Kikwete Kubali Yaishe Kama Jerry Rowlings wa Ghana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Kubali Yaishe Kama Jerry Rowlings wa Ghana

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Oct 31, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Kikwete. Mkapa. Mwinyi and Sons.

  Muna haki sawa ya kuitwa Watanzania kama hao munaowaita majuha na makokoto. Kwa hiyo sote sisi na ninyi ni Majuha na Makokoto kwa kuwa sote ni Watanzania.

  Sasa basi, Bwana JK sioni nafasi ya wewe kushinda uchaguzi huu.

  Mimi ni mtoto wa kijijini. Nimechunga ng'ombe mimi. Nimekula maziwa fresh yasiyochujwa wala kuchemshwa mimi.Nimeishi maisha ya kunyeshewa mvua bila mwavuli nikalowa chakachaka. Nimelima kwa jembe la mkono mimi. Watu wa mikoa ifuatayo wanaishi maisha ya aina hiyo. Safari hii hawana mzaha. Hawaogopi kuitwa kokoto tena. Hawaogopi kiutwa majuha.

  Shinyanga, Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Manyara, Musoma.

  UTASHINDWA VIBAYA KATIKA MIKOA HII.

  Mikoa mingine utakayoshindwa vibaya: Kilimanjaro, Arusha.

  Jana mlitumia muda wa masaa matatu kuwaita makokoto, lakini kumbuka Mkwere: Wazazi wetu wametumia miaka mitano ya utawala wako kutoa maamuzi ya kukumwaga.

  Sorry to say it was too late to change their minds.

  Subiri matokeo.

  Utashindwa, na tunaomba uiache nchi yetu kwa amani kama alivyofanya Jerrry Rowlings kwa John Kufour.
   
 2. c

  chanai JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa akubali tu kwa moyo mkunjufu na ataendelea kuheshimika katika nchi hii. Vinginevyo........................
   
 3. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ataendelea na ubishi wake lakini safari hii lazima achapwe kiboko..
   
Loading...