Kikwete kafanya mengi kipindi chake cha uongozi, tutamkumbuka...

Haki gani atadai zaidi ya kuchaguliwa kwa kishindo mwaka 2005, hii ya 2010 sio haki yake ni Wizi tu ambao aliusuka na kuufanikisha. Tutamkumbuka sana kama rais mwizi.

mmh, hapo kwenye 'mwizi' atakuwa hajavunja katiba ya JMT, aliyoapa kuilinda na kuitetea?
 
Lazima akumbukwe kwa kuwakabidhi watu wengine URAIS! Baada ya wananchi kumpa nafasi hiyo muhimu!.
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?
Tutamkumbuka kwa ya babu seya... Pia Raisi aliyeomba majina ya Wauza Madawa ya Kulevya Akiahidi kuyaweka hadharani bila mafanikio akiyakalia sijui ataenda kumuelezea muumba wake. Tutamkumbuka kwa kuunda Tume Nyingi... na Safari Nyingi kwa gharama za walipa kodi.. Ahadi zisizotekelezeka ni = na Uongo.. Tutakumbuka Kusurvive kwa miaka kumi bila Raisi Sisi Watanzania tuna uwezo wa kujiongoza wenyewe. tutakumbuka sana tu mze wa kucheka cheka akioneshwa kipande cha chupa akiambiwa ni almasi anapokea kwa furaha huku anacheka kama...!!#@!*) bila kusahau kutuacha tukiwa bado masikini... Long live our Nation
 
Tutakumbuka anavyopenda kutembea nje ya nchi,hata kukiwa na msiba nyumbani kwake!
 
tutamkumbuka kwa jinsi alivyoshindwa kidhibiti mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali ktk kipindi chake na kusababisha hali ya maisha kuiwa tight sana.
 
By the end of 2015 JK will be remembered as the worst president in the history of Tanzania.

Hopefully he will remain the worst from 2015 onwards.
 
Tutamkumbuka kama mtu aliyekosa kutoa leadership wakati inapohitajika, mfano ktk changamoto za upatikanaji nishati ya uhakika, migomo ya wafanyakazi. Vile vila kama raisi aliyepreside wakati wa mikataba ya Ki-Karl Peters mfano TRL, ATCL, DOWANS etc

Vile vile raisi asiyekuwa na vipaumbele vya wananchi bali vya mafisadi.
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?
Bila kusahau ni Rais pekee ambaye alitangaziwa wazi wazi kuwa ameongezewa ulinzi imara toka kwa Yahya Hussein.
 
tusimhukumu sasa. ni ukweli kwamba kwa miaka mitano ameonyesha udhaifu mkubwa kuliko rais yeyote aliyewahi kutawala tz. bado ana nafasi tumhukumu baada ya miaka yake iliyobaki
 
Pia tutamkumbuka kwa kua rais wakwanza tz kuwaumbua mafisadi wanaoiba mali za tz nakuwapeleka mahakamani,pia kuvunja serikaliyake na kumtimua waziri mkuu kwa tuhuma tu zakushiriki ufisadi,hakuna hata rais 1 ktk east africa aliewahi kuwaumbua nakuwatimua mawaziri wake kwa kujihusisha na ufisadi.mnyonge mnyongeni hakiyake mpeni.
 
mkuu ni kweli ILA AKAWATETEA TENA REJEA KAULI YA HOSEA
umesahau amejenga magofu ya udom~
 
Mimi binafsi nitamkumbuka kama mtu pekee aliye madarakani kutokana na maamuzi ya Tume ya taifa ya uchaguzi na si idadi kubwa ya wapiga kura
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?

1) RA/EL wanamakosa gani katika sakata la Dowans?

2) Milipuko ya mabomu imetokea kipindi cha JK lakini inawezekana kabisa kuwa ni hujuma za watu kama wewe mnaomchukia JK bila sababu.

3) Kashfa ya EPA ni JK aliyoiibua na ni JK aliyehakikisha japo baadhi ya hizo pesa zinarudi. Kumbuka EPA ilianza na fedha ziliibiwa kabla ya Kikwete kuwa madarakani.

Tutayomkubuka nayo Kikwete ni mema yote na kujituma kweke.

1) Kwa kipindi kifupi vyuo vikuu 11 na bado hajamaliza muda wake.

2) Mashule ya sekondari zaidi ya awamu zote zilizopita ukijumlisha na tulizorithi kwa mkoloni.

3) Zahanati kila kata.

4) Muhimbili kwa kipindi chake kifupi ameiwezesha kwenye upasuaji wa moyo na mishipa midogo ya fahamu. Na kuwapeleka masposhilisti kibao kusomea fani hizo.

5) Barabara kwa kiwango cha lami ni zaidi ya awamu zote zilizopita na bado.

6) Mortgage kuwawezesha wananchi kupata nyumba kwa mikopo nafuu. Tayari, sijui kama umesikia kitu inaitwa Tanzania Mortgage Refinance Company? Kama bado, subiri utaiona ikiyawezesha mabenki kuwapa watu mikopo.

7) Benki za wakulima? Au na hili hulijuwi?

8) Kuwekeza kwenye pembejeo za kilimo na kuzigawa nchi nzima.

10) Kuweza kuibadili mikataba na makampuni ya uchimbaji Madini na kumchaguwa mbunge wa upinzani kuendesha shughuli za hiyo tume.

11) Kutatua mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar na sasa Zanzibar ni njema.

12) Kufungua midomo ya wapinzani mpaka sasa wanaweza kusikika. Subutu, wakati wa awamu zilizopita!

Na mengine mengi tu.
 
Kila Rais hukumbukwa kwa jambo au mambo kadhaa mazito wakati wa muongo wa uongozi wake. Kwa upande wa JK, wa-TZ watamkumbuka sana kwa mambo makubwa matatu: 1. Vituko vya RA/EL na zengwe la Richmond/Dowans 2. Milipuko ya mabomu huko mbagala na g'mboto 3. Kashfa ya mabilioni ya fedha za EPA. Una lingine la kuongezea hata kama zuri, asije akasema wa-TZ hawajamtendea haki?

Haya mengine sawa ila hili la kashfa ya EPA anayetakiwa kukumbukwa ni Mkapa ambaye ndiye muasisi wa hii kashfa. Jk atakumbukwa kwa kushindwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahusika wa EPA akiwemo Mkapa.
 
Nadhani wana jf waliowengi hutoa maoni yao kwa chuki tu na bila utafiti wa kina ,mara nyingi tunamsahau mtu aliesababisha maisha yakaanza kuwa magumu hapa nchini ambae ni Mkapa na utawala wake,kwani aliuza kila kitu bila hata kufuata maagizo ya babake(Julius),pia aliweza kuhamishia rasilimali kubwa ya wananchi mikononi mwa wageni na kuwafanya wa tz wengi kukata tamaa kabisa tangu kipindi hicho,kilichopo sasa hivi ni kuwa JK anaonekana hafai ni kwa sababu ndie kiongozi pekee ambae ametokea kuruhusu media zote kuwa huru na kuongea chochote na maendeleo ya technology kwa kiasi fulani kumesababisha wananchi wengi kuanza kujua kuwa nini wanastahili.
kwa mtazamo wangu nadhani JK anachojaribu kufanya sasa ni kuhakikisha CCM inakufa na kupotea kabisa kwani alishajaribu kutaka kushirikiana na viongozi wengi katika kuleta maendelo lakini ikaonekana hawapo tayari,kwa hiyo kinachofanyika sasa ni jitahada za kuhakikisha CCM inatoweka kabisa hapa nchini,na ninadhani mimi nitamkumbuka JK kwa hili!ijapokuwa wengi wetu hatujaelewa dhamira yake.
ktk kuconclude ningependa wengi wetu tujitahidi ktk kumuunga mkono JK katika kuhakikisha kuwa CCM inapotea kabisa.
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom