Kikwete kumpisha Magufuli mapema

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
DSC00468.jpg

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete, sasa anatajwa kuwa tayari kumwachia chama hicho Rais, Dk. John Magufuli, kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake, Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Uamuzi huo unatafsiriwa kuwa ni mkakati wa kuimarisha ufanisi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli, na inatarajiwa kwamba hatua hiyo ya Kikwete itakuwa mapema kabla ya uchaguzi wa CCM miaka miwili ijayo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, kitendawili cha Kikwete kung’atuka mapema uenyekiti kinaweza kuwekwa bayana Februari 5, 2016 ambapo CCM kitakuwa kikitimiza miaka 39 tangu kuzaliwa kwake Februari 5, mwaka 1977.

Taarifa hizo za uhakika zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu vya uhakika vya habari baada ya gazeti hili wiki iliyopita kufichua namna baadhi ya wafanyabiashara wasio waadilifu walivyopanga kutumia ‘kichaka’ cha chama kuzima kasi ya Magufuli serikalini, zinaweka bayana kwamba, Kikwete anaunga mkono kwa dhati kazi inayofanywa na Dk. Magufuli ambaye alimpachika jina la Tingatinga.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alisema Kikwete amekuwa na uhakika wa kasi ya Magufuli tangu kampeni zianze mwishoni mwa Agosti mwaka huu na hatimaye upigaji kura Oktoba 25.

Mjumbe huyo alilieleza gazeti hili; “…ili kumpa nguvu zaidi ya kutumbua majipu, Mwenyekiti yupo tayari kumpisha Magufuli kwenye uenyekiti wa chama mapema zaidi ili nguvu zake azielekeze pia katika kukisafisha na kukiimarisha chama.”

Akizungumza na wana CCM kwenye ofisi ndogo ya makao makuu ya chama Lumumba, jijini Dar es Salaam, Oktoba 30, 2015, baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu, Magufuli aliweka bayana hisia zake juu ya namna anavyochukizwa na kile alichokiita unafiki ndani ya CCM.

Gazeti hili katika toleo lake lililopita namba 437, lilieleza namna baadhi ya wafanyabiashara kwa kushirikiana na sehemu ya viongozi waandamizi wa CCM, walivyoanza kutengeneza mkakati wa kumdhoofisha Magufuli, kupitia chama chake.

Katika mkakati huo baadhi ya vigogo wa chama wenye mafungamano ya karibu na wafanyabiashara hasa wanaoshiriki biashara zenye utata na kukwepa kodi, wamepanga kuhakikisha Magufuli hapewi uenyekiti wa chama hicho mapema kama ilivyo mazoea ya chama hicho, badala yake wanataka abaki kuwa Rais hadi mwaka 2017 chama hicho kitakapofanya uchaguzi.

Habari hiyo ilieleza zaidi kwamba, mtazamo wa vigogo hao ni kwamba mpaka muda huo chama chini ya Mwenyekiti wake wa sasa, Rais (mstaafu) Jakaya Kikwete, wanaweza kuwa na namna ya kudhibiti kasi ya Magufuli ambayo inaelezwa kuwagusa vibaya wanaoaminika kuwa walikuwa wafadhili wa chama hicho.

Habari hiyo iliendelea kufafanua ya kuwa wengi wa wafanyabiashara na vigogo hao ambao walikuwa ni wananufaika katika biashara zao kupitia ufadhili wa kuchangia chama na kuwa karibu na viongozi ili ‘kufanya mambo yao yaende vizuri’ wanaelezwa kuanza ushawishi kwa Mwenyekiti Kikwete, aendelee na uenyekiti mpaka ufike wakati wa uchaguzi rasmi kwa mujibu wa kalenda ya chama.

Raia mwema
 
Wastaarabu wako ccm, hakuna kin'gan'ganizi wa Madaraka kama kile chama cha akina nanhii
 
Vasco atakuwa kashinikizwa aondoke mapema madudu mengi aliyoshindwa kuyakabili chini ya utawala wake ndio sababu ya kukimbia kivuli chake.
 
Ni vyema amwachie mapema maana kuna mambo wakienda kwenye chama anakosa uhuru kwa vile mwenyekiti ni Mtangulizi wake.
 
Ukawa wafurahia magufuli kuwa mwenyekiti wa ccm,

hawa jamaa utashaangaa keesho yake tu wanarudi kulia lia humu jf
 
Back
Top Bottom