Kikwete kuchangisha graduates wa UDSM bilion 17. Je, watakubali kuchanga?

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
RAIS Jakaya Kikwete ameandaa chakula cha jioni kwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), pamoja na wadau wengine wa elimu kuchangisha shilingi bil. 17 kwa ajili ya mradi wa kujenga kituo cha wanafunzi chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza UDSM, na rais wa wahitimu wote chuoni hapo, Jaji Joseph Warioba, alisema kituo hicho kina lengo la kupunguza tatizo la uhaba wa majengo.

Aliongeza kuwa chakula hicho ni harakati za kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.
Warioba alisema UDSM imepata mafanikio mengi lakini inakabiliwa na uchakavu wa majengo, upungufu wa majengo ya kufundishia na maeneo ya kupumzikia.
"Idadi ya wanafunzi imeongozeka sana, ingawa wengi wao hawakai hapa wanakaa nje ya chuo. Majengo hayatoshi na mengine yamezeeka, wakati mwingine mwanafunzi ana kipindi asubuhi na jioni anakosa mahali pa kupumzikia kwa sababu anaishi nje ya chuo," alisema Warioba.

Maswali yangu ni machache tu;
1: kama hawa ndoo lile kundi linalokosa mikopo , je hizo pesa za kuchanga watazitoa wapi???
2: Kama wajibu wa serikali ni kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya chuo kikuu kama cha UDSM inakarabatiwa ila hakuna kinachofanyika na pesa za walipa kodi zinawekwa mifukoni kwa manufaa yao na kuja tena kuwachangisha hawa walala hoi wanafunzi ili wajenge wenyewe je nini kazi ya hii serikali ya JK na kodi za watanzania zinaenda wapi?????

3: Je nikisema huu mchakato wa kutaka kuchangisha hizi pesa bilion 17 ni kwa manufaa ya BMW (Baba Mama na Watoto) kwa ajili ya huyu JK nitakuwa nimekosea????
 
Au ndoo mbinu za kumuongezea Ridhiwan Mtaji wa kuongeza shehena za semi za mafuta ndani ya mgodi wa Geita maana Ridhiwani yeye ana Tenda ya Kusupply mafuta ndani ya mgodi wa GEITA na mama Salima ana tenda ya kampuni ya kufanya usafi na kuwapikia wafanyakazi wa Geita ,,, na kuna tenda pia wanataka kuzichukua ndani ya migodi minne ya Barrick(Buzwagi, Bulyanhuru, North Mara na Tulawaka) ya aina hiyohiyo,, inawezekana ni kuwaongezea mtaji!!!!!!!!!!
 
Hebu jaribu kusoma kwa makini ulichokiandika, halafu usome na maswali yako. Hata ulichoandika haukijui.
 
Watu wengine kwa kutumia masaburi kufikiri bana!kwanza wanaochangishwa ni wahitimu waliowahi kusoma udsm,akiwemo warioba mwnyw na,zito,mnyika, mdee,kikwete,nk.pili wewe nani amekwambia kuwa wananchi hawapaswi kuchangia maendeleo ya nch yao na nani amekwambia ni serikali peke yake ndo inatakiwa kuwaletea watu maendeleo.utakufa maskini na mawazo yako mgando wewe.ndo nyie ukiona baba yako ana kanyumba na kagari bas we ndo umefika hata kaz hufanyi unakuwa kula kulala...badilika we masaburi.!
 
Nitachangia nikiwa kama mwana UDSM....mleta maada yakupasa kutambua ni wa2 wengi wenye nafasi mbalimbali ambao wamesoma UDSM,so wakati umefika nasi kukisaidia chuo.
 
Mimi ningependa kuchangia bila kungojea hiyo free lunch. Ila ningependa kuona Lwekaza Mukandala anapumzishwa kwanza
 
Tayari wengine tumeshangia..jamani tukumbuke hiki chuo ndicho kilichotufanya tuwe hapa tulipo.
Kikwete ni Symbolic representation tu, wanaohusika na ukusanyaji wa hizo hela ni UDSM wenyewe.
Mimi tayari nimeshanunua tiketi yangu ya Dinner na JK hiyo Jumanne! Jamani wana alumnai wote shirikini kwenye hii dinner, Tiketi ni laki 2 tu
 
kumbe nawewe umesoma udsm!emu tukumbushe umemaliza mwaka gani?jaman na sie tulosoma pale UCC ka cheti ka computer tunaingia ktk hyo sijui udsm convocation alumnai?
 
Nimesoma miaka ya zamani kidogo..nadhani kabla ya UCC kuanzishwa.
As long as ulisoma UDSM kwa ngazi yoyote ile u are in.
 
Hivi Mods, ni lazima kila member aanzishe thread humu JF?... Nyingine kwakweli zinaishushia JF standing yake in public. Huu ni mfano.
 
we unataka viwekwe v2 gan? Au kwa kuwa haujasoma Udsm ndo macho yanakutoka? Anzisha na wewe ya chuo chako
 
Hivi Mods, ni lazima kila member aanzishe thread humu JF?... Nyingine kwakweli zinaishushia JF standing yake in public. Huu ni mfano.

hiyo taarifa ya kuchangisha ni nzuri tu ila maswali aliyouliza mtoa mada hayaendani na taarifa husika nimeomba mods ayatoe maswali hayo.
JK ameitwa tu kama mmoja ya waliosoma hapo, pesa inachangwa na uongozi wa chuo
 
RAIS Jakaya Kikwete ameandaa chakula cha jioni kwa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), pamoja na wadau wengine wa elimu kuchangisha shilingi bil. 17 kwa ajili ya mradi wa kujenga kituo cha wanafunzi chuoni hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza UDSM, na rais wa wahitimu wote chuoni hapo, Jaji Joseph Warioba, alisema kituo hicho kina lengo la kupunguza tatizo la uhaba wa majengo.

Aliongeza kuwa chakula hicho ni harakati za kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.
Warioba alisema UDSM imepata mafanikio mengi lakini inakabiliwa na uchakavu wa majengo, upungufu wa majengo ya kufundishia na maeneo ya kupumzikia.
“Idadi ya wanafunzi imeongozeka sana, ingawa wengi wao hawakai hapa wanakaa nje ya chuo. Majengo hayatoshi na mengine yamezeeka, wakati mwingine mwanafunzi ana kipindi asubuhi na jioni anakosa mahali pa kupumzikia kwa sababu anaishi nje ya chuo,” alisema Warioba.

Maswali yangu ni machache tu;
1: kama hawa ndoo lile kundi linalokosa mikopo , je hizo pesa za kuchanga watazitoa wapi???
2: Kama wajibu wa serikali ni kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya chuo kikuu kama cha UDSM inakarabatiwa ila hakuna kinachofanyika na pesa za walipa kodi zinawekwa mifukoni kwa manufaa yao na kuja tena kuwachangisha hawa walala hoi wanafunzi ili wajenge wenyewe je nini kazi ya hii serikali ya JK na kodi za watanzania zinaenda wapi?????

3: Je nikisema huu mchakato wa kutaka kuchangisha hizi pesa bilion 17 ni kwa manufaa ya BMW (Baba Mama na Watoto) kwa ajili ya huyu JK nitakuwa nimekosea????

Hapo mwisho hujakosea kabisa.
 
Nadhani wanaochangishwa ni wahitimu wa chuo ambao wana mafanikio katika jamii.
Ni aibu kwa rais wa nchi kuwapigia magoti matajiri! Nadhani mafisadi sasa wanajipanga kumuweka sawa! Hivi huyu mtu ana mpango gani katika kusimamia marekebisho ya sera mbovu za madini na maliasili nyingine? Nchi imejaa utajiri wa kila aina na mabilioni ya shilingi yanakwapuliwa na wawekezaji kila kukicha, halafu anatuletea mambo ya kitchen party hapa! Hivi ana mang'amuzi kweli huyu!
 
Siamini kama kuna watu humu wanjiiita 'wana-jf' halafu hawako tayari kuona UDSM inaboreshwa angalau kimiundombinu.Pana tabu pale jamani
 
Tayari wengine tumeshangia..jamani tukumbuke hiki chuo ndicho kilichotufanya tuwe hapa tulipo.
Kikwete ni Symbolic representation tu, wanaohusika na ukusanyaji wa hizo hela ni UDSM wenyewe.
Mimi tayari nimeshanunua tiketi yangu ya Dinner na JK hiyo Jumanne! Jamani wana alumnai wote shirikini kwenye hii dinner, Tiketi ni laki 2 tu
inaelekea ulikuwa una-cram madesa kwelii. maana hata alumnae imekuwa alumnai...
 
Back
Top Bottom