Kikwete kushuhudia matatizo ya wananchi miaka minne baadaye! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kushuhudia matatizo ya wananchi miaka minne baadaye!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 24, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kikwete atatembelea maeneo mbalimbali ya Dar kesho kuangalia matatizo ya maji yanayowakabili wananchi. Huu ni mwaka wa nne wa utawala wake na hatimaye amegundua Watu wa Dar wanamatatizo ya maji safi na maji machafu (usiniulize tofauti). Wananchi wanatakiwa kujitokeza "kwa wingi" ili kutoa "kero" zao kwa Rais - kwa mujibu wa RC Lukuvi.


  Naweza kujua Rais ataahidi nini: "Serikali ina mpango madhubuti wa kutatua matatizo haya na wahisani mbalimbali wamekwishapatikana kusaidia ujenzi wa mitaro na utandazaji wa mambo mapya ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi".

  Kwanini wakazi wa Dar wanapendeza wanapotoka out, mitaani, maofisini, kwenye sherehe na hata kwenye vyumba vyao lakini wamezoea kuzungukwa na uchafu na hawaoni kutopatana kwa hivyo viwili? NI kweli uchafu ni sehemu ya maisha yetu au ndio utamaduni wenyewe tunaouenzi na kuudumisha?

  This is what transpired earlier today:

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Ilani ya Chama ya uchanguzi 2010-15 ndiyo inaagiza hivyo?
   
 3. e

  emiliana hyera Member

  #3
  May 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni fursa pekee kuexpress matatizo yetu live tena kwa umazi pia nasi tubadilike jamani cuz changes start by u first before the other do to you, mbona tunatupa taka kwenye mitaro ni serikali jamani? au kuachia vyoo mvua ikinyesha NI SERIKALI?
   
 4. TingTing

  TingTing Member

  #4
  May 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ni kwa kuwa wanapuuzia huo upupu au kuachilia mbali kitu ambacho si sahihi kwani uchafu huwa unaletaga mlipuko wa magonjwa mbali mbali. Wakati umewadia wa vijana kuzinduka na kuchukua hatua katika kila nyanja kwa manufaa ya Taifa, manufaa yao wenyewe na vizazi vyao vijavyo.
   
 5. TingTing

  TingTing Member

  #5
  May 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii imenikumbusha leo Kiongozi Dalai Lama akiwa anatoa hotuba yake kwa wahitimu wa University of Washington na kuwaeleza kuwa mabadiliko uanzia kwa mtu binafsi kabla ya kwenda kwa wengine. Akasema, "vizingiti viko, vipingamizi vipo lakini mtu hutakiwi kupoteza matumaini".

  Kila mwananchi anapaswa kufahamu kuwa mabadiliko siyo serikali bali ni sisi raia ambao ndio tunapitia matatizo mbali mbali kutokana na maamuzi yasiyojali raia wake. Tusiteteee vyama, tunatakiwa tuangalie ni mwakilishi gani atatufanyia nini na iwapo hatofanya chochote basi huyo hafai kurudi mjengoni tena.

  Je, kuna kiongozi ambaye anaweza kujivunia kuna kitu amewaachia wananchi wake au wakazi wa jimbo analowakilisha!
   
 6. W

  WildCard JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Vipi nafasi ya CEO wa DAWASCO iliyotangazwa miezi kadhaa iliyopita?
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa kama hakuna Sehemu Rasmi tutupe wapi
   
 8. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Sana sana atasababisha kero ya foleni Dar!
   
 9. w

  wasp JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana jipya baada ya kukwaruzana na TUCTA na baadaye kugundua kwamba amechemka anataka kusafisha njia kwa wafanyakazi wa DSM. Mtafutieni safari ya kwenda Washington Merikani.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  May 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  HIvi kuna uwezekano kuwa hajui kuwa kuna matatizo ya maji machafu na usimamizi wa maji machafu jijini Dar?
   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  DAWASCO wengi ni FIBUCA. Wao walienda MnaziMmoja badala ya Uwanja wa Taifa kuungana na TUCTA. JK anawatembelea kuwashukuru pia!
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  May 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Una maana ya Majitaka? Kama una maana hiyo ni kweli tatizo ni kubwa kwa sababu waliounganishwa kwenye mfumo rasmi wa majitaka hawafiki hata 2% ya wakazi wote wa Dar.
   
 13. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kikwete alizaliwa Bagamoyo na kukulia kwenye mazingira ya kawaida akishuhudia matatizo na shida zote zinazowakabili Watanzania. Cha kufurahisha ni kuwa hata wakati wa kampeni yake ya Urais haikumwia vigumu kutafuta maneno mazuri ya kuwavuta wapiga kura "...MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA..." Kwa kutambua hali halisi ya maisha ya Mtanzania alijua kibwagizo hicho kitambeba pasipo pingamizi. Jambo la kusikitisha sana ni kuwa baada ya kuingia Ikulu amesahau kila kitu na kila tatizo linalowakabili Wananchi anakuwa akilalama kama vile ni mgeni na muda wote anataka maelezo ya kwa nini hali iko hivyo, Kikwete alitudanganya Watanzania wote.
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbona hii haiihitaji hata Kutembelea jamani, Mbona inafahamika kwamba Dar haina Mfumo Mzuri wa Maji taka? Ladba haamini kama hili tatizo lipo kwa hiyo anataka kuthibishiwa na Wananji
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Kwa maana ya kwenye red tusimlaumu kwani hawezi kutofautisha shida na raha kutokana na kukulia kwenye shida - hivyo hawezi kupigania raha; je safari hii tuchague kiongozi aliyekulia kwenye raha ili alete raha kwa watanzania wote?
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  May 24, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  .
  Siyo hajui kuhusu matatizo ya maji, bali anajua sio tuu maji safi/taka ni tatizo dar, ni kero!.
  Lengo la ziara ni kuonyesha anajali kero za wananchi, hii ni part and parcel ya campaign trail, ili akifika hiyo mikutano ya hadhara, kila kitu atareffer Ilani ya Chama cha Mapinduzi, iliahidi nini, nini wamwetekweleza na nini bado, kile ambacho bado, atasisitiza tutakamilisha awamu ijayo.

  Hichi ndicho yeye na mawaziri wake wote, na Makatibu Wakuu wanachokwenda kufanya wiki hizi mbili zilizobaki kabla ya bunge la Bajeti, Juni 8. Mtashuhudia magazeti yakipambwa na spreads za matangazo ya 'Utekelezaji wa sera za CCM kwa Wizara fulani...
  Kutangulia ni kutangulia tuu, just imagine walivyojipanga strategically kushinda, nyinyi na CCJ yenu hata usajili bado, bado mtaingia vitani bila level playing field ukitegemea kushinda?.

  Kuna siku niliwahi kuandika humu, " If you can't beat them, join them and fight from within"!.
   
 17. MANI

  MANI Platinum Member

  #17
  May 24, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ziara yake italeta mabadiliko yoyote kwani shida hizi zipo zaidi ya miaka ishirini na hata wakati anaingia ikulu zilikuwepo sasa muda wa kutoka umefika ndio anajua kuwa hilo lipo. Ni usanii na kampeni kabla ya wakati.
   
 18. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Mimi sijaelewa namna atakavyokagua, je ni kuangalia miondombinu? Majitaka kwa maana mifereji ya barabarani, kwa maana Kimara hakuna mfumo wa maji taka kutoka majumbani. Je, atapita katika baadhi ya nyumba na kufungulia mabomba ya maji safi yaliyowekwa na Wachina? Kwa kuangalia kama maji yanatoka, DAWASCO watafungulia maji eneo hilo leo na kuishia kudanganywa tena! Kama ni kusikiliza wananchi, huko ni kupoteza muda na kuishia kudanganywa tena kwani watapandikiza wazungumzaji! Pia apite na kwenye DAWASCO kiosks kulinganisha na maji yanayotoka kwenye mabomba ya Wachina.

  Nasikia magari yote ya kuuza maji ni mradi wa wafanyakazi wa DAWASCO!!!
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mhh kama ni kweli hii ni kali kabisa . Kwani tatizo la maji limeanza jana.???? Au Tatizo la maji imekuwa kama ajali ya treni au basi imetokea ghafla?

  lets assume JK au wahusika wao kule masaki, mikocheni na nk hawajui ukubwa au udogo wa tatizo la maji .je hawana ndugu, jamaa na marafiki wakuwaambia matatizo ya maji wanayopata wakaza si tu wa dar hata wa mwanza kwenye ziwa victoria au wa kigoma kwenye ziwa Tanganyika.

  Sidhani kama wanachi bado tutakubali danganywa toto za kuarijika na ziara wa wazito amabo hawafanyi maamuzi kwenye madesk yao kuondoa hizo kero.

  Badala ya kutembelea kuangalia kero ya maji aite wataalamu wapendekeze solution . zaidi ya hapo atakuwa anafanya politics zaidi badla ya kufanya implimentation

  Serikali inakumbatia sera za kuweka visima vya maji mjini tena alikuja P didy kufungua kisima mwananyamala . Ni kukosa mwelekeo. Tungeeelewa kiais kama kisima Pdidy angekifungua Mtwara au Dodoma.

  Je tukianza kuwa na sera za kuwa na visima dar tena mjini hapo tunaelekea wapi.
   
 20. a

  akilipana Member

  #20
  May 24, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wamlete huku kwetu mbagala na asindikizwe na msanii diamond akimwimbia, "kwetu mbagalaaa..."
   
Loading...