Kikwete kajenga barabara nyingi kuliko awamu zote tatu?

labda ungesema hela zetu zimejenge barabara nyingi sana awamu hii,nafikiri watu wanashindwa kuelewa senteci kama hizi
kikwete ni msimamiaji tuu,thats all
 
Akili za huyu dada zimekaa vyp sijui' viwanda?' kikwete amejenga kiwanda kipi? Shule- hebu angalia elimu inayotolewa angalia ufaulu, tangu 2006 alivyoingia ufaulu fm 4 iliku zaidi ya 60% leo wanafunzi 51% wanafeli,shule ya msingi eti kati ya watoto 10 wanaomaliza la saba watatu hawawezi kusoma kitabu cha darasa la pili, sita kati yao hawawezi kusoma kitabu cha kiingereza cha darasa la tatu....Chuoni wanafunzi wanamaliza bila kwenda field pia hawana walimu wa kutosha.Afya kumbuka kilichotokea kwa babu Loliondo na matokeo ya ziara za wataalamu wizara wa afya wanavyofungia hospitali na zahanati...Ntarudi baadaye.

Lol! akili za huyo dada anajua muumba aliyeumba na kutuletea mauza uza ulimwenguni hapa! khaa! ama kweli akili ni nywele! na kuanzia leo nasema binadamu wote si sawa!
 
Hizo barabara alizojenga ni zipi na kilometa ngapi?Labda watasema ni barabara 313 za angani ambazo ni jumla ya safari zake nje ya nchi
 
Haya mambo ya barabara ni siasa tu na hamna cha maana basi waje kujenga na barabara yetu ya Goba na si porojo tu.
 
Tazama shule ngapi za sekondari wakati wake na awamu zote zilizopita. Tazama zahanati. Tazama vyuo vikuu. Tazama barabara. Tazama viwanda. Halafu urudi useme uyasemayo.
ni kweli faiza. Tazama reli inavyofanya kazi. Tazama bandari isiyochelewesha mizigo ya watu. Tazama meli nyingi ni mpya. Tazama migodi inavyotunufaisha watanzania. Tazama bajeti yetu ambayo kwa sasa sio tegemezi. Tazama sasa hatuna mgao wa umeme kama zamani. Tazama wananchi wenye furaha na ambao hawafuliki kwenye mikutano na maandamano ya chadema. Tazama viongoz wetu walivyo waadilifu. Sasa hakuna ufisadi kama zaman. Tazama shule zina walimu kibao hadi wengine hawana masomo ya kufundisha. Shule za kata zote ni za gorofa. Tazama uchumi umekuwa na mambo mengine kibao. Tunasonga mbele na hatua zetu zinaridhisha.
 
Kabla ya Kikwete, awamu zote chini ya 10,000Kms, miaka 6 ya Kikwete zaidi ya 10,000Kms na bado zaja.

Aseme Rais wa Awamu ya Nne ndo Rais aliye fanya safari nyingi zaidi za nje kuliko wote waliomtangulia-hapo ningemuelewa!
 
Aseme Rais wa Awamu ya Nne ndo Rais aliye fanya safari nyingi zaidi za nje kuliko wote waliomtangulia-hapo ningemuelewa!
Na hilo pia ni ukweli usiopingika, usisahau na ni Rais pia aliyepokea wageni mashuhuri wengi kuliko yoyote, na ni Rais pia anaetembelea mikoani kuliko yoyote yule. Anaposafiri nje huwa anaenda kwa shughuli maalum.
 
Lol! akili za huyo dada anajua muumba aliyeumba na kutuletea mauza uza ulimwenguni hapa! khaa! ama kweli akili ni nywele! na kuanzia leo nasema binadamu wote si sawa!
60% ya wanafunzi wangapi na 51% ya wanafunzi wangapi wa Form IV ? Ukipata jibu njoo liweke halafu tuendelee na hoja yako nyingine. Nnaapa huwezi toa jibu kwani litakusuta.
 
Kabla ya Kikwete, awamu zote chini ya 10,000Kms, miaka 6 ya Kikwete zaidi ya 10,000Kms na bado zaja.

kwa mara ya kwanza leo ngoja nikujibu.

Sio kweli kuwa JK kajenga barabara nyingi kuliko awamu zote zilizotangulia , ukweli uko hivi JK alikuta barabara zenye urefu wa kilomita 6,453 za lami zikiwa tayari , na kwa mpango wa sasa wa Magufuli ni kuwa mpaka 2015 wawe weamejenga mpaka kufikia kilomita 11,364.

sasa kuwa amejenga nyingi kuliko awamu zote linatoka wapi , hebu tajeni barabara moja mpya zaidi ya ile ya mwandiga kigoma iliyojengwa na JK na kukamilika , ninaposema mpya ni zile alizoibua yeye na sio zile za mkapa alizomwachia kwa ajili ya kufanya uzinduzi.

Unajua mpya ya Kigoma ile ya mwandiga ni km ngapi? zipo 60 KM
 
hawa mawaziri wa jk wafunge kwa kuropoka uongo.
kwanza kwa nini wizara ya ujenzi hisianzishe website ya miradi yake
ikiwemo ya barabara kuonye ilijengwa lini?
na nani kwa hela kutoka wapi?
na ghalama ya miradi hiyo?
waweke na contact namba ili mambo kuwa ya uwazi zaidi.

hapa hawata kuwa na haja ya kutulangua na taarifa za uongo bungeni.
 
hawa mawaziri wa jk wafunge kwa kuropoka uongo.kwanza kwa nini wizara ya ujenzi hisianzishe website ya miradi yakeikiwemo ya barabara kuonye ilijengwa lini?na nani kwa hela kutoka wapi?na ghalama ya miradi hiyo?waweke na contact namba ili mambo kuwa ya uwazi zaidi.hapa hawata kuwa na haja ya kutulangua na taarifa za uongo bungeni.
Mzee wa kwanza kwa nini, kila post yako ili neno lazima ulitumie, fani ya ni Askari
 
barabara nyingi za nchi hii zimejengwa na serikali ya awamu ya tatu
kuna ambazo kikwete alikuta zinaendelea kujengwa lakini pesa yake ilikuwa tayari

hao wanataka kupiga cross na kufunga wenyewe

Umesema vyema kabisa .JK amekuja anakuta kila kitu kwenye programu na yeye hana pesa za kujenga ila za kutalii Duniani .Hana muda but Mkapa ndiye apewe sifa kaacha zinajengwa na prog ilikuwa tayari so Nyalangu anajikomba tu kwa komba ili apate kamkate kake mnafiki mkubwa huyu .

hapa pia nakataa, bara bara nyingi zilijengwa enzi za nyerere, labda mseme bara bara za kiwango cha lami ni mzee mkapa, lakini pia njia nyinge muhimu za uchukuzi km reli zimekufa enzi za mkapa.

Kabla ya Kikwete, awamu zote chini ya 10,000Kms, miaka 6 ya Kikwete zaidi ya 10,000Kms na bado zaja.

hii hapo chini ni nukuu kutoka taarifa ya waziri mkuu alipotoa hitimisho bungeni
Serikali ya Awamu ya Nne imekamilisha Miradi yote 27 ya Barabara Kuu zilizoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tatu. Sasa hivi unaweza kutoka Mtwara-Dar es Salaam-Dodoma
 
Kwa hakika JK amefanikisha km 60 za barabara huko Mwandiga tangu mwaka 2005, hakuna barabara aliyoanza kuijenga yeye kama Rais, tuwe wakweli tusitake sifa za Nyani.
 
hapa pia nakataa, bara bara nyingi zilijengwa enzi za nyerere, labda mseme bara bara za kiwango cha lami ni mzee mkapa, lakini pia njia nyinge muhimu za uchukuzi km reli zimekufa enzi za mkapa.

Umesema kweli!

Lakini hapo kwenye red napingana na wewe! Mashirika mengi yamekufa enzi za mzee Ruksa hivyo Mkapa alipoyakuta yana hali mbaya akaamua kuyabinafsisha. Pia kumbuka yote hayo ni matokeo ya Azimio la Zanzibar (miaka '90s).

Kwa hiyo mzee Mkapa hakuwa na jinsi zaidi ya kuyauza hayo mashirika yaliyokuwa na hali mbaya.
 
Jana nilimsikia huyu waziri mdogo wa biashara anaitwa Nyalandu katika kipindi cha tuongee asubuhi star tv akisema kuwa awamu ya nne ambayo inaongozwa na Kikwete wamejenga barabara nyingi au niseme kilometa nyingi kuliko awamu zote tatu zilizotangulia kwa pamoja. Hivi ni kweli? Je ni barabara zipi?

Huwezi kwa miaka 4 kujenga barabara nyingi na ndefu kuliko zilizojengwa huko nyuma! Hii ni mipango ya awamu ya 3 inaendelezwa tu na awamu ya 4. Msisahau vilevile pesa nyingi zinatoka nje na watu wa nje wanayao katika kujenga barabara. kUna madini, uranium, mashamba ya kililmo na uwekezaji mwingine sasa unafikiri kama huko yaliko madini hakufikifki hao wawekezaji watafikaje. Ndio maana wazungu na wachina wametoa fedha kwa ajili ya kuweza kuweka mirija yao kisawasawa.
 
huyu mzee mwinyi ndo gurudumu lilipoanzia la kwenda mrama mpka jk senior(nyerere) alisema ikulu sio sehemu ya walanguzi..na kuhusu jk kashangia world gueness record kuwa ni rais wa kwanza kuudhuria misba na sherehe nyingi kuliko marais wote duniani na anayedhurula dunia kiasi cha kulingana na vasco da gama..

wewe ndetichia, kama ni kweli ameingia kwenye kitabu cha guiness world record, basi hilo ndio jambo kubwa alilolifanya kupita maraisi wote waliomtangulia.
 
Labda itabidi tuvae miwani yenye lens za nguvu kuweza kuziona hizo barabara. Au itabidi tuwashe kurunzi kuzitafuta ziliko. Lakini kama Naibu Waziri alimaanisha safari za kwenda nje then yuko right JK anaongoza. Je mwajua gharama ya safari moja ya JK kwenda nje? Kwa taarifa yenu si chini ya Shilingi za Tanzania Bilioni 3
 
Back
Top Bottom