chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,383
- 24,939
Habari wakuu.
Kuna taarifa kwamba Mhe Rais mstaafu Jakaya Kikwete kesho atapanda Mlima Kilimanjaro kwa mara ya kwanza kabisa toka awe Rais wa Tanzania.
Hizi ni habari njema japo inashangaza kidogo imekuwaje kwa kipindi chote hicho cha miaka kumi akiwa madarakani hakufanya jambo hili la Kizalendo ambalo huenda lingeongeza hamasa kwa watalii wa nje na ndani kuutembelea mlima huo mrefu kuliko yote Afrika.
Natoa pongezi kwa Mh Jk lakini vilevile viongozi wawe na Utamaduni wa kuvienzi vya nyumbani. Safari za Ughaibuni Jk hakukosa hata moja ila hapo Kilimanjaro alipasahau kabisa.
Namtakia kila la kheri kwa utalii huu wa ndani hapo kesho.
Wasalaam...