Kikwete kafanya mengi kipindi chake cha uongozi, tutamkumbuka...

na hawa nyoka wa ndimi 2 na wale wa mdimu nani kawaleta? mbona hamlitaji hili nalo neno ingawa sina maana hiyo? kwani ni upepo tu utapita pia ni sehemu ya mafanikio katika nchi yetu jamani kwani hatukuwa nao hapo awali au wanaJF mnalisemeaje kuhusu hili?
 
Jambo zuri hapa ni kuorodhesha ahadi zake zote alizoahidi 2005 na 2010 kama ametekeleza robo tatu ya hizo basi hatutakiwi kumbeza bali kumpongeza ila kama hajafikia hapo na laana iwe juu yake.Anayejua ahadi zake aorodheshe plz!
 
Sitamsahau Jk alipoingia madarakani mshahara ulikuwa 240,000\= leo napata 2,200,000/= ingekuwa ni ridhaa yangu apewe kipindi kimoja cha ziada.
 
Sitamsahau Jk alipoingia madarakani mshahara ulikuwa 240,000\= leo napata 2,200,000/= ingekuwa ni ridhaa yangu apewe kipindi kimoja cha ziada.

imetumika kanuni gani ndani ya miaka saba upanda kutoka 240,000/= hadi 2,200,000/=

sawa na ongezeko la wastani wa 280,000/= kila mwaka yaan nyongeza ya takribani 117% kila mwaka????
 
Kweli kazi tunayo hapa tz kuwa na mtu kama wewe na ndio maana nchi hii ipo hapa kama unampenda huyo jk wako mbebe na mpeleke nyumbani kwako

Ivi kweli wewe "great thinker" ama kwa sababu JF ndo habari ya mjini so tunajiunga tu ivi neno "Democracy" unaelewa maana yake?na je unaijua misingi ya Democracy?sasa kila mtu apende unapopenda wewe?basi washauri wanachama wenzako muununue huu mtandao muendeleze promo zenu
 
Mtu asikudanganye, JK hana hili wala lile. Kadhalilisha wadhifa wa urais Tanzania. Kawa rais ombaomba, mzururaji, mvivu na asiye na maamuzi wala dira yoyote. Nafikiri hana ufahamu wake, anatumia ufahamu wa nguruwe pori!

Hehehe so rais gani ataeingia madarakan kwa nchi hizi Africa ambae hatakuwa ombaomba kwa nchi yake ?ikiwa ugiriki inataka ipatiwe manusura?
 
Almanusura ailete timu nzima ya Real Madrid kwa mabilioni ya walalahoi.

Vipi ulikuwa mshauri ikulu kujua kiasi cha fedha kwa real madrid ama hehe naona umeanza na mabilioni?na je kama waliombwa kwa makubalino maalumu mfano Brazil? Ama ndo "great thinkers"?
 
Anateua wanawake wazuri wazuri wote kuwa wasaidizi wake

lol! Anna Tibaijuka anamfika Oprah wa bongo movie kwa uzuri kwa hiyo(na hemu kwa faida yako usopenda kufatilia vitu bali unapenda kuongea vitu tafuta list ya wanawake wanaofanya kazi ikulu/wasaidizi wake tuwacheki vipi wanasifa hizo ulotoa wewe?
By the way naamin hicho chama unachopenda wewe ndo kina sifa hizo sababu yule jamaa wazinifu wenzake ndo kawapa nafasi pale kitu ubunge
 
Ni kweli mkuu,tumeona maana kateua majaji feki kwa mapenzi yake binafsi na si vigezo, pili amesamehe walioiba pesa ya EPA kwa kuwaambia warudishe tu, amesababisha akina ulimboka kutolewa meno bila ganzi.nk. Amefanya meeeeeengi mazuri!
 
Kumsifia kikwete ni kutowatendea haki watanzania. Eehh Mungu, tuvushe salama na uongozi huu wa kikwete asiyejua kwa nini tunasafiri na wapi tunakoelekea!
 
Hehehe so rais gani ataeingia madarakan kwa nchi hizi Africa ambae hatakuwa ombaomba kwa nchi yake ?ikiwa ugiriki inataka ipatiwe manusura?

nchi ombaomba lakini angalia magari wanaotumia viongozi wetu..hivi kesha ni ombaomba kama sisi na raisi wao anasafiri kama wetu au hana ndege ya kusafiria..
 
Hakuna hata moja zuri alilofanya kwa maendeleo sahihi ya watanzania....

Kama kuna mambo yanamtambulisha Mtu Mjinga ni maandishi au maneno!
Honestly ! I don't wanna be part of it!
Lakini hizi tathmini za magufuli Kia katika historia ya nchi yetu kipindi hiki barabara zimejengwa sana hazina ukweli AMA ?

Pili hivi Kama kukubali ukweli na ukaishi bila kuathiri mind yako kuna nini!
QUOTE

THINK POSITIVE, NEGATIVE THINKING HAS BIOCHEMICAL EFFECT IN YOUR BRAIN,
So I'm not here to elaborate biochemical but to atleast to Let you be objective on whatever you are going to say or write coz kuna watu wengi wanasoma hizi message na wanafikiria sana sasa km wewe unakosoa na Unachokosoa ni single line tu hujengi hoja! Nadhani utakua unaangukia kwenye kauli Mjinga msubiri aandike au afungue mdomo
 
Atakumbukwa kwa kwenda kuzoa kile kibabu kilichokuwa kinalima Nyanya huko Iringa ambacho hata meno hakina Kikongwe Mangula
 
lol! Anna Tibaijuka anamfika Oprah wa bongo movie kwa uzuri kwa hiyo(na hemu kwa faida yako usopenda kufatilia vitu bali unapenda kuongea vitu tafuta list ya wanawake wanaofanya kazi ikulu/wasaidizi wake tuwacheki vipi wanasifa hizo ulotoa wewe?
By the way naamin hicho chama unachopenda wewe ndo kina sifa hizo sababu yule jamaa wazinifu wenzake ndo kawapa nafasi pale kitu ubunge

Ndo maana nchi hii itaendelea kuwa masikini kwa kuwa watu km wewe hawajishughulishi kufikiria
 
nchi ombaomba lakini angalia magari wanaotumia viongozi wetu..hivi kesha ni ombaomba kama sisi na raisi wao anasafiri kama wetu au hana ndege ya kusafiria..
Viongoz wa ugiriki wameranda sana hizo nchi za shirikisho lao ili waweze kunusuriwa uchumi wao tu sasa usishangae kiongoz kusafir kikazi ama ukiskia kaenda kula bata tu hapo ndo pakushangaa!
 
Vipi ulikuwa mshauri ikulu kujua kiasi cha fedha kwa real madrid ama hehe naona umeanza na mabilioni?na je kama waliombwa kwa makubalino maalumu mfano Brazil? Ama ndo "great thinkers"?

Kijana nadhani hauna data. Real madrid ilitoa masharti ya kuja hapa nchini ambayo gharama yake ilikuwa ni bilioni moja kwa siku ikiwa ni malazi, chakula, posho ya kulipa wachezaji wake kwa siku zote watakazokuwa hapa.
Usifikiri watu tunaropoka tuu. una lingine?
 
Back
Top Bottom