Kikwete kafanya mengi kipindi chake cha uongozi, tutamkumbuka...

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
695
12
Kikwete amefanya mambo mengi nataka niwakumbushe tuu watanzania wenzangu.

1) Amepandisha mfumuko wa bei kutoka asilimia 4 mpaka asilimia kumi na tano,
2) Amesafiri mara nyingi nje ya nchi na mara nane kwenda marekani.
3) Bei ya mafuta imepandisha kwa kasi sasa ni sh.1600 kwa lita.
4) Amezindua mpango wa kibiongo kwanza na mfuko wa mbolea laki.
5) Amekataa kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa chini na kuwatishia kuwapiga na kuwafukuza kazi.
6) Amemteua Sofia Simba kuwa waziri wa utawala bora ambaye yuko makini kweli kweli.
7) Amesaini sheria ya uchaguzi aliyobambikiwa kwa mbwembwe.
8) Amewachekea mafisadi.

Tutamkumbuka kwa mengi sana hasa hili la kukemea mgomo wa wafanyakazi na kucheka na mafisadi amejitahidi kwa kweli tumpongeze kwa hilo.
Amejenga UDOM,
Amejenga sekondari kila kata ya NCHI hii,
Kuna kesi mahakamani zaidi ya 15 za rushwa kubwa nchini,
Daraja la Msumbiji limekamilika,
Barabara ya kusini na ile ya Mwanza zinakamilika mwaka huu,
Uhuru wa habari umepanuka sana, humu JF tunamkejeli tunavyotaka,
Karuhusu swahiba wake EL aende na maji,......................................
Great thinkers always view things in three dimension.

Mimi kama binafsi ninaona kuwa japo JK kuna mambo yanamshinda kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake ila ninampa credit kama kiongozi kwa mambo yafuatayo.

1. Uvumilivu: Nina uhakika kabisa kuwa JK ana uwezo wa kutumia mkono wa chuma katika kuiongoza nchi kwa kunyamazisha kila mpiga kelele, lakini ameacha wazi watu waseme yanayowakera (at least kwa hili kuna advancement of freedom of expression)

2(a). Transparency: Kuna mambo ya funika funika mengi sana yamekuwa yakifanyika kabla ya JK kuwa madarakani laiti kama yangefunuliwa nafikiri tungemuona JK ni shujaa kwa sasa. Tulikuwa tunazisikia reports za CAG, lakini hivi sasa zipo open japo kupitia mtandaoni.

2(b). Kama angeamua kuizima issue ya EPA angeweza kwani nina uhakika kabisa kuwa kabla ya uamuzi wa kumteua Auditor serikali ilikuwa inajua madudu yaliyofanywa katika kutafuta pesa za uchaguzi 2005 na baadhi ya watu ku-take advantage, angeminya information zote kutoka, hakuna ambaye angejua nini kilifanyika, Ila sasa tunajua na Manyang'au wote wanajiuliza mara mbilimbili kufanya anything of that nature again.

2(c). Mauaji ya wafanya-biashara wa mahenge akina Chigumbi, uchunguzi wa tume aliounda uliwekwa hadharani na hatua kuchukuliwa tofauti ilivyokuwa ikifanywa na wa kabla yake mambo yote yalikuwa yanaishia kwenye makablasha. hatua hii pia inaleta nidhamu kwa polisi waliobaki kuwa ukiharibu utafunuliwa tu.

UBAYA WA JK TUNAUONA NI KWA KUSHINDWA KUWACHUKULIA HATUA WATUHUMIWA, LAKINI NCHI YOYOTE YA SHERIA RAIS SI MAHAKAMA AU POLISI KUWA KILA KITU LAZIMA ATOE AMRI YEYE. WATENDAJI WA CHINI WANAOGOPA NA HATA WANAFIKIA KUSEMA NCHI ITACHAFUKA WATU FULANI WAKIGUSWA(KUMBUKA KAULI YA IGP-MWEMA) SASA UNATARAJIA JK AFANYE NINI?.

NINA UHAKIKA KABISA KUWA JK NAE KAMA BINADAMU BADO ANAHITAJI KUISHI (UNAKUMBUKA KAULI YA MKAPA?) SASA KAMA NCHI HAIJAFIKIA KIWANGO CHA KUMHAKIKISHIA ULINZI 100% NI LAZIMA AWE MWANGALIFU NA GENGE LA MAFIA WANAOITAFUNA NCHI.

LAWAMA ZANGU KUU KWA JK NI KUNG'ANG'ANIA KAZI AMBAYO INATAKA MAAMUZI MAGUMU NA MAKUBWA WAKATI AKIWA AMEZUNGUUKWA NA WATUHUMIWA AMBAO ANATAKIWA KUCHUKUA HATUA DHIDI YAO, ANGETANGAZA KUWA PEMBENI NA KUMTAFUTA MTU JASIRI AMUUNGE MKONO KUONDOA UOZO HUO HATA KAMA ATATOKA UPINZANI KAMA DR. SLAA. ANGEFANYA HIVYO BASI NI KWELI TUNGEMLILIA SANA BAADA YA MIAKA MITANO IJAYO KUWA NI RAIS ALIYEIOKOA TANZANIA TOKA KWENYE MIDOMO YA SHARK (MAFISADI) LAKINI NA HUU NAO NI UAMUZI MGUMU AMBAO PIA HAUWEZI.
 
Amekaribisha wageni wengi IKULU kwa tafrija...ma Lunch..ma Dinner kwa pesa za kodi zetu ..........wageni ambao ujio wao hauna tija kwa Taifa
 
Amedhalilisha Umma wa Wafanyakazi wote wa Tanzania...........na kendelea kuwakumbatia Mafisadi
 
Almanusura ailete timu nzima ya Real Madrid kwa mabilioni ya walalahoi.
 
Amejenga UDOM,
Amejenga sekondari kila kata ya NCHI hii,
Kuna kesi mahakamani zaidi ya 15 za rushwa kubwa nchini,
Daraja la Msumbiji limekamilika,
Barabara ya kusini na ile ya Mwanza zinakamilika mwaka huu,
Uhuru wa habari umepanuka sana, humu JF tunamkejeli tunavyotaka,
Karuhusu swahiba wake EL aende na maji,......................................
 
Kuna kesi mahakamani zaidi ya 15 za rushwa kubwa nchini,
Mimi nimeipenda hii, kama kuanzisha kesi ni sifa kwa nini asianzishe kesi zingine 100 ziwe zinapigwa kalenda hadi atakapomaliza muda wake?
 
Mimi nimeipenda hii, kama kuanzisha kesi ni sifa kwa nini asianzishe kesi zingine 100 ziwe zinapigwa kalenda hadi atakapomaliza muda wake?

Lakini angalau ameonyesha kautashi kidogo. Mramba huyu anayeburuzwa mahakamani hivi sasa hatakuwa tena Mramba wa enzi ya Mkapa hata kama atashinda kesi hii.
 
JF Premium Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

Wilcard Kwa taarifa yako; Yafuatayo ni mIradi iliyobuniwa na kuanzishwa na Mkapa;
Ujenzi wa sekondari kila kata ya NCHI hii,

Ujenzi wa Daraja la mkapa,
Barabara ya kusini na ile ya Mwanza na nyingine nyingi
 
Amejenga UDOM,
Amejenga sekondari kila kata ya NCHI hii,
Kuna kesi mahakamani zaidi ya 15 za rushwa kubwa nchini,
Daraja la Msumbiji limekamilika,
Barabara ya kusini na ile ya Mwanza zinakamilika mwaka huu,
Uhuru wa habari umepanuka sana, humu JF tunamkejeli tunavyotaka,
.........................................

Underlined:: Hizi shule unaweza kumpeleka mtoto wako kama wewe ni muungwana??

Red: Haya ni maendeleo ya mikakati ya Mr Ben Mkapa
 
jf premium member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png

wilcard kwa taarifa yako; yafuatayo ni miradi iliyobuniwa na kuanzishwa na mkapa;
ujenzi wa sekondari kila kata ya nchi hii,

ujenzi wa daraja la mkapa,
barabara ya kusini na ile ya mwanza na nyingine nyingi

pia chuo cha udom kimebuniwa na mr ben, jk kafanya kadandia kama kawaida yake ya kundandia meli ikwa imeondika
 
Underlined:: Hizi shule unaweza kumpeleka mtoto wako kama wewe ni muungwana??

Red: Haya ni maendeleo ya mikakati ya Mr Ben Mkapa

Wapo watoto wa WATANZANIA wenzetu wanasoma huko. Wachache wamevuka kwenda kidato cha tano. Rais ajaye angalau ana pa kuanzia.
 
Tunataka miradi ambayo kabuni J.K. Labda kauli mbiyo ya Kilimo Kwanza na kupaisha bei ya mbolea, sukari, chumvi, sabuni, mafuta ya kula, unga, mchele, na kila kitu wakati mshahara ni uleule!!!!!
 
Lakini angalau ameonyesha kautashi kidogo. Mramba huyu anayeburuzwa mahakamani hivi sasa hatakuwa tena Mramba wa enzi ya Mkapa hata kama atashinda kesi hii.
Hatukuchagua rais wa 'angalau' wa kufanya majaribio, basi safari hii tumpe Mtikila 'angalau' na yeye ajaribu.
 
pia chuo cha udom kimebuniwa na mr ben, jk kafanya kadandia kama kawaida yake ya kundandia meli ikwa imeondika

Siamini kama hili ni kweli. Mfutieni Mkapa dhambi zake chache alizofanya basi! Halafu, angalau JK ameyafanyia kazi haya ambayo yote mnamlundikia mtangulizi wake. Unakumbuka mradi wa maghorofa ya Michenzani kule Zanzibar alooyaacha Mzee Abeid Amani Karume? Walipita Marais wanne pale na hawakuyafanyia kitu hadi Rais wa sasa ambaye ni mwanae ndiye amekuja kuyamalizia. JK anafanyakazi bwana.
 
Amejenga UDOM,
Amejenga sekondari kila kata ya NCHI hii,
Kuna kesi mahakamani zaidi ya 15 za rushwa kubwa nchini,
Daraja la Msumbiji limekamilika,
Barabara ya kusini na ile ya Mwanza zinakamilika mwaka huu,
Uhuru wa habari umepanuka sana, humu JF tunamkejeli tunavyotaka,
Karuhusu swahiba wake EL aende na maji,......................................

weweeee

daraja si lake (nkapa)
mpango wa shule si wake ( nkapa)
bara bara (nkapa)

hayo mengine yasiyo na tija kwa taifa ndo yake
 
Back
Top Bottom