Tetesi: Kikwete Kuongezewa Muda wa Utawala

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,731
21,133
Mwenyekiti wa NLD, Dk Makaidi alisema zipo dalili na ushahidi kuwa uchaguzi ukifanyika mwaka huu CCM itang'olewa madarakani na kwa kulijua hilo, Serikali inafanya kila njia ili kuahirisha uchaguzi usifanyike mwaka huu.

"Kubadili Katiba ya sasa kwa lengo la kuahirisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu sio tu kutaathiri misingi muhimu ya Katiba ya sasa, bali pia kutaathiri amani ya nchi yetu. Tumeona kinachoendelea Burundi baada ya Rais Pierre Nkurunzinza na chama chake kuamua kujiongezea muda wa kutawala nchi hiyo," alisema.

"Tumeona yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Conga (DRC) baada ya Joseph Kabila kutaka kufanya hivyo, Kikwete na wana-CCM wenzake wasitake kuiingiza nchi yetu katika majanga yasiyokuwa na sababu," alisema.

Chanzo: MCL
 
Lakini kama muda unaongezwa kidogo kama miaka miwili au mitatu hivi ili kukamilisha ahadi zake na kuweka mambo ya nchi sawa sioni tatizo
 
Umesoma vizuri paragraph ya pili na kutafakali kidogo?

Lakini kama muda unaongezwa kidogo kama miaka miwili au mitatu hivi ili kukamilisha ahadi zake na kuweka mambo ya nchi sawa sioni tatizo
 
Unajua ni swala la watu kuamua na kukubaliana tu jamani. Kwa mfano ikigundulika ahadi walizotoa hazijakamilika na muda ndo huu unayoyoma. Sasa wakiomba tuwasubiri kidogo wakamikishe ahadi zao kuna ubaya gani? Nchi si ipo tu? Hata kama kama wakipewa miaka mitatu ili wafanye final touches kuna shida?
 
Kuruhusu huyu bwana kuendelea hata siku moja baada ya muda wake ni kukaribisha machafuko kwani mafisadi ndio watakuwa wanamalizia lala salama ya kutuibia!!
 
Lakini kama muda unaongezwa kidogo kama miaka miwili au mitatu hivi ili kukamilisha ahadi zake na kuweka mambo ya nchi sawa sioni tatizo

Hakujua na usomi wake wa BA Economics na honorary doctorate kuwa ahadi alizokuwa anatoa hazitekelezeki ndani ya kipindi chake kikatiba.
 
Unajua ni swala la watu kuamua na kukubaliana tu jamani. Kwa mfano ikigundulika ahadi walizotoa hazijakamilika na muda ndo huu unayoyoma. Sasa wakiomba tuwasubiri kidogo wakamikishe ahadi zao kuna ubaya gani? Nchi si ipo tu? Hata kama kama wakipewa miaka mitatu ili wafanye final touches kuna shida?

Kwani waliopita walitimiza ahadi zao zote? Nyerere mwenyewe hakuweza kutimiza yote...na hiyo miaka mitatu ikiisha hajakamilisha utamuongeza mingapi tena
 
Huyu jamaa ni shemeji yake Nkurunzinza na yuko sympathetic kwa wale magaidi wa FDLR na pia inasemekana ana uhusiano wa kibiashara na Joseph Kabila. Wote hapo wanafanana sitashangaa Kikwete akitaka kujiongezea muda
 
Hii thread ukiwauliza Kikwete arudi? Watakuambia Ndiyo. MAGUFULI KIBOKO YAO.
 
Mwenyekiti wa NLD, Dk Makaidi alisema zipo dalili na ushahidi kuwa uchaguzi ukifanyika mwaka huu CCM itang'olewa madarakani na kwa kulijua hilo, Serikali inafanya kila njia ili kuahirisha uchaguzi usifanyike mwaka huu.
"Kubadili Katiba ya sasa kwa lengo la kuahirisha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu sio tu kutaathiri misingi muhimu ya Katiba ya sasa, bali pia kutaathiri amani ya nchi yetu. Tumeona kinachoendelea Burundi baada ya Rais Pierre Nkurunzinza na chama chake kuamua kujiongezea muda wa kutawala nchi hiyo," alisema.
"Tumeona yanayoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Conga (DRC) baada ya Joseph Kabila kutaka kufanya hivyo, Kikwete na wana-CCM wenzake wasitake kuiingiza nchi yetu katika majanga yasiyokuwa na sababu," alisema.
Chanzo: MCL
Kama itatokea Jpm akaongezewa miaka miwili au mitatu haitakuwa mbaya sana
 
Back
Top Bottom