Kikwete: Katiba mpya isiegemee udini, ukabila au kulenga kuvunja muungano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=3][/h]

kikwete.jpg

Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonya kuwa mchakato wa kuandika Katiba Mpya usifanywe kwa kuegemea udini, ukabila, ubinafsi, siasa ama kulenga kuvunja Muungano.

Rais Kikwete amesema hayo baada ya kuwaapisha wajumbe wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, Ikulu, Dar es Salaam hapo Jana na kuwahutubu wajumbe wa tume hiyo akiwaambia, Tanzania hakuna udini wala ukabila, hivyo wajumbe wa Tume ya Katiba mnatakiwa kuongozwa na maoni ya wananchi siyo ya makundi mnayotoka, hatutaki ipatikane Katiba itakayoegemea udini, ukabila, siasa wala kulenga kuvunja Muungano, katiba ni ya Watanzania wote.

Tume hiyo itaanza kazi yake ya miezi 18, Mei mosi mwaka huu, kwa kukusanya maoni ya wananchi na kutengeneza rasimu ya katiba, baadaye zikifuata hatua mbili muhimu ambazo ni kuundwa kwa Bunge Maalumu la kuchambua rasimu hiyo, kisha wananchi kupiga kura ya maoni.
 
Muungano sio kitu chakulazimishana Mh JK ikiwa upande moja utakuwa na sababu na kusema hawataki basi hio ndio Democracy, kwanza ujulikane kuwa Muungano huu haukuwachirikicha wananchi a.b. umeuwa utaifa wa Tanganyika na Katiba yake ambaye alikuwa ni mchirika mkuu wa Muungano.
 
kama ni hivyo si angeiandika wenyewe tu. au anafikiri kuwa rais ndio katuzidi kwa akili na maarifa, Huwezi kumshangaa mwanaasha!
 
Ni kwanini viongozi kutoka Tanganyika wanakuwa ving'ang'anizi wa muungano wakati wazanzibar hawataki muungano?

Wakati umefika kujadiliana maana sisi watanganyika inaonekana kama tunanufaika sana na huo muungano,acha wazanzibar waondoke na zanzibar yao na Tanganyika tubaki na tanganyika yetu.Kujadili muundo wa muungano ni lazima siyo ombi
 
tunajua Jk hutaki kuingia kwenye historia kama wewe ni rais aliyeasisi kuvunja muungano, lakini wewe ni wewe na sisi wenye nchi tuko milioni 48 na wengi wetu hatuupendi muungano au sehemu kubwa ya huu muungano na hili lazima lijadiliwe kama halijadiliwi tutakuja kuuvunja huu muungano wenu kwa nguvu sababu hamna kitu chenye nguvu duniani kama wazo zuri lililofikia wakati wake, hamna wa kuzuia hili.
 
Abdulsahaf, wewe nafikiri ni mzenji, Hilo kwanza.

Pili posti yako imekaa kinafikinafiki kidogo, unamwonyesha Rais JK akiwa amevaa kuashiria Rais Mwislamu wa Tanzania.

Tatu picha na ujumbe ulioandika haviendani, yaani Rais anayepinga udini ndo mwenyewe mdini, kwa jinsi alivovaa.

Nne kudhihirisha kuwa posti yako ni ya kinafiki, umeshindilia kwa maoni yako mwenyewe kupinga muungano.

Tumewazoea wazenji, mnakuja Kama mnvyokwenda.
 
Mh.Rais Jk Kikwete amekemea udini nchini Tanzania,Hayo ameyasema katika siku ya mtoto wa Afrika ambapo pia amesisitiza kwamba watoto wana haki ya kulindwa na kuthaminiwa ikiwa ni pamoja na kupewa haki zao.
 
Ni jambo la faraja kama rais amekemea tatizo la udini. Lakini shida kubwa ninayoona ni kwamba wananchi wengi hawana uhakika na kauli ya rais ni ya kweli toka rohoni kwake na kwamba anachosema ndicho anachofanya nje ya uso wa vyombo vya habari.

Kama tunataka kunusuru balaa linalotunyemelea basi iko haja ya kuwa na 'definition' mpya kuhusu serikali kutokuwa na dini. Lazima tuwekane sawa nini maana ya serikali kutokuwa na dini katika context ya Tanzania.

Na kwa maoni yangu maoni yangu nishauri bunge lipitishe sheria inayozuia mwanasiasa kushiriki kwenye mambo ya dini. Kama mwanasiasa atahudhuria ibada au hafla ya dini basi afanye hivyo kama muumini wa kawaida kabisa, lakini iwe mwiko mwanasiasa kutoa hotuba kwenye mikusanyiko ya dini (msikitini/kanisani/temple) hata kusalimia iwe marufuku. Asali na aende zake. Hakuna mambo ya Harambee, haya ndio yanaleta balaa kama ukabila na siasa Kenya. Kwani huko nyuma makanisa yalikuwa yanapataje michango? Tufumbe macho ni kutenganisha kwa vitendo siasa na dini.
 
nafurahi kusikia kikwete nae anaweza kukumea...
apunguze kucheka cheka bwana kipindi anapokua anakemea
 
Na kwa maoni yangu maoni yangu nishauri bunge lipitishe sheria inayozuia mwanasiasa kushiriki kwenye mambo ya dini. Kama mwanasiasa atahudhuria ibada au hafla ya dini basi afanye hivyo kama muumini wa kawaida kabisa, lakini iwe mwiko mwanasiasa kutoa hotuba kwenye mikusanyiko ya dini (msikitini/kanisani/temple) hata kusalimia iwe marufuku. Asali na aende zake. Hakuna mambo ya Harambee, haya ndio yanaleta balaa kama ukabila na siasa Kenya. Kwani huko nyuma makanisa yalikuwa yanapataje michango? Tufumbe macho ni kutenganisha kwa vitendo siasa na dini.
Kwa staili hii utawa isolate "wadini"! walio katika siasa wataikimbia siasa, ambao hawajajiingiza katika siasa wataikwepa, matokeo yake unakuwa na Serikali iliyo upande wake na wananchi "wadini" upande wao!
Kwa nini kusiwe na utawala wa majimbo ya kidini?
 
Wacheza disco ndio wadini wakubwa! Wanatamani nchi yote ijae kumbi za disco tu! Wanaosababisha hadi sasa hali kuwa tete ni vigazeti na viradio mbao vilivyojaa makanjanja, hawa wataiangamiza nchi siku sinyingi.

Tumeshuhudia yalotokea Zanzibar ukweli unajulikana CCM ndio waliochoma makanisa ili ishu ya kutaka muungano uvunjike ife na ishu igeuke kuwa ya kidini na mwisho habari ya muungano ikiguswa ionekane ni udini. Jiulize kwanini hadi sasa haiundwi tumehuru kuchunguza ishu hii? Ishu inajulikana ndio maana makanjanja wanang'ang'ania vitu visivyopo ili kudivert mind za mazuzu wasiojua kinachoendelea.

Mmesahau janjaweed ilivyofanya uharibifu Zanzibar? Ndio hao walotumika kuchoma makanisa Zanzibar,Waislam na Uamsho ni kisingizio tu ili kuhalalisha dhulma.
 
huo mkutano aliozungumza wa mtoto wa afrika umejaa usanii mtupu na tatizo kubwa kinara wa uandaaji bwana Abubakar Fransis Kabwogi ni tapeli mkubwa wa kimataifa JK kaingia mkenge tenda kwenda kufungua mkutano magumashi
 
Mh.Rais Jk Kikwete amekemea udini nchini Tanzania,Hayo ameyasema katika siku ya mtoto wa Afrika ambapo pia amesisitiza kwamba watoto wana haki ya kulindwa na kuthaminiwa ikiwa ni pamoja na kupewa haki zao.

udini aliuanzisha kikwete na ccm yake, halafu kuhu watoto je atafuta kauli yake ya wamba wtoto wanaopewa mimba ni viherehere leo anazungumzia kuwa linda wakati wanao wabaka watoto wanalipwa m 10...
 
Wacheza disco ndio wadini wakubwa! Wanatamani nchi yote ijae kumbi za disco tu! Wanaosababisha hadi sasa hali kuwa tete ni vigazeti na viradio mbao vilivyojaa makanjanja, hawa wataiangamiza nchi siku sinyingi.

Tumeshuhudia yalotokea Zanzibar ukweli unajulikana CCM ndio waliochoma makanisa ili ishu ya kutaka muungano uvunjike ife na ishu igeuke kuwa ya kidini na mwisho habari ya muungano ikiguswa ionekane ni udini. Jiulize kwanini hadi sasa haiundwi tumehuru kuchunguza ishu hii? Ishu inajulikana ndio maana makanjanja wanang'ang'ania vitu visivyopo ili kudivert mind za mazuzu wasiojua kinachoendelea.

Mmesahau janjaweed ilivyofanya uharibifu Zanzibar? Ndio hao walotumika kuchoma makanisa Zanzibar,Waislam na Uamsho ni kisingizio tu ili kuhalalisha dhulma.

ipandisheni ccm mahakamani kwa kusabibisha nyie mmeonekana magaidi na wachoma makanisa.

Sidhani kama una ushahidi wa kuitia nyinyiemu hatiani, lakin umma wote unajua makanisa yalichomwa na taasisi ya kiislam uamsho.
 
Ni jambo la faraja kama rais amekemea tatizo la udini. Lakini shida kubwa ninayoona ni kwamba wananchi wengi hawana uhakika na kauli ya rais ni ya kweli toka rohoni kwake na kwamba anachosema ndicho anachofanya nje ya uso wa vyombo vya habari.

Kama tunataka kunusuru balaa linalotunyemelea basi iko haja ya kuwa na 'definition' mpya kuhusu serikali kutokuwa na dini. Lazima tuwekane sawa nini maana ya serikali kutokuwa na dini katika context ya Tanzania.

Na kwa maoni yangu maoni yangu nishauri bunge lipitishe sheria inayozuia mwanasiasa kushiriki kwenye mambo ya dini. Kama mwanasiasa atahudhuria ibada au hafla ya dini basi afanye hivyo kama muumini wa kawaida kabisa, lakini iwe mwiko mwanasiasa kutoa hotuba kwenye mikusanyiko ya dini (msikitini/kanisani/temple) hata kusalimia iwe marufuku. Asali na aende zake. Hakuna mambo ya Harambee, haya ndio yanaleta balaa kama ukabila na siasa Kenya. Kwani huko nyuma makanisa yalikuwa yanapataje michango? Tufumbe macho ni kutenganisha kwa vitendo siasa na dini.

Mkuu maoni yako mazuri sana, ila kwa heshima na taadhima nakuomba unipe definition kwa uelewa wako nini "UDINI"?
 
Kwa staili hii utawa isolate "wadini"! walio katika siasa wataikimbia siasa, ambao hawajajiingiza katika siasa wataikwepa, matokeo yake unakuwa na Serikali iliyo upande wake na wananchi "wadini" upande wao!
Kwa nini kusiwe na utawala wa majimbo ya kidini?

Sideeq, naongelea utawala na siasa vs. dini na siasa. Based on what I am seeing now, kuna haja kabisa ya kutenganisha siasa na dini. Mtu achague moja, dini au siasa. Na tumipige marufuku kutumia wanasiasa kuhutubia au kuongoza shughuli yoyote ile ya kidini. Ukabila unakuwa mgumu, wanasiasa wametumia lakini wameona ni shida kutumia makabila kwa manufaa ya kisiasa, lakini dini wameona mwanga. Sasa tufunge huu mlango kabla hatufikwa na balaa.
 
ametoa tamko kuhusu azimio la bakwata kukataa sensa?
kama hajakemea nampa big up kwani atakuwa ameona ajenda yao haina maana.
silence is the answer.
 
Back
Top Bottom