Kikwete kainua uchumi wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete kainua uchumi wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zawadi Ngoda, Sep 19, 2009.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ukiziamini takwimu za CIA kupitia website yao (www.aneki.com), basi hutakuwa na ubavu wa kukipinga kichwa cha habari hapo juu. CIA ni shirika lnaloaminika sana duniani, na lipo up to date katika takwimu zao.

  Miaka miwili iliyopita nilitembelea mtandao wao na nikapata aibu, pale nilipoiona Tanzania katika bora 10 masikini duniani. Kwa wasomaji wazuri wa mtandao wa wakati ule T/Daima wanaweza kukumbuka jinsi nilivyokuwa naleta takwimu hizi kwa masikitiko. Mara leo hii upepo umegeuka na naweza kuandika kwa majigambo jinsi uchumi ulivyopanda kama ndege, mig 21. Leo hii Tanzania ipo nafasi ya 28, ikipanda toka nafasi ya 8 mwaka 2007. Ifuatayo ni orodha ya nchi 33, ikianzia Zimbawe msikini sana ikiwa na GDP $200, na ya 33 ni Chad ikiwa na GDP $1600

  Top 100 countries with the lowest GDP per capita

  Samahani; nilijaribu kuziweka hapa hizo nchi lakini hazijatokea. Hivyo tembelea www.aneki.com. Na angalia katika Top 100 countries.........kama hapo juu.


  Mwaka 2007 Tanzania ilikuwa na GDP kama Somalia leo hii, $600 (sh 780000) na tulishika nafasi ya 8. Ninafurahi kusema kuwa leo hii tuna GDP ya $1400 (sh 1820000). na kuzibwaga nchi kadhaa na kushika nafasi ya 28. Kiwango hicho cha pesa kinafanya tofauti ya sh 1040000 kwa kipindi cha miaka miwili. Kwa hesabu rahisi ukuaji wa GDP kwa kipindi cha miaka miwili ni wastani wa sh 520000 kwa mwaka.

  Ikiwa kama Kikwete atachaguliwa tena, katika uchaguzi wa 2010 na kuwa madarakani mpaka 2015, na kwa mwendo kasi huu inamaanisha kuwa GDP ya Tanzania mwaka 2015 itakuwa sh 1820000 +(520000*6)= 4940000 = $3800. Hii inamaanisha kwamba kama ilivyo leo hii, basi Tanzania itakuwa katika nafasi ya 67, sawa na Djibouti yenye kiwango hicho leo hii.

  Watanzania tutakuwa wendawazimu kama hatutaridhika na kufurahia maendeleo hayo kiuchumi. Kwa maendeleo hayo, tunaweza vile vile tukasema bye bye misaada, sasa wenyewe tutajiendesha, kama vile warusi walivyofanya mwaka 2004 kwa IMF na World Bank. Na hii ndio ndoto yangu kubwa na nafikiri ndio ndoto ya Serikali na watanzania wote kwa jumla.

  Tabasam la Kikwete lina bahati, ngekewa na linazivuta nchi zote duniani kuiona Tanzania kama Tumaini la uwekezaji. Kusema kuwa Kikwete anaweza, sio tu propaganda bali Takwimu zinajionyesha.

  Pamoja tutashinda, safari ni ndefu na uvumilivu ndio dawa.
   
  Last edited by a moderator: Sep 19, 2009
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  There are lies, damn lies, and Statistics.

  There was a man who drowned in a river with an average depth of six inches!

  Statistics are like a bikini; what they show is suggestive, but what they leave out is crucial!

  So, the economies of a couple of countries like Zimbabwe have sunk below us, and you conclude from that that JK has done well? He didn't push past them; they just sank beneath us!

  The average Tanzanian has less access to power, water and even money, now than he had when JK took over. Try telling him that JK has improved the economy! I was going to say he would beat you up, but then I remembered that he doesn't have enough energy to do that anymore! Poor bloke!
   
 3. c

  care4all Senior Member

  #3
  Sep 19, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilivyo muelewa Zawadi ni kuwa GDP ya Tanzania imepanda na ndio sababu ya Tanzania kupanda chat kwenye hiyo orodha... kama nchi nyingine ndio zingekuwa zimedidimia, ni kuwa GDP zao zingekuwa zimedidimia wakati ile ya Tanzania ingekuwa palepale (Constant).
   
 4. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  We all know that in spite of mismanagement; our rate of GDP growth has slipped only from an annual rate of 7.5% when JK took over to about 5% now. So, the GDP had no choice but to increase (since its growth rate was, and still is, in positive territory). Since our population growth rate (2.9% and decreasing, thanks to the ravages of HIV Aids and other maladies), is below the GDP growth rate, then our GDP Per Capita had no choice but to increase too!

  So, it depends on how you look at it. If you look at the fact that JK has shrunk our annual growth rate, like I do, you criticise him. On the other hand, if you are mesmerized by the fact that our GDP Per Capita has become better than those of a couple of other sickly economies, then you congratulate him (as you do).

  The GDP Per Capita Statistics that you allude to do not prove that JK is a good leader. They only prove that there are some countries that have fared worse than we have.
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Kwa ukweli mtu anayehitaji hongera ni Mkapa. Mkapa kafanya kazi kubwa sana kwenye uchumi lakini anamapungufu yake ya kuwaachia mafisadi na kusaini mikataba mibaya. Mkapa pamoja na kuchukiwa alikuwa na mipango mizuri zaidi kwa wawekezaji hata kwenye sera ya afya kuliko Kikwete. Kikwete amekuwa raisi kwa muda mfupi sana na ni wawekezaji wachache wapya wamekuja wakati wa kikwete. Kikwete lakini atasaidiwa na Pinda wawekezaji wameshajua Pinga ni mtu anayejua mambo na mfuatiliaji kuliko Kikwete sana wanamtumia pinda, Kenya wamemtumia pinda na alikuwa huko majuzi na sasa hawalalamiki tena, South Korea wametumia Pinda. Pinda ndiye mtu atakaye msaidia kikwete kwani anaonekani ni mtu serious na muda unavyoenda watu wanamuona pinda atakuwa kama Putin wa Russia.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ukweli mwingine wa kutopata wawekezaji wapya ni kuwa Mkapa alihakikisha anauza kila kitu, sasa huyo mwekezaji mpya atawekeza wapi??
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini kikwete si kwamba hajafanya kitu sema ana matatizo ktk uteuzi wa watendaji.
   
 8. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Why don't you go and get direct figures www.cia.gov; these are correct figures just released: Create Date: Sep-17-2009 08:51
  GDP (Purchasing Parirt); there are no current estimates for 2009

  GDP (purchasing power parity):
  [​IMG] $54.25 billion (2008 est.)
  country comparison to the world: 88 $50.65 billion (2007 est.)
  $47.27 billion (2006 est.)
  note: data are in 2008 US dollars
  GDP (official exchange rate):
  [​IMG] $20.72 billion (2008 est.)
  GDP - real growth rate:
  [​IMG] 7.1% (2008 est.)
  country comparison to the world: 36 7.1% (2007 est.)
  6.7% (2006 est.)
  GDP - per capita (PPP):
  [​IMG] $1,300 (2008 est.)
  country comparison to the world: 204 $1,300 (2007 est.)
  $1,200 (2006 est.)
  note: data are in 2008 US dollars
  GDP - composition by sector:
  [​IMG] agriculture: 27.1%
  industry: 22.5%
  services: 50.4% (2008 est.)
   
 9. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Habari yako ina chumvi na sukari. Ni kweli kama Mkapa aliwaita wawekekezaji, huku nchi ikiambulia 3% kwanini dunia nzima isije Tanzania. Maana hakuna nchi watakayokwenda na kupata faida kama Tanzania. Wawekezaji kama hao hatuwahitaji, na hawana faida kwa Mtanzania. Ndio maana Kikwete alipoingia madarakani, kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kweda kwa wawekezaji na kujadiliana nao upya ili kurekebisha mikataba.

  Kama wadhani Pinda ni mzuri, basi i kwa vile alichaguliwa na Kikwete. Na kiongozi mzuri ni yule anayeweza kuchagua timu nzuri ya kushirikiana nae kikazi. Fikiria kama angemkazania Lowasa mpaka leo kama Mkapa alivyomkumbatia Sumaye katika uongozi wake wote, licha ya kulalamikiwa mara kadhaa.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkisema JK ndo kaudidimiza uchumi wa TZ nitawaelewa lakini mnaposema kainua uchumi wa TZ nashindwa kuwaelewa ndo tuseme mnajikomba kwake ili angalau mpate kaupendeleo flani au? Maana ukiangalia bei za vitu zipo juu kulinganisha na kipato cha mtu wa kawaida Tanzania vile vile JK ameongeza gap baina ya walio nacho na ambao hawana kitu yaani maskini matajiri kipindi hiki cha miaka 4 ndo wamepaa maradufu na maskini wameshuka balaa ngoja tuone miaka mingine hiyo mtakayo mchagua.

  Huyu kashindwa kabisa kudhibiti mfumuko wa bei atajitetea ooh mdororo wa uchumi ndo umesababisha acheni kututania jamani mdororo wa uchumi nyi watanzania mnauza nini nje mpaka mkakubwa na mdororo? Zaidi ya Pamba napo inauzwa kwa kusua sua ni nn kingine mnauza nje? Ambacho TZ mnajivunia kuwa kinatuingizia kipato na fedha za kigeni. Nafikiri mnasifika kwa kutembeza bakuri kwa hisani badala ya kukomalia KILIMO ambacho ndo uti wa mgongo.
   
 11. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kwanini unogopa kukubali kuwa GDP ya TANZANIA IMEKUA? N a kama huamini takwimu za CIA, basi tupe kile chanzo unachokiamini. Kwa sababu hatuwezi kuishi bila takwimu kama tupo makini. Ni lazima tujue juzi tulikuwa wapi, jana, leo na ndipo tutaweza kupanga mipango ya kesho. Sasa tuambie mwenzetu unapotaka kujua uchumi wa nchi kama unapanda au kushuka unaangalia wapi?

  HIV/AIDS inakula sana uchumi wa Taifa kuliko hilo punguo la watu.
  1) Mgonjwa ambaye huugua zaidi ya miaka mitano anakosa nguvu na morali ya kufanya kazi.
  2. Ndugu na jamaa huacha kazi kwa ajili ya kumuuguza mgonjwa.
  3. Gharama kubwa kwa serikali katika kutoa elimu, matangazo, madawa na wataalam.

  Kupungua kwa Annual growth rate kumetokana na azma ya Kikwete kushirikisha wananchi wa kawaida katika uchumi. Kitu ambacho mimi ninamuunga mkono, kwani Mkapa hakukifanya na hata kudharau kabisa kile tuitacho uti wa mgongo wa Uchumi "Kilimo". Kumbuka: Muundo wowote wa uchumi usiowashirikisha wananchi, utafeli.

  Hatuwezi kujenga uchumi kama India. India ni moja kati ya nchi ambazo zinatafsiriwa kama Tajiri na masikini kwa wakati mmoja. Kwa sababu uchumi wa nchi umeshikwa na 20% ya wananchi, na wengine wamesahauliwa kabisa. Ninaposema kusahauliwa, ninamaanisha kuwa hawapo kabisa katika program ya taifa hata kwa siku zijazo. Hivyo japo India inaviwanda vikubwa (TATA, Vifaru, computa, matrekta n.k) lakini huwezi kuamini kuwa 60% ya wananchi wake wanaishi kwa kipato cha chini ya $1 kwa siku. China na India zina idadi ya watu karibu sawa, lakini tofauti ya nchi hizo ni mipango kwa wananchi wao. Wakati China ina mpango kwa wanachi wake (Elimu, afya, kilimo, malazi n.k), India haiwekezi hata senti tano kwenye hayo maeneo.

  Ukifanya hivyo kama India, annual growth rate itakua. Mahesabu hapo ni madogo, chukulia unafamilia ya watoto 5 sawa na kaka yako. Wote mnafanya biashara ya Duka,, itoayo faida ya milioni 2 kwa mwezi. Watoto wako wakifika darasa la saba ndio mwisho, hakuna sekondari. Aidha waolewe au waoe na kujiendeshea maisha yao wenyewe. Na kaka yako akaamua kuwaendeleza na kulipa takriban 1milioni kwa mwaka kwa kila mtoto. Kimahesabu kaka yako yuko chini kwa 5milion (-5milion), kwa mwaka, nawe utakuwa na +5milion. Kama unadhani nchi iendeshwe hivyo kama mdogo wako +5M)basi Msifu Mkapa, Vinginevyo (-5M) msifu Kikwete.

  Ni Zimbabe tu ndio iliyoshuka GDP yake, nyingine zote zimepanda lakini si kama Tanzania.

  Kifupi unanikumbusha msemo niliousoma humu humu JF, Mwana JF aliandika " If you think that education is expensive, try ignorance"


   
 12. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,717
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  hizi ni takwimu ambazo hazimsaidii chochote mkulima kule kijijinini au mfugaji aliyechomewa boma lake kule arusha hivi karibuni na kudaiwa yeye ni mkenya.....wala mkurya aliyehamishwa pale nyamongo ili kupisha muwekezaji wa Barick....and the list goes on and on....

  My take on this: mwenye shibe hamjui mwenye njaa

  why this now: maandalizi kwa ajli ya 2010
   
 13. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kuna watu wana majibu yao ktk kila suala sasa ukileta majibu tofauti na watakavyo wao hawakubali hawa hawa waliziamini takwimu za hao hao miaka ya nyuma kuonyesha ccm haina uwezo wa kuongoza taifa hili, leo hawa hawa hawawaamini kwa sababu haziwasidiii wao

  wana wivu na fisadi, maana fisadi hana sababu
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Hakuna doubt kuwa, JK bado hajaja na jipya. Sanasana naona kuwa kwenye kipindi chake uchumi umetetereka na utekelezaji wa sera madhubiti za Mkapa kuhusu kudestabilize uchumi zimelegalega, tunaona inflation tunaona increase in gvt spending. Uchumi wetu unashuka, hatuwezi kujifananisha na Zimbabwe ambayo inaporomoka au Somalia. Tujaribu kujifananisha na Kenya au Rwanda.GDP per capita sio kigezo kizuri cha kuonesha maendeleo uchumi au kuonesha maisha bora ya wananchi. Kama tajiri mmoja ameingiza mabilioni ya pesa nchini basi per capita inaweza kupanda hata kufikia dola 2000 lakini inawezekana mtanzania wa kawaida akawa na per capita ya dola 50 tu.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Sep 20, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hapana :

  www.aneki.com siyo website ya CIA. CIA kama chombo cha serikali ya Marekani, website yao lazima iwe na extension ya .gov.

  CIA wanatumia secure servers kwa computer zao zote na website ya CIA ni https://www.cia.gov. Mara ya mwisho nilipofika kwenye ofisi zao na laptop yangu, nilishangaa kutambua kuwa walikuwa wanajua kila kitu kilichoko kwenye hard disk yangu. Kwa bahati nzuri nilikuwa na mambo ya uhandisi tu, kwa hiyo sikupata kashkash yoyote.

  Webpage ya CIA kuhusu Tanzania ni hii hapa.

  Wao wenyewe wamasema hivi kuhusu uchumi wa Tanzania. Napenda uangalie hiyo sentensi ya kwanza kwa vile inazima yote yanayofuatia.


   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ahsante JMK, toka umeingia madarakani, takwimu zote zinaonyesha ukuaji, mashule ya sekondari zaidi ya asilimia 100 juu, vyuo vikuu zaidi ya asili mia 100, mazahanati zaidi ya asilimia 100, kazi mpya zaidi ya asilimia mia moja, uchumi ndio kama hiyo report hapo juu inavyojieleza, kesi zinazosikilizwa na kumalizwa mahakamani zaidi ya asilimia 200, na, na, na, Yote hiyo kwa muda mchache wa kuanzia 2005.

  Ni Rais gani mwingine wa Tanzania aliyeweka rekodi inayokaribia hii? = HAKUNA!
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mashule gani hayo unayozungumzia ndugu yangu? Majengo bila waalimu wenye taaluma? Kama hayo ndiyo maendeleo kwako basi njia ni ndefu.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na idadi ya waalimu Over 100%
  na vyuo vya waalimu Over 100%
  na mishahara ya waalimu imepanda sijui kwa asili mia ngapi?
  na madai ya waalimu yanashughulikiwa kwa kasi kuliko kipindi chochote kile.
  na karibuni tutaanza kuona matunda ya kuipa nchi elimu.

  Kutokuwa na waalimu bora (wasio na taaluma) ni uozo alioukuta JMK na ndio anaushughulikia ipasavyo! Upo hapo ulipo?

  Jee kama hukuanza sasa kujenga mashule na kutumia hao waalimu uozo uliowakuta hao bora utawatoa wapi ghafla ghafla? Kwanza jenga madarasa, pili nyumba za waalimu, tatu tafuta waalimu bora, hata ikibidi kuwaleta kutoka nje ya nchi. Kama huna madarasa, nyumba za kuishi hao waalimu hata ukiwaajiri leo watasomesha wapi? chini ya muembe kama wakati wa awamu zilizopita? hebu fanya fikra japo kidogo tu!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,101
  Trophy Points: 280
  Jasusi ndugu yangu huu ni usanii wa kuzusha takwimu za uwongo ambazo hazina kichwa wala miguu! Miaka nenda miaka rudi tunaambiwa uchumi wetu unakuwa kati ya asilimia 5 na 6 lakini bado Watanzania wasiokuwa na kazi ni mamilioni bado mishahara ambayo haitoshi hata wiki mbili! Nchi nyingine uchumi wao ukikua wananchi wanakuwa wa kwanza kuona manufaa ya kukua kwa uchumi maana purchasing power yao huongezeka na wao watakuwa wa kwanza kusema hivyo siyo kwa kutumia data za kupikwa, kwa mfano Rwanda wananchi wanaona hali bora ya maisha yao. Hizi ni kampeni za kuanza kumsafisha VDG kuelekea 2010 wakati hakuna lolote aliloliweza tangu aingie madarakani bali ni usanii wa hali juu. Juzi si ulimsikia anajivunia rekodi yake ya mapambano dhidi ya ufisadi wakati Chenge bado anapeta, Idrissa bada anapeta, Mkapa bado anapeta, Wakala wa Rada Vethlani bado anapeta, akina Jeetu, Manji, Subhash, Karamagi, Rostam, Lowassa, Msabaha, Mgonja na wengineo chungu nzima halafu mkuu anaona hii ni rekodi ya kujivunia! tena mbele ya hadhara ya Watanzania! Sijui kama atakubali kuna lolote aliloshindwa katika ahadi alizozitoa katka kampeni yake ya 2005 za Mausha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana, Atapitia mikataba ya uchimbaji wa madini yetu ili Watanzania tufaidike na rasilimali zetu badala ya 3% tunayoambalia sasa tangu mwaka 2000 na Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya (labda ya kuwakingia kifua mafisadi)
   
  Last edited: Sep 20, 2009
 20. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
Loading...