Kikwete kama kweli ushindi wako haukuwaletea faraja mafisadi, mkamate Manji

Kikwete, uliwahi kutamka kuwa katika vita dhidi ya mafisadi huna rafiki wala ndugu, huo ulikuwa wakati sakata la Kagoda lilipopamba moto hadi kuihusisha Ikulu. Nakumbuka pesa za walipa kodi ilivyotumiwa na serikali eti katika kujaribu kufichua utata ulioigubika Kagoda hadi makachero wa Tanzania wakalazimika kusafiri hadi nchi za Ulaya na Asia kwa ajili ya kuchunguza baadhi ya kampuni zilizohusishwa na Kagoda.

Cha jabu ni kuwa hivi sasa kuna kesi kortini imefunguliwa dhidi ya Kagoda na mtu anayedai kuwa ndiye alieidhamini Kagoda kuchota fedha Benki Kuu. Si hilo tu mtu huyo anaenda mbali na kudai kuwa hata wakati utata wa Kagoda unatuumiza vichwa, mtu huyo huyo kwa mara nyingine aliweza kuikopesha Kagoda kiasi kikubwa cha fedha. Huyo mtu naambiwa si mwingine bali ni mshikaji wako Yusufu Manji.

Wananchi wengi wanajua kuwa hadi leo serikali inadai haiwajui wamiliki wa Kagoda na hivyo imeshindwa kuichukulia hatua zozote. Swali langu kwako ni je, mathalan mshiriki wa Kagoda sasa kajitokeza wazi bila kificho, serikali yako inasubiri nini kumkamata mara moja ili aweze kuhojiwa zaidi. Kama serikali itakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote dhidi ya Manji, basi tutaamini zile tetesi kuwa Kagoda ndiyo CCM.

Kuchaguliwa kwa Kikwete kulileta faraja kubwa kwa mafisadi !
Sasa yametimia.Fisadi papa limegonga mwamba.Heko JPM.Mzigo mzito mbebeshe Msukuma.
 
Kikwete ni sawa na mbwa asiye na meno. Tunachotakiwa kufanya watanzania ni kuing'oa ccm 2015 then tuwakamate wote tukianzia na Kikwete mwenyewe na waliomtangulia. Wanayo mashitaka mengi ya kujibu.
Mh aya
 
BAVICHA wamepoteana, kilichobaki kutetea Barrick na Singasinga Seti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bavicha hawatetei wezi mkuu tatizo watu hawafungui fikra zao kutafakari Mambo cjui kwa nn?Manji ni kweli anayo makosa mengi na hakuna anayemtetea kwa makosa hayo kushiriki kuiibia nchi.

Tatizo ni mbinu zinazotumika kupambana na wezi wa nchi kuna watu kuna upendeleo wa hali ya juu.Unakumbuka mwanzo Manji alipewa kesi ya madawa.Pili akakamatwa na Mihuri na sare za jeshi kiuhalisia Manji alikuwa ni mzabuni wa jeshi alikuwa anasambaza sare za jeshi cha kujiuliza hiyo tenda alijipa mwenyewe sio kweli tenda alipewa na viongozi wa jeshi iwaje Leo ababe mzigo peke take?,Pesa bank alisaini yy ndio zikatoka kuna vitu kama umesoma huwezi kudanganywa kiulahisi.

Yote Tisa mtu Bashite kabadili hadi plate number za gari kachukua gari binafsi kaweka plate number ya serikali je hii ni sahihi.Kama tusipopinga uonevu kwa jilani yako kesho utaonewa ww au mwanao.

Ukiamua kupambana na wahalifu basi roho ya uonevu iondoe usibague huyu ni mwanachama mzuri na huyu hatabiliki uanachama wake.Kinachooneka ni unafiki.

Sent using Iphone 7+
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom