Kikwete kama kweli ushindi wako haukuwaletea faraja mafisadi, mkamate Manji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kama kweli ushindi wako haukuwaletea faraja mafisadi, mkamate Manji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Mar 6, 2011.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kikwete, uliwahi kutamka kuwa katika vita dhidi ya mafisadi huna rafiki wala ndugu, huo ulikuwa wakati sakata la Kagoda lilipopamba moto hadi kuihusisha Ikulu. Nakumbuka pesa za walipa kodi ilivyotumiwa na serikali eti katika kujaribu kufichua utata ulioigubika Kagoda hadi makachero wa Tanzania wakalazimika kusafiri hadi nchi za Ulaya na Asia kwa ajili ya kuchunguza baadhi ya kampuni zilizohusishwa na Kagoda.

  Cha jabu ni kuwa hivi sasa kuna kesi kortini imefunguliwa dhidi ya Kagoda na mtu anayedai kuwa ndiye alieidhamini Kagoda kuchota fedha Benki Kuu. Si hilo tu mtu huyo anaenda mbali na kudai kuwa hata wakati utata wa Kagoda unatuumiza vichwa, mtu huyo huyo kwa mara nyingine aliweza kuikopesha Kagoda kiasi kikubwa cha fedha. Huyo mtu naambiwa si mwingine bali ni mshikaji wako Yusufu Manji.

  Wananchi wengi wanajua kuwa hadi leo serikali inadai haiwajui wamiliki wa Kagoda na hivyo imeshindwa kuichukulia hatua zozote. Swali langu kwako ni je, mathalan mshiriki wa Kagoda sasa kajitokeza wazi bila kificho, serikali yako inasubiri nini kumkamata mara moja ili aweze kuhojiwa zaidi. Kama serikali itakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote dhidi ya Manji, basi tutaamini zile tetesi kuwa Kagoda ndiyo CCM.

  Kuchaguliwa kwa Kikwete kulileta faraja kubwa kwa mafisadi !
   
 2. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Embu nikumbushe kagoda inahusika na nini?
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh! hili nalo neno. Serikali ya Kikwete hiko matatani kweli maana kila anapojitahidi kuziba lile linaibuka hili jipya. Siku ya kufa Nyani basi miti yote huteleza......

  Ni kweli ndugu yangu nami nilisoma habari hiyo kwenye vyombo vya habari nikashangaa sana. Kama Manji aliwadhamini Kagoda basi anawafahamu vizuri sasa kwa nini asikamatwe na kuhojiwa walipo? Sakata hii itawatoa ofisini Afande Mwema, Hosea na Mnyika (aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali). Kamati yao iliudanganya umma na kufanya matumizi mabaya ya fedha za umma kuficha ukweli. Hii ni sakata mpya inayohitaji kuanzishwa na Makamanda wa CDM. Kikwete kwishilia mbali.... umedanganya Umma na kutumia ofisi ya umma vibaya hivyo amepoteza sifa za uongozi..... Pole sana handsome guy Kikwete!!
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mwanahalisi toleo Na. 228 - Wizi wa Kagoda
  YUSUF Manji, mfanyabiashara wa Dar es Salaam, ni miongoni mwa walionufaika na mabilioni ya shilingi ambayo yalikwapuliwa na kampuni ya kitapeli ya Kagoda Agriculture Limited kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), MwanaHALISI limegundua. Taarifa zinasema Manji, kupitia kampuni yake – Quality Finance Corporation Limited (QFCL) – ambayo anamiliki na baba yake, Mehboob Manji, "anakabwa koo na serikali" ili arudishe dola za Marekani 28 milioni (Sh. 31 bilioni) zikiwa sehemu ya fedha zote zilizoibwa na Kagoda.
  Nyaraka zilizopo zinaonyesha kuwa Manji na kampuni yake walikopa kiasi hicho cha fedha kutoka kampuni ya Kagoda chini ya mkataba wao wa tarehe 12 Septemba 2005.
  Kampuni ya Kagoda ilikwapua jumla ya dola za Kimarekani 30,732,658.82 (Sh. 40 bilioni) katika Akanuti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT. Fedha hizi na nyingine zipatazo Sh. 73 zilichotwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
  Manji anadaiwa chini ya kinachoitwa urejeshaji kiasi fulani cha madeni ya EPA kwa mpango wa Rais Jakaya Kikwete wa msamaha kwa wezi au washirika wao watakaokubali kurejesha sehemu ya fedha zilizoibwa.
  Barua ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika, Kumb. Na. JC/B.20/29/16 ya 20 Mei 2008 iliyotumwa kwa Manji, inamtaka Manji alipe fedha hizo katika kipindi alichokubaliana katika mkataba wake na serikali. Mwanyika alikuwa akijibu ombi la Manji la 28 Agosti 2008 la kutaka kusogeza mbele muda wa kurejesha mabilioni hayo kadri ya makubaliano.
  Manji alikuwa akimkumbusha Mwanyika kuwa makampuni yake yalitoa dhamana ya mali isiyohamishika na vilevile kutoa hundi nane zenye tarehe za mbele.
  "Bahati mbaya tumeshindwa kufanya malipo ambayo yalikuwa yafanywe tarehe 1 na 15 Aprili 2008 kutokana na upatikanaji kwa viwango vidogo wa fedha za kukulipa…Tunaona pia kuwa hatutaweza kukamilisha wajibu wetu hata kwa tarehe 1 Mei 2008," anaandika Manji.
  Katika barua hiyo, Manji anaomba kusogeza mbele muda wa kulipa na kwamba warejeshewe hundi zao ili waweke tarehe mpya.

  Kagoda inaeleza katika mkataba wake na Manji kuwa mkopo huo ulipaswa kulipwa katika muda wa miaka mitatu (3), kwa riba ya asilimia 11 kwa mwaka. Haijafahamika Kagoda walipata wapi mamlaka ya kukopesha fedha iliyodaiwa kukusanywa kutoka kwa wadai wa serikali wa nje ya nchi.
  Manji na baba yake Mehboob, ndio wanaonyeshwa kuwa walisaini mkataba huo kwa niaba ya QFCL, huku waliosaini kwa niaba ya Kagoda, wakitajwa kuwa ni Francis William na John Kyomuhendo ambaye tangu sakata la Kagoda ametajwa kuwa mfanyakazi wa Rostam Aziz.
  Mbali na Manji na baba yake kuwa wakurugenzi wa QFCL, ni haohao ambao pia ni wadhamini binafsi wa mkopo ili kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa.
  Taarifa zinaonyesha pia kuwa ni Yusuf Manji aliyedhamini Kagoda kufungua akaunti katika tawi la CRDB Benki la Holland jijini Dar es Salaam ambako mabilioni ya shilingi yalipitia.
  Mkataba wa makampuni hayo mawili ulisimamiwa na mwanasheria Nasir Rattansi na mkopo wenyewe ulitakiwa kuwa umemalizwa kulipwa ifikapo 28 Desemba 2008.
  Kufumuka kwa taarifa hizi za Kagoda kunaiweka serikali ya Kikwete katika mazingira magumu. Serikali imekuwa ikikana kufahamu wamiliki wa Kagoda na kwa zaidi ya miaka mitano sasa imekaa kimya juu ya wizi wa kampuni hiyo.
  Aidha, serikali imekuwa ikijikanyaga kuhusu wizi huu. Aliyekuwa waziri wa fedha, Zakia Meghji aliwaandikia maodita wa kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini akisema, fedha za Kagoda zilitumika kwa "kazi za usalama wa taifa."
  Katika barua yake ya 15 Septemba 2006, Meghji anasema, "Kama unavyofahamu vema, mamlaka ya serikali huwa na siri, vilevile haja ya kugharamia matumizi ya busara.
  "Kwa hiyo... malipo ya dola 30,732,658.82 za Marekani yaliyofanywa na BoT kwa Kagoda Agriculture Limited, yaliidhinishwa na serikali kugharamia matumizi yake nyeti na ilikuwa lazima kuchukua hatua hii ya kudumisha usiri huu."
  Hatua hii inaleta maswali mengi kuliko majibu; yakiwa ni pamoja na iwapo Manji na wakwapuaji wa Kagoda ndio hasa wanaitwa "Usalama wa taaifa."
  Hata hivyo, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, 12 Septemba 2005, siku ambayo kampuni ya Manji na baba yake wanadai kufunga mkataba wa kukopa mabilioni ya shilingi, Kagoda yenyewe ilikuwa haijasajiliwa.
  Cheti cha usajili wa Kagoda Na. 54040 kilichotolewa na ofisi ya Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara na Makampuni (BRELA), kinaonyesha Kagoda ilisajiliwa 29 Septemba 2005, siku 17 baada ya Manji kufunga mkataba na kampuni ya kitapeli.
  Watu muhimu katika siri ya Rais Kikwete kuhusu wezi wa fedha za BoT ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP), Said Mwema, Mkurugezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na Mwanyika, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Maalum ya rais ya kufuatilia walioiba benki.
  Kazi za kamati hii zimebaki siri ya watu hao wanne; hata idadi ya watu waliogundulika, walioahidi kulipa na kiasi watakacholipa imebaki siri yao.
  MwanaHALISI lina taarifa, tangu miaka mitatu iliyopita, kuwa mwenye kampuni ya Kagoda au anayejua shughuli zake ni Rostam Aziz.
  Wakili Bhyidinka Sanze wa kampuni ya mawakili ya Malegesi – Malegesi Law Chambers – ya Dar es Salaam, katika andishi rasmi kwa Kamati ya rais ya kushughulikia wizi kwenye akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), anakiri kuwa ni yeye alishuhudia "…mikataba ya Kagoda na makampuni mengine ya nje."
  Anasema alishuhudia mkataba wa Kagoda ndani ya ofisi za kampuni ya Caspian Construction Limited ambayo inamilikiwa na Rostam iliyoko Mtaa wa Milambo Na. 50 katikati ya jiji la Dar es Salaam.
  Sanze anasema, "Niliitwa na Bw. Malegesi ofisini kwa Bw. Rostam Aziz…Nilipofika…niliwakuta Bw. Rostam Aziz, Peter Noni (Mkurugenzi Mtendaji wa sasa wa benki ya raslimali) na Bw. Malegesi; wakaniambia fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kugharamia uchaguzi wa CCM na rais wake."
  Andishi la wakili linaeleza kuwa Rostan Aziz, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia Sanze kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambako rais mstaafu Benjamin Mkapa alitoa maelekezo kwa Gavana Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam kwa ajili ya uchaguzi.
  Bali taarifa zilizoenea Dar es Salaam zinasema Rostam aliamua "kumuuzia kesi Manji ili kujinusuru na kashfa ya Kagoda."
  MwanaHALISI lilipowasiliana na Manji kutaka kufahamu iwapo madai hayo ni kweli alijibu, "Hivi sasa ni vita." Hata hivyo, Manji hakufafanua vita hivyo vinalenga kuangamiza nani.
  Nyaraka zilizo mikononi mwa gazeti hili zinaonyesha risiti kadhaa za serikali zinazodaiwa na wa ndani wake kuwa ndizo zilizotolewa na serikali kuthibitisha Manji kurejesha fedha za Kagoda.
  Miongoni mwa risiti hizo ni Na. 31494282 yenye thamani ya Sh. 4.5 bilioni; 31494264 ya Sh. 4.5 bilioni na 31494283 ya Sh. 4.5 bilioni. Bali tarehe za risiti hizo zinagongana na zile ambazo Manji alielekeza katika mawasiliano yake na Mwanyika ya tarehe 28 Aprili 2008.
  Juhudi za kuthibitisha uhalali wa risiti hizo na malipo yanayodaiwa kufanyika hazikufanikiwa. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile hakupatikana kwa maelezo ya Katibu Muhtasi wake kuwa alikuwa katika mkutano akijiandaa kwenda bungeni Dodoma.
  Baada ya mwandishi kusisitiza ni lazima aonane na Likwelile kwa sababu kuna jambo la dharula, katibu huyo alisema Likwelile hawezi kuwa na muda huo.
  "Kwanza umepitia mapokezi? Huwezi tu kuja ofisini kwa mtu kwa vile wewe ni mwandishi na ukapewa nafasi ya kuzungumza naye. Ukitaka labda nikupangie miadi uje siku nyingine," alisema mwanamama huyo.
  Mwandishi aligoma kuondoka kutoka katika ofisi hiyo na ndipo katibu huyo aliposema kuwa bosi wake (Likwelile) ameagiza kama kuna maswali yapelekwe katika ofisi ya uhusiano ya wizara.
  Risiti hizo zilipelekwa kwenye ofisi ya uhusiano ambayo nayo ilizipeleka kwenye ofisi inayohusika na hundi zilizolipwa na hazina, lakini majibu hayakuweza kupatikana kwa madai kwamba jambo linalozungumziwa ni la miaka mitatu.


  Leo huyo Yusuf Manji eti ameishtaki Kagoda akidai aliidhamini kwenye huo wizi na siyo hivyo tu aliikopesha mabiloni !
   
 5. m

  mzambia JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ahsante
   
 6. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni sawa na mbwa asiye na meno. Tunachotakiwa kufanya watanzania ni kuing'oa ccm 2015 then tuwakamate wote tukianzia na Kikwete mwenyewe na waliomtangulia. Wanayo mashitaka mengi ya kujibu.
   
 7. Countrywide

  Countrywide JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2017
  Joined: Mar 2, 2015
  Messages: 2,521
  Likes Received: 1,843
  Trophy Points: 280
  leo kakamaatwa
   
 8. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2017
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  hahahaha Mkuu unafukua makaburi. Maana humu wanasema jamaa hana kosa ni visa tuu vya mwenye nyumba!
   
 9. Countrywide

  Countrywide JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2017
  Joined: Mar 2, 2015
  Messages: 2,521
  Likes Received: 1,843
  Trophy Points: 280
  msimamo wako bado upo??
   
 10. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2017
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 14,509
  Likes Received: 21,523
  Trophy Points: 280
  Safari hii Chadema wamehamia Upande wa Manji!

  Hata Rais angesema wenye Mimba Waendelee na Masomo Basi wao wangekuwa upande wa wanaopinga Wajawazito kuendelea na Masomo baada ya kujifungua!
   
 11. MoseKing

  MoseKing JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2017
  Joined: Jul 5, 2017
  Messages: 649
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 180
  Pesa pesa za Lowassa, Manji na Rostam kwanini zinawaharibu akili CHADEMA namna hii
   
 12. Boniphace Bembele Ng'wita

  Boniphace Bembele Ng'wita Verified User

  #12
  Jul 8, 2017
  Joined: Dec 25, 2013
  Messages: 2,472
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Noted
   
 13. nao

  nao JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2017
  Joined: Jul 30, 2015
  Messages: 1,352
  Likes Received: 994
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi kabisa
   
 14. baruti 1

  baruti 1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2017
  Joined: Apr 4, 2017
  Messages: 605
  Likes Received: 687
  Trophy Points: 180
  i hope unamuunga mkono magufuli now
   
 15. W

  Wakudadavuwa JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2017
  Joined: Feb 17, 2016
  Messages: 9,302
  Likes Received: 7,855
  Trophy Points: 280
  Kweli njaa haina baunsa, siamini kama ni wewe kwa sasa upo bize FB,JF nk kumtakatisha Manji.
   
 16. N

  NorthJuu JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2017
  Joined: Mar 19, 2017
  Messages: 262
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60
   
 17. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,646
  Trophy Points: 280
  Kubenea alikuwa na nondo!
   
 18. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,439
  Likes Received: 10,646
  Trophy Points: 280
  Wezi wa nchi hii ni wachache sana na Magu atawanyoosha.

  Go Ngosha Go
   
 19. McNair

  McNair Senior Member

  #19
  Jul 8, 2017
  Joined: Mar 18, 2017
  Messages: 184
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  Kumamae...kanyagi gia Mr. President umewashika pabaya
   
 20. Countrywide

  Countrywide JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2017
  Joined: Mar 2, 2015
  Messages: 2,521
  Likes Received: 1,843
  Trophy Points: 280
  muda
   
Loading...