawake nchi nzima ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kutoa chanjo za saratani kwa wanawake nchi nzima !

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mibikimitali, Oct 19, 2010.

 1. M

  Mibikimitali Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MGOMBEA urais wa CCM, Jakaya Kikwete jana alihamishia kampeni zake jijini Dar es salaam ambako aliahidi kuwajengea wafanyabiashara ndogondogo majengo ya kufanyia shughuli zao kwenye wilaya zote, huku akiahidin chanjo ya saratani kwa wanawake.Tayari wafanyabiashara hao wameshajengewa jengo kubwa la ghorofa pacha linaloitwa Machinga Complex ambalo liko Mtaa wa Lindi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo ambao wameshaanza kulitumia, ingawa biashara bado haijapamba moto.
  Akihutubia mkutano wa hadhara jana jijini Dar es salaam, Kikwete alisema wamachinga wataendelea kupata neema kwa kuwa atawajengea majengo mengine kama hilo lililo eneo la Karume ambalo ni kwa ajili ya wilaya.

  "Hii ni ahadi yangu naitoa tena na tena... tayari tumeshapata wafadhili kutoka China ambao watatoa Sh100 bilioni za kujengea majengo hayo na kila wilaya, tutayajenga mawili," alisema Kikwete.

  Kikwete alitaja maeneo ambayo yatajengwa majengo hayo kuwa ni eneo la soko la Buguruni kwa ajili ya jengo jingine la wilayani Ilala, Tazara na eneo la Temeke Stereo kwa ajili ya wilaya ya Temeke wakati wilayani Kinondoni majengo hayo yatajengwa maeneo ya Magomeni Kondoa na Mbezi Luis, akibainisha kuwa kila moja litakuwa na uwezo wa kuchukua watu 7,000.

  Kwa kuangalia uywezo wa mejngo hayo matano na lile la Mtaa wa Lindi, majengo yote yataweza kuchukua wafanyabiashara 35,000 kwa wakati mmoja.
  Tayari Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilishasema kuwa majengo hayo yako kwenye mpango wake na kwamba lilikuwa linasubiri maombi kutoka halmashauri za wilaya za Dar es salaam ili lipate baraka za kuendelea na mradi huo.

  Kikwete, ambaye anawania kurejea Ikulu kumalizia ngwe ya pili ya miaka mitano, pia aliahidi kusimamia ugawaji wa maeneo hayo ya biashara mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa majengo hayo akitaka kudhibiti ubabaishaji ambao ulijitokeza kwenye jengo la Machinga Complex.

  Kikwete alisema kwamba katika ugawaji wa maeneo kwenye jengo la Machinga, watu wasio na sifa walipewa nafasi kutokana na kuwa na undugu ama urafiki na wagawaji.
  "Ndiyo maana ugawaji ulichelewa sana kipindi kile eneo lile la Ilala kwa kuwa niligundua kuna ujanja unaoendelea pale lakini nilisimama kidete wakapata wahusika," alisisitiza Kikwete.

  Kuhusu wanawake, Kikwete aliahidi kuwa watapatiwa chanjo ya saratani nchi nzima ifikapo mwakani baada ya kuliona tatizo hilo kuwa linazidi kuwa sugu.
  Alisema kwa sasa serikali inatoa chanjo kwa kutumia hospitali ya Ocean Road ili kupunguza tatizo hilo hapa nchini.

  "Hili ni tatizo ambalo limeshakuwa sugu kwa kuwa saratani zipo aina tatu; kuna ya koo, matiti, na ngozi, sasa imegundulika kuwa akina mama ndio wanaopata saratani kwa kiasi kikubwa hapa nchini. Tunaanza nao mwakani kwa kutoa chanjo nchi nzima," alisema mgombea huyo.

  Kikwete pia alisema kuwa katika kuboresha elimu nchini, serikali ijayo itahakikisha inatilia mkazo masomo ya sayansi na kwamba kila mwanafunzi atapata kitabu chake.
  Alifafanua kwamba tayari vitabu vimeshaagizwa kwa ajili ya kutatua tatizo la upungufu wa vitabu katika shule za sekondari zenye mchepuo wa sayansi.
  Kikwete pia aliahidi kujenga miundombinu kwenye eneo la Tazara wilaya Temeke ambako wafanyabiashara ndogondogo wapatao 40,000 wataweza kujenga viwanda vidogodogo.

  Source: http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/5646-kikwete-kujenga-machinga-complex-tano-zaidi-dar.html
   
 2. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili la chanjo huyu baba huwa haelewi au vipi? Chanjo kwa wananawake wote? Angeuliza wataalamu wamwambie chanjo inatolewa kwa nani na kwa namna gani. Mambo ya kutoa ahadi za kudanganya mabaya sana, ahadi imekosewa tangu inatolewa itatekelezwaje? :mmph:
   
 3. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kwanza kabisa hakuna chanjo ya Saratani ya titi, ngozi au koo , huu ni uongo wa mchana kabisa ! Hata nchi zilizoendelea wanawake wanashauriwa kwenda kufanya Mamogram ili waweze kudetect kama wana saratani ya matiti au lah. Sasa kama kungekuwa na Chanjo ya hiyo saratani kwa nini wafanye hizo Mamogram kila mwaka.

  Swali langu ni jee hizi ahadi zilikuwa part ya speech yake au alizitoa tuu kichwani ? Kama zilikuwa kwenye speech then whoever wrote that speech ought to be fired!
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Rufiji,
  Asante. Nilitaka kuuliza hilo jambo la chanjo kwa sababu hata hapa Marekani sijawahi kulisikia. Sasa Dr. Kikwete kalipata wapi?
   
 5. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  kweli watanzania tu RAISI
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndio maana tuna haja ya kuwa na Mdahalo ili maswali kama haya yapate kuulizwa..
   
 7. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Huyu jamaa amepewa nini na hao wanawake?

  aangalie maisha ya watanzania wote,, yeye na wanawake tu...

  Jamani tumpige chini huyu jamaa...

  nimeangalia ahadi zake nikakuta ni zaidi ya trilion 20 sasa atapatawapi!!
   
Loading...