MWANALUGALI
JF-Expert Member
- Feb 1, 2010
- 601
- 34
Uundwaji wa baraza la Mawaziri uliofanywa na Kikwete hivi karibuni kumedhihirisha kuwa Rais Kikwete amejitanabahisha kuwa ktk kundi la Wapiganaji dhidi ya Mafisadi kwa kwaacha nje ya Baraza lake wale watuhumiwa wakubwa wa ufisadi na badala yake akawajumuisha wapiganaji kama Samuel Sitta na Dr H.Mwakyembe.
Hivi kweli Kikwete ana ubavu wa kumtosa moja kwa moja rafiki yake wa kweli ambaye hawakukutana barabarani? Hivi ana msimamo thabiti wa kukataa matakwa ya Rostam kwenye Serikali yake? Ngoja tusubiri tuone kama hatafanya mabadiliko muda si muda ili kuwaingiza marafiki zake Mafisadi ambao kwa sasa wameachwa.
Kitendo cha kutowagusa Mahanga Makongoro na Sofia Simba ni ishara ya kulinda connection au ni matokeo ya bahati tu? Hivi Makongoro atakaa amwangalie SIx usoni wakikutana kwenye baraza?