Kikwete kapotea na kufutika haraka machoni mwa Watanzania ndani ya siku 2. Kuna somo hapa

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,949
4,633
Magufuli anafanya kazi kwa mujibu wa taratibu wala hakwenda kujilinganisha na jk acha viongozi wetu wachape kazi.
 
Nyota ya kikwete itaendelea kuwaka miongoni mwa watanzania na duniani kote wacha kejeli kiongozi wa watu tunampenda sana jk pamoja na magufuli wetu.
 
Hv kweli huu ni uzi wakuweka hapa I think the drama will never end kwa style hii
 
Hakuna masika yasiyokuwa na mbu. Subiri kidogo utaanza kumtamani JK. Tatizo lako ni kuwa kale kakofia na t shirt bado ni new. Siku vikianza kuchakaa utakana kauli zako. Acha Magufuli afanye ya size yake. Tunataka kuona akitimiza ahadi zake.
 
Maisha bora kwa Mtz vs Hapa kazi TU. Tifuaneni sasa uzi wenu huu
 
Nyota ya kikwete itaendelea kuwaka miongoni mwa watanzania na duniani kote wacha kejeli kiongozi wa watu tunampenda sana jk pamoja na magufuli wetu.
Nyota unaiona mwenyewe,

Kikwete aliitumia ikulu kama ofisi binafsi ya kulipa fadhila kwa marafiki zake ndio maana aliendelea kugawa vyeo hadi dakika za mwisho.
 
... Labda tuseme ni mapema mno kutoa tathmini ya viongozi hawa wawili, tutakuwa hatuwatendei haki..
 
Nyota ya kikwete itaendelea kuwaka miongoni mwa watanzania na duniani kote wacha kejeli kiongozi wa watu tunampenda sana jk pamoja na magufuli wetu.

ni kweli kikwete ataendelea kukumbukwa na akina masogange na wale mawazir waliogawana raslimali zetu na escrow
 
ni kweli wakina wema sepetu na diamond hawatamsahau maana ikulu ilikuwa kama choo cha stand, hongera magufuri viongozi wote tunataka tutibiwe nao muhimbili atakaye kwenda India au ulaya ajilipie mwenyewe
 
Uko serious kabisa!?? Hujui utendaji wa Magufuli.

siyo sahihi kulinganisha utendaji katika nafasi ya uwaziri na katika nafasi ya urais .tunamjua vizuri sana JPM katika nafasi ya uwaziri..sasa tunampima kwenye urais, au wewe unataka tu-conclude tu
 
Back
Top Bottom