Kikwete kutinga Australia kati ya November na December | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kutinga Australia kati ya November na December

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andindile, Jun 3, 2009.

 1. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Habari zilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima la leo (Jumatano June 3 2009) zinaeleza kuwa Rais wa JMT ndugu Kikwete anatarajia kwenda Australia mnamo mwezi November au December. Aliyemtengenezea njia mkulu wetu ni waziri Membe aliyetembelea Australia hivi karibuni kutokana na mwaliko wa waziri wa mambo ya nje wa Australia ndugu Steven smith. Inasemekana kuwa safari tunazolaumu kuwa zimezidi kupita kiasi, mkulu hazitengenezi mwenyewe bali hutengenezewa na wizara ya mambo ya nje. Hii ni kutokana na kauli ya Mheshimiwa Masilingi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alipokuwa ana kamati yake wakikagua mahesabu ya wizara hiyo nami namnukuu "kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wizara hiyo (wizara ya mambo ya nje), tayari rais Kikwete amepata mwaliko mwingine wa kufanya ziara ya kikazi nchini australia, kati ya Novemba na Desemba" mwisho wa kunukuu.

  Je Kikwete kabla ya kwenda Australia atatembelea nchi zipi?
  Je kuna haja ya kumwekea limiti ya safari Rais wetu?
  Je tuunde wizara ya mambo ya vijijini ili ishugulikie mialiko ya rais kwenda vijijini ili akahamasishe uzalishaji na uboreshaji wa miundombinu huko?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Atarudi tena Marekani September. UN
   
 3. BrainPower

  BrainPower Senior Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Questions that immediately come in mind,

  a) What benefits will these trips bring ?
  b) What are the opportunity costs ?

  Then weigh them against each other

  Mfano Kama matokeo ya ziara hii ni Australia kufungua embassy Tanzania itakuwa imezaa matunda mazuri. Kwasababu ilivyo sasa hivi hatuwezi kupata visa kwenda Australia mpaka tupeleke medicals , applications ubalozi wao Nairobi ? Its a big headache. Ni aibu, Hata Zimbabwe na ugomvi wao wote lakini ina ubalozi wa Australia.

  Sasa kama hii trip inalenga kwenye mazungumzo tuu lah ! bora wasaidizi wake (mawaziri) wafanye hayo mazungumzo. Au atumie Skype bwana. I think the opportunity cost is high for only this reason.
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  JK anajisahau kuwa sasa ni Raisi na Sii tena Waziri wa Nje!
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Wizara ya mambo ya nje haiwezi kutengeneza safari za Rais bila ridhaa yake; hii yote ni jitihada za wazi za wapambe wa Kikwete kutaka kutetea UVASCO DAGAMA wake. Safari nyingi anazofanya hazina tija na zingeweza kufanywa na wasaidizi wake na kuokoa fedha nyingi za walipakodi zinazotumika kwenye safari hizo! Mfano ni hii safari ya juzi kwenda kuonana na GOOGLEna IBM, nadhani waziri mwenye dhamana ya tekinolojia angefaa zaidi kwenda huko kama ilikuwa lazima!!
   
 6. M

  Mfalme Member

  #6
  Jun 3, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu, mimi ni mgeni hapa. Tuko pamoja!.

  Duh! huyu muheshimiwa nadhani amechukuwa tu uraisi kwa maslahi binafsi, lakini kazi anayoipenda ni ya uwaziri wa mambo ya nje. Sasa siangeifuta tu hiyo wizara ya mambo ya nje akaisimamia mwenye na akajiita raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na waziri wa mabo ya nje....?. Halafu kibaya zaidi ni kila anaposafiri na huyo waziri Membe yuko naye ubavuni.
   
 7. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Wengine Rose garden lazima tutinge.
  Libeneke la ma Miss, twanga pepeta...na dansi zote tumo humo humo
  Faida iko wapi?
  Mwacheni Mheshimiwa na Safari zake

  Atakuja kuhukumiwa pale itakapothibitishwa hayo siyo kwa manufaa ya Wananchi.
  Anaelewa fika Wakati wake ni tofauti na waliompita, anaelewa hilo fika.

  Sitoshangaa kama akautwika. Mzigo wa Mafisadi wanaomchekea sasa hivi.

  A perfect everything...A perfect scapegoat! Kapish
   
 8. H

  Heri JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2009
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Probably ataingia kwenye Giuness Book of Records as being a President widely travelled. He will possibly cover may be 90 % of the world , North Pole and South Pole inclusive.
   
 9. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Re: Kikwete kutinga Australia kati ya November na December
  Probably ataingia kwenye Giuness Book of Records as being a President widely travelled. He will possibly cover may be 90 % of the world , North Pole and South Pole inclusive.


  mbavu sina kwa kucheka.......:)
   
 10. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mimi naona nasisi twapoteza muda wetu, tulimchagua tumuache amalize kipindi/vipindi vyake, kazi kwetu ni kujifunza kwa ajili ya kuamua tofauti baadaye.
   
Loading...