Elections 2010 Kikwete kufanya mdahalo Ijumaa, aweza kutangaza hali ya hatari Jumapili?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Hakuna ulazima wowote wa Rais Kikwete kufanya "mdahalo hewa" baada ya kura kupigwa na kujijenga kama bado ni Rais wakati wananchi wanasubiri matokeo ya Uchaguzi. Ninawashauri kina kinana kama lengo la "mdahalo hewa" wa Rais Kikwete kuwavutia wapiga kura waufanye wakati wa kampeni yaani (hadi Jumamosi). Watanzania wana haki ya kumsikiliza Kikwete ili awasaidie kufanya uamuzi wa kupiga kura.

Kitendo cha kupanga kufanya "mdahalo hewa" siku ya Jumapili, wakati kura zinasubiliwa na matokeo hayajatoka ni kitendo chenye lengo la kuandaa mazingira ya vitisho na hata kutangaza hali ya hatari hasa kama exit polls zinaonesha CCM kufanya vibaya.

Matokeo yake Rais Kikwete atatumia nguvu ya EPACT ya 1986 ambapo vyombo vyote vya habari vinaweza kupigwa marufuku kutangaza na radio zote kuanza kuimba nyimbo wanazozitaka na hivyo kuchakachua utaratibu wa kutangaza matokeo.

Kwa kufanya mazungumzo hayo usiku wa kuhesabu kura na kabla ya matokeo yote kutoka CCM inawataka wananchi wajikusanye kuandamana au kufanya vurugu ili hatimaye waweze kufungulia virungu dhidi yao.
Tutumie hekima basi tunapopanga baadhi ya mambo. Kwa vile uchaguzi utakuwa umeshapita sidhani kama kuna ulazima wa Kikwete kuzungumza usiku wa kuhesabu kura.

Kama atashinda basi atazungumza na wananchi siku ya kuapishwa. Is that too much to ask?
 
Mwanakijiji unaona mbali. nakupongeza
ila siku hizi umeanza kuwabembeleza hawa wakoloni?
unaongea kama una mawazo mazito mkulu.
kunani??????????
 
Nimekusoma Mzee. Mungu ailinde Tanzania. tunapita kipindi kigumu. ni sawa na mama yuko labour ward.
 
Hiyo habari mbona haieleweki.yaani atafanya mdahalo baada ya wananchi kutoa maamuzi ili isaidie nini.Nani kakupa hizo habari?tuhabarishe tusio nataarifa
 
Nilikuwa na mawazo haya haya mungu tusaidie lakini MM mawimbi ya tsunami yaja wewe subiri Dr Slaa amalize kuhutubia Dar ndio utanielewa kama unayakumbuka mapinduzi ya Iran miaka ile au India serikali pamoja na dola zake waliua wananchi na kuwaumiza but mwisho wa siku askari wakakimbia na kuacha silaha zao. Mmungu tusaidie
 
JK unataka kufia madarakani..hahaaa jumba bovu linakuangukia sasa
 
Hili jambo limekaaje?

Jumapaili anahutubia kama nanI?

Ni mkutano wa mwisho wa mwezi?

Kama ni kampeni ... kapeni zitakuwa zimeshamaliziaka.... someone help ...it is all very confusing!!
 
Nadhani ni hotuba ya mwisho wa mwezi au ya kuaga maana anajua wazi kwamba hata akipita atadumu muda mchache sana kutokana na afya yake.
 
Mwanakijiji... for the first time in my very short life on this earth I am preparing my family for a kenyan experience

aTangaze, asitangaze, kuzuia people's power haiwezekani, tumeona kila sehemu duniani... my personal experience ni sri lanka

kila tone la damu lina laana yake duniani

But I am still hoping intelligence itamsaidia kufanya busara, na kama atashinda kihalali, basi tukubali matokeo
 
habari nilizo nazo toka vyanzo vya uhakika ni kuwa, baada ya dr wa ukweli mh. slaa kumwaga nondo za uhakika leo jioni. kikwete anajindaa kujibu mapigo kwenye mdahalo utakaorushwa hewani 29th october. ccm wamejaa kiwewe na hawana jinsi kwa kuwa dr wa kweli mwenye phd ya darasani amewatoa kamasi.

tuone yatakayojiri, kwa kuwa hawana jinsi tai iko shingoni
 
Kikwete anajiahangaisha..kampa Dr slaa nguvu zote hizi kwa kushindwa kuwaburuza mahakamani Rostam ..Kagoda, ELowasa Ricmond... Ben Mkapa..EPA...etc..

Angewatosa ..Dr Slaa asingekuwa maarufu milele...Leo anajibu mapigo gani kama sio upuuzi tu!

leo hii ufisadi unalitafuna taifa kidini, kikabila, kikanda, kielimu, ki....etc Ni mjinga tu..atakaye msikiliza Kikwete
 
Kikwete anajiahangaisha..kampa Dr slaa nguvu zote hizi kwa kushindwa kuwaburuza mahakamani Rostam ..Kagoda, ELowasa Ricmond... Ben Mkapa..EPA...etc..

Angewatosa ..Dr Slaa asingekuwa maarufu milele...Leo anajibu mapigo gani kama sio upuuzi tu!

leo hii ufisadi unalitafuna taifa kidini, kikabila, kikanda, kielimu, ki....etc Ni mjinga tu..atakaye msikiliza Kikwete
hainiingii akilini kwenye benchi la kikwete kuna rostam, mramba, membe, chenge (spika mpya), lowassa, nchimbi, january na babake, shamte, dibibi, miraji, riziwani, salma, zungu, sophi simba, meghji, chiligati
 
wako ikulu wanahangaika sana, wameshapiga simu, kila kona waehakikishiwa kuwa mdahalo umepokewa vema kila mahali, maeneo ya moshi vijijiini hasa katika bar ya kariwa kati, saed kubenea alishuhudia live shughuli zote zikifungwa tangu saa 12 kushuhudia mdahalo, vijana walihama nyumbani hadi vijiweni kama vile wanaangalia mpira wa yanga na simba, huko likuyu namtumbo, watu wengi wasiyo na televisheni walisheheni kwenye vibaa vya pombe kama vile wanaangalia mpira
 
Kikwete anajiahangaisha..kampa Dr slaa nguvu zote hizi kwa kushindwa kuwaburuza mahakamani Rostam ..Kagoda, ELowasa Ricmond... Ben Mkapa..EPA...etc..

Angewatosa ..Dr Slaa asingekuwa maarufu milele...Leo anajibu mapigo gani kama sio upuuzi tu!

leo hii ufisadi unalitafuna taifa kidini, kikabila, kikanda, kielimu, ki....etc Ni mjinga tu..atakaye msikiliza Kikwete

Hayo ndo mambo ya kusubiri 'desa" sasa mwishoni!!!!!! haya bwana watanzania amueni manake unasubiri watu wote wazungumze na wafanye midahalo kupata pointi za kutoa mwishoni!!!! Anyway wananchi ndo waamuzi!!!!
 
tuliokua wilaya ya temeke hapakua na premier league wala nini... kila kitu kilikua ITV nadhani wamepata audience ambayo ni record breaker
 
Oparation nyingi kubwa tunatumia ganzi ya muda mrefu, ila hii ya tarehe 29 hakuna haja ya ganzi, tunapasua jipu la CCM bila ganzi tena halijaiva. Tuna ma Dr. wa ukweli sio feki
 
Back
Top Bottom