Kikwete kawaokoa Wabunge wa CCM?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Ilikuwa Zitto afungiwe vikao viwili vya Bunge na hiyo ingemleta hadi kikao cha kwanza cha mwakani. Pamoja na hayo ufafanuzi uliotelewa na Spika mara baada ya kufungiwa ilitajwa kuwa Zitto kafungungiwa kushiriki vikao vya Bunge na Kamati. Unless niwe nimekosea, leo tunaambiwa kufungukiwa kwake kunakoma in three weeks.. what happened? ja JK inawezekana ameamua kupunguza makala ya hasira za wananchi kwa kumrudisha mwakilishi wao Bungeni kabla ya muda wa adhabu kuisha?
 
kikwete aweze kuwa kang'amua kuwa upinzani unashika chati kwa jambo lililokuwa dogo, ambalo kwa kufukuzwa kwake kumewapa sauti kubwa wapinzani kiasi cha kuwa wafadhili wameanza kupiga kelele na utawala wa kikwete.

hii yote ni katika jitihada za kurudisha imani ya utawala wake kwa wafadhili
 
Ilikuwa Zitto afungiwe vikao viwili vya Bunge na hiyo ingemleta hadi kikao cha kwanza cha mwakani. Pamoja na hayo ufafanuzi uliotelewa na Spika mara baada ya kufungiwa ilitajwa kuwa Zitto kafungungiwa kushiriki vikao vya Bunge na Kamati. Unless niwe nimekosea, leo tunaambiwa kufungukiwa kwake kunakoma in three weeks.. what happened? ja JK inawezekana ameamua kupunguza makala ya hasira za wananchi kwa kumrudisha mwakilishi wao Bungeni kabla ya muda wa adhabu kuisha?

Mkuu Mwanakijiji, i stand corrected if i'm wrong, lakini hii statement kwamba adhabu ya Zitto imekuwa ya wiki tatu si inamaanisha kwamba hataudhuria vikao vyote vya bunge linalokaa hivi sasa, ambalo muda wa vikao hivyo ni wiki tatu, then linaahirishwa mpaka Januari mwakani. So in essence, hiyo adhabu ya Zitto bado ime-stand vilevile kwamba hatahudhuria vikao vya bunge mpaka Bunge litakapokutana January-2008.
 
hapana, baada ya kikao cha kawaida cha Bunge Novemba 16, kesho yake anaweza kuingia kwenye vikao vya kamati.. (adhabu inaisha novemba 16)
 
hapana, baada ya kikao cha kawaida cha Bunge Novemba 16, kesho yake anaweza kuingia kwenye vikao vya kamati.. (adhabu inaisha novemba 16)

Mzee Mwanakijiji usipotoshe watu!!! Spika ameweka wazi,,, mambo ya mpaka Bunge la January sijui Feb, ilikuja tu kama tafsiri ya watu kwamba kama hatakuwa bungeni kipindi hiki then the next kikao ni hicho cha January sijui Feb. watu walitafsri vikao...na sio adhabu kamili...hili ni tatizo letu wabongo na waandishi wetu...

Ndio hao hao walisema mpaka Zitto apewe barua...

Lakini kwa mtizamo mpana, baada ya kifungo cha kikao hiki, ataendelea na shughuli zake... hivyo atahudhuria kamati,,, na mshahara atapata mzima,,, na kama kutakuwa na kikao cha Bunge cha Dharura atahudhuria pia...

Hakuna kilichobadilika jamani,,, punguzeni kuongozwa na mioyo yenu, tangulizeni kuongozwa na akili zaidi....
 
angalia kauli yangu ya kwanza.. kama watu walielewa hivyo miye basi ni mmojawapo, kwanini huwezi kusahihisha kitu hadi iwe mtu anapotosha? Nimesema "unless niwe nimekosea"... Naomba usome adhabu aliyoomba Mudhihir ilikuwa ni ipi?
 
Hapa naona tunachanganyana,basi mwenye kuweza kuelezea mwanzo adhabu ilikuwaje na sasa nini kimebadilika nafikiriri tutaweza kuelewa vizuri badala ya kuchanganya mambo na kufanya hata wanaosoma hapa wataona kama ni kijiwe cha udaku.
 
angalia kauli yangu ya kwanza.. kama watu walielewa hivyo miye basi ni mmojawapo, kwanini huwezi kusahihisha kitu hadi iwe mtu anapotosha? Nimesema "unless niwe nimekosea"... Naomba usome adhabu aliyoomba Mudhihir ilikuwa ni ipi?

Unakumbuka Zitto alitolewa kwenye kikao kilichokua kinaendelea + kikao hiki cha October/November,,, aljebra inasema?
 
Kumaliza mjadala huu, mwanakijiji hebu tupe kilichosemwa na spika ile siku ya adhabu inatolewa,maana umeanzisha hoja kwa kutanguliza defence statement
 
Mzee Mwanakijiji usipotoshe watu!!! Spika ameweka wazi,,, mambo ya mpaka Bunge la January sijui Feb, ilikuja tu kama tafsiri ya watu kwamba kama hatakuwa bungeni kipindi hiki then the next kikao ni hicho cha January sijui Feb. watu walitafsri vikao...na sio adhabu kamili...hili ni tatizo letu wabongo na waandishi wetu...

Ndio hao hao walisema mpaka Zitto apewe barua...

Lakini kwa mtizamo mpana, baada ya kifungo cha kikao hiki, ataendelea na shughuli zake... hivyo atahudhuria kamati,,, na mshahara atapata mzima,,, na kama kutakuwa na kikao cha Bunge cha Dharura atahudhuria pia...

Hakuna kilichobadilika jamani,,, punguzeni kuongozwa na mioyo yenu, tangulizeni kuongozwa na akili zaidi....

Mzee Mwanakijiji watu washaathiriwa na kauli za serikali, ooh! anapotosha, mara Uzushi, mara ana lengo la kuchonganisha nk.

Kwa taarifa yenu, mdhihiri alitaka mpaka iwe january ndo adhabu yake iishe, la pili hivyo vikao viwili vimekaa lini? Nikihesabu tangu afungiwe hiki ni kikao cha kwanza kukaa akiwa nje, au walihesabu na kile kilichomfungia?

Kuhusiana na barua, aliwahi kuulizwa kwa nini Zitto hajapewa barua, akasema ni uzembe wa sekretarieti yake akijitetea kuwa siyo yeye anayepaswa kuandika hiyo barua; cha kushangaza sasa anaibuka akisema barua siyo lazima. Wakati anatoa jibu baada ya kuulizwa na waandishi alikuwa hajui hilo? Au watu wa sekretarieti ndo walimweleza utaratibu? Ikiimaanisha alikuwa haujui utaratibu?

Juzi nimeshangaa alivyoibuka na Kanuni za Bunge akisahau majibu aliyotoa kwa waandishi!
Huenda nao hawazisomi vizuri hizo kanuni, wanazima moto!
 
Hume, wanafikiri hatujui taratibu za Bunge. Mudhihir alipotoa hoja ya Zitto kufungiwa alitakiwa apendekeze na adhabu. Sasa Adhabu aliyopendekeza ni ipi, na kwa vile hoja yake iliungwa mkono ina maana na adhabu ilikubalika. Sasa leo wanageuka kinyume nyume nini?
 
Kwa taarifa yenu, mdhihiri alitaka mpaka iwe january ndo adhabu yake iishe, la pili hivyo vikao viwili vimekaa lini? Nikihesabu tangu afungiwe hiki ni kikao cha kwanza kukaa akiwa nje, au walihesabu na kile kilichomfungia?

Ni uelewa mdogo tu, bado kama hakutakuwa na Kikao Cha Bunge cha Dharura, Mh. Zitto ataanza kuhudhuria kikao cha January... huelewi nini hapa!!!

Spika hajabadilisha kitu chochote,,, ameongeza maelezo ya ziada muelewe tu, kwamba adhabu rasmi inaishia vikao viwili, ambacho cha mwisho ni hiki hapa... lakini kikao rasmi cha bunge atakachokuwepo ni Januari.

Haki zake zitaanza kulipwa full kuanzia mwisho wa kikao cha pili,, ambacho ni hiki kinachoendelea...

maana nadhani mnataka kusema mmeweka pressure spika akabadilisha kitu hakuna... ni uelewa wenu ulio na pazia la....

Hivi mlianza kuacha hesabu tangu darasa la kwanza au chekechea?
 
Hume, wanafikiri hatujui taratibu za Bunge. Mudhihir alipotoa hoja ya Zitto kufungiwa alitakiwa apendekeze na adhabu. Sasa Adhabu aliyopendekeza ni ipi, na kwa vile hoja yake iliungwa mkono ina maana na adhabu ilikubalika. Sasa leo wanageuka kinyume nyume nini?

nikuulize kitu ?

kabla hujanipa ruhusa bana mie sina muda hapa, nauliza tu are you after zitto au wananchi wa tanzani ? everywhere, zitto, zitto, zitto, zitto ! karamagi je ?
LOL
 
Adhabu ya Zitto mwisho Nov 17

2007-10-31 09:50:05
Na Beatrice Bandawe, Dodoma

Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta, amesema adhabu ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, inaisha Novemba 16, mwaka huu na hivyo kuanzia Novemba 17 anaruhusiwa kushiriki katika shughuli zote za kibunge kama kawaida.

Hata hivyo, Novemba 17 ndio mwisho wa kikao cha Bunge kilichoanza jana.

Bw. Sitta, alisema hayo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya adhabu ya mbunge huyo.

Bw. Sitta, alisema mbunge huyo amekuwa akinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari kuwa amepewa adhabu hiyo bila kupewa barua kitendo kinachomfanya ashindwe kuelewa mipaka ya adhabu yake.

Bw. Kabwe, alipewa adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi Januari mwakani, kwa madai ya kutoa kauli ya uongo Bungeni dhidi ya Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi, inayohusu kusaini mkataba na Kampuni ya Barrick, juu ya Mradi wa Buzwagi, jijini London nchini Uingereza.

Akitoa ufafanuzi huo, Bw. Sitta alisema, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Na. 61 Mbunge aliyesimamishwa kazi kwa mujibu wa Kanuni ya 59(3) au ya 60(2) atatoka katika Bunge na hataingia tena katika sehemu yoyote ya Ukumbi wa Mikutano ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa, na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zozote zinazoambatana na mshahara huo.

``Bunge halikuona sababu ya kumuandikia barua kwa sababu Kanuni zinajieleza wazi,`` alisema Bw. Sitta na kuongeza kuwa ni vizuri wabunge wakazitii kanuni zote badala ya kupotosha umma.

Hata hivyo, alisema kuwa kipindi cha adhabu cha Bw. Zitto kinaisha Novemba 16, na kwamba Novemba 17 anaweza kushiriki katika shughuli zote za Bunge zikiwemo kuhudhuria Kamati za Bunge.

Alisema kwa kuwa adhabu hiyo inaisha baada ya Kikao cha Mkutano wa tisa na baada ya hapo kutakuwa hakuna kikao kingine mpaka Januari, hivyo mbunge huyo atarejea tena ndani ya Ukumbi wa Bunge, Januari mwakani.
Wakati Bw. Zitto anasimamishwa na maelezo yakatolewa kwamba atarejea bungeni humo Januari, ilieleweka pia kwamba hatohudhuria shughuli nyingine za bunge hadi muda huo.

Wakati huo huo, Bw. Sitta, aliwafahamisha wabunge kuwa jana alikuwa amevaa joho jipya lililofumwa na nyuzi za dhahabu.

``Kwa wale ambao hawajagundua, Spika leo amevalia joho jipya. Lile la zamani lilikuwa limechakaa,`` alisema Spika.

Alisema vazi hilo ambalo huchakaa baada ya miaka 12 hadi 15, limeshonwa na mafundi maalum mjini London, nchini Uingereza.

Nadhani inaeleweka
 
Back
Top Bottom