Tanzania sasa hivi siyo nchi inayohitaji siasa sana bali mawazo ya kuendeleza nchi. Imefikia wakati wa Kikwete kukaa kikao cha chai na Slaa na kuchukua mawazo ni vitu gani vya kufanya kupeleka nchi mbele. Tatizo la kuchukua mawazo ya CCM pekee ni kwamba wengi wao wanatoa mawazo kwa manufaa yao binafsi ya kikazi na hivyo mawazo yao mangi si ya ndani au ya uwazi. Huu ni wakati wa kuchukua mawazo kwa watu wanaofikiria tofauti na kwa manufaa ya nchi na sio CCM. Kuna tatizo kubwa la utendaji shule za watoto hazifanyi vizuri, Madaktari wanakimbia nchi kila siku, reli imechakaa, umeme bado mgao mpaka leo, bei ya mafuta juu, bei ya kuingiza vifaa vya biashara juu hivyo tatizo ni kubwa na kwa sasa unahitaji nchi nzima kufanikiwa