KIKWETE ! Kaa chini na CHADEMA muongee ili muyamalize

Mpeni sifa Yesu

JF-Expert Member
May 23, 2010
646
125
Ninaongea kwa moyo wangu wote, kutokana na hali halisi ninavyoiona, kwamba wabunge wa Chadema wana dukuduku moyoni, na pamoja na kwamba wana ccm wanajua ya kuwa chadema wana dukuduku, wao hawataki kushusha munkari na kuheshimu hisia za chadema wakawaombe au propose kwa chadema ili wakae chini wafanye diplomacy, wayaongee wayamalize, kama kuwekeana mikakati na ahadi etc wafanye.

matokeo yake, kikwete na ccm wote wanaongea kwa hali ya kujiamini bila kuheshimu hisia za chadema, na chadema ambao wanazo legitimate allegation kinawauma na dukuduku/chuki inazidi kukua.

NAKUSHAURI KIKWETE, ukiachia hii chuki izidi kukua mioyoni mwa watanzania na mioyoni mwa wanachadema wote, hautakuwa umejenga kitu chochote. ila ukijifanya mjinga siku ipite, ukawaambia chadema tukae chini tuyaongee tuyamalize ili tusipoteze muda na mambo haya tuendelee kujenga nchi, hapo NDO NITAKUONA UNAZO BUSARA NZURI.

Nakuambia kabisa, jambo hili ukilichukulia mzahamzaha na kutamka kauli kama zile ulizotamka wakati wa hotuba yako, unaacha sumu mioyoni mwa watz wengi sana, hata kama wengi wanaugulia moyoni kwasababu hawana pa kuongelea. Huu ndio ushauri wangu kwako.
 

vicenttemu

Member
Nov 16, 2010
43
0
Yah, wazo lako ni jema Mkuu. Lakin itakua ngumu kukaa meza moja aisee. Inavyooneka kuna jambo ndani ya mioyo. Reconciliation inawezekana lakini.
 

Mpeni sifa Yesu

JF-Expert Member
May 23, 2010
646
125
ni kweli, hata kama jambo liko moyoni, lakini wanavyoendelea kukaa kimya, machuki yanaendelea kukua ndani ya mioyo, siku majipu yakilipuka wanaanza kuumizana. ni wazi kuwa ccm wameboronga na kwa hili hawatakiwi kutumia ubabe, wawe wapole, washuke tu ili wayamalize..mbona kila kitu kiko wazi?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom