Kikwete kama kweli ushindi wako haukuwaletea faraja mafisadi, mkamate Manji

Bavicha hawatetei wezi mkuu tatizo watu hawafungui fikra zao kutafakari Mambo cjui kwa nn?Manji ni kweli anayo makosa mengi na hakuna anayemtetea kwa makosa hayo kushiriki kuiibia nchi.

Tatizo ni mbinu zinazotumika kupambana na wezi wa nchi kuna watu kuna upendeleo wa hali ya juu.Unakumbuka mwanzo Manji alipewa kesi ya madawa.Pili akakamatwa na Mihuri na sare za jeshi kiuhalisia Manji alikuwa ni mzabuni wa jeshi alikuwa anasambaza sare za jeshi cha kujiuliza hiyo tenda alijipa mwenyewe sio kweli tenda alipewa na viongozi wa jeshi iwaje Leo ababe mzigo peke take?,Pesa bank alisaini yy ndio zikatoka kuna vitu kama umesoma huwezi kudanganywa kiulahisi.

Yote Tisa mtu Bashite kabadili hadi plate number za gari kachukua gari binafsi kaweka plate number ya serikali je hii ni sahihi.Kama tusipopinga uonevu kwa jilani yako kesho utaonewa ww au mwanao.

Ukiamua kupambana na wahalifu basi roho ya uonevu iondoe usibague huyu ni mwanachama mzuri na huyu hatabiliki uanachama wake.Kinachooneka ni unafiki.

Sent using Iphone 7+
UKUKU kazini

JPM Baki
 
Kikwete, uliwahi kutamka kuwa katika vita dhidi ya mafisadi huna rafiki wala ndugu, huo ulikuwa wakati sakata la Kagoda lilipopamba moto hadi kuihusisha Ikulu. Nakumbuka pesa za walipa kodi ilivyotumiwa na serikali eti katika kujaribu kufichua utata ulioigubika Kagoda hadi makachero wa Tanzania wakalazimika kusafiri hadi nchi za Ulaya na Asia kwa ajili ya kuchunguza baadhi ya kampuni zilizohusishwa na Kagoda.

Cha jabu ni kuwa hivi sasa kuna kesi kortini imefunguliwa dhidi ya Kagoda na mtu anayedai kuwa ndiye alieidhamini Kagoda kuchota fedha Benki Kuu. Si hilo tu mtu huyo anaenda mbali na kudai kuwa hata wakati utata wa Kagoda unatuumiza vichwa, mtu huyo huyo kwa mara nyingine aliweza kuikopesha Kagoda kiasi kikubwa cha fedha. Huyo mtu naambiwa si mwingine bali ni mshikaji wako Yusufu Manji.

Wananchi wengi wanajua kuwa hadi leo serikali inadai haiwajui wamiliki wa Kagoda na hivyo imeshindwa kuichukulia hatua zozote. Swali langu kwako ni je, mathalan mshiriki wa Kagoda sasa kajitokeza wazi bila kificho, serikali yako inasubiri nini kumkamata mara moja ili aweze kuhojiwa zaidi. Kama serikali itakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote dhidi ya Manji, basi tutaamini zile tetesi kuwa Kagoda ndiyo CCM.

Kuchaguliwa kwa Kikwete kulileta faraja kubwa kwa mafisadi !

Mhh, si mchezo
 
Kweli njaa haina baunsa, siamini kama ni wewe kwa sasa upo bize FB,JF nk kumtakatisha Manji.
Acheni ulofa nyie watu, Wakudadavuwa hebu nioneshe sehemu hata moja mimi Mag3 nimemtakatisha Manji. Mimi natetea kuheshimu Katiba na utawala unaofuata sheria. FYI pesa za Manji ndizo zilikuwa zinainufaisha CCM pamoja na Magufuli akiwa Waziri mwandamizi ndani ya serikali hiyo ya Kikwete. Katiba ikifuatwa kikamilifu, watu kama Manji hawawezi kupona na hivyo hivyo madikteta uchwara kama Magufuli hawatapona.

Yanayompata Manji na Rugemarila sasa hivi yalitakiwa yawe yanawapata walioidhinisha uchotaji wa pesa nao ni viongozi wa serikali ya CCM. Manji na wafanya biashara wengine CCM ilikuwa inawafumbia macho kwa sababu ilikuwa inafaidika na pesa zao. Walitumika kama benki ya akiba ya CCM ikisubiri kuvuna kila walipohitaji hela. Kampeni za CCM na viongozi kama Magufuli ziliwezeshwa na pesa za akina Manji na wenzake.

Magufuli kaahidi kuwatetea na kuwalinda waliokuwa mabosi wake huku akifukuzana na vidagaa kama Manji ambao hakuna namna wangeweza kufanikiwa bila kuwezeshwa na serikali. Hivyo hivyo watuhumiwa wote ambao hawakuwa serikalini hawangeweza kufanikiwa kama si kwa tamaa ya viongozi wa serikali akiwemo dikteta uchwara Magufuli. ndio maana sisi wengine tunasubiri serikali hiyo iwakamate wote bila kujali sura zao.

Kigugumizi cha Magufuli kuwawajibisha waliokuwa viongozi waliokuwa serikalini kinasababishwa na nini? Kwa nini ukamate wapokeaji huku watoaji wakitamba mitaani na kunufaika na mali walizochuma kifisadi? Marais waliomtangulia Magufuli wengine watoto wao hadi wake zao Magufuli anazidi kuwapa madaraka, je kulikoni? Yeye mwenyewe pamoja na tuhuma lukuki kabana kama hakushiriki, je kulikoni? Acheni kujitoa akili.
 
Duh! Manji kawa kadagaa ka UFISADI kwa CHADEMA ya siku hizi?
Kwa hiyo LOWASA mliyetuwekea 2015 ndo angewakamata akina KIKWETE na akina SUMAYE - MAPAPA?
Kweli CHADEMA kuna mabadiliko!
Hahahahah

Hawa jamaa kila siku wazidi kuwa wajinga!

Walituletea Lowassa ili akawakamate mafisadi papa!

Hebu msome huyu Mag3 hapa alivyoandika'
''Kama serikali itakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote dhidi ya Manji, basi tutaamini zile tetesi kuwa Kagoda ndiyo CCM.''

Baada ya Manji kukamatwa ningependa kujua kama sasa ameamini kuwa Kagoda haikuwa CCM.

Leo Manji kwa hawa nyumbu amekuwa kidagaa wakati walikuwa kila mara wanaanzisha thread wakisema ni fisadi papa!

Huu ni unafiki wa kiwango cha Juu!
 
Duh! Manji kawa kadagaa ka UFISADI kwa CHADEMA ya siku hizi?
Kwa hiyo LOWASA mliyetuwekea 2015 ndo angewakamata akina KIKWETE na akina SUMAYE - MAPAPA?
Kweli CHADEMA kuna mabadiliko!
Nimesema huko nyuma na ninarudia, Lowassa asifanywe wimbo, akamatwe na kufikishwa mbele ya sheria, kugugumizi cha nini kumkamata? Kama ni wimbo umechuja!

Namwita Manji dagaaa kwa sababu hakuvamia Benki Kuu, huo uwezo hawezi kuwa nao, wako watu ambao waliidhinisha akabidhiwe hizo hela na hao ndio nawaita mapapa.

Mbona Magufuli anapotuhumiwa utetezi ni kuwa alikuwa anatekeleza maamuzi ya wakubwa wake? Kwenye nyumba na kivuko chakavu je hao wakubwa wamewajibishwa?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nami nathibitisha hilo Mkuu. Katika watu humu wenye misimamo isiyoyumba kama bendera fuata upepo wewe ni mmoja wao. Hongera sana kwa hilo.

Ccm wanajaribu likitoa ktk mahusiano na manji sahvi....maana wanatapatapa tu

Ova
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Similar Discussions

Back
Top Bottom