Kikwete Jiuzulu uinusuru nchi...

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,551
29,633
Kwa heshima na taadhima pia kwa uchungu naandika.

Rais wangu umeonesha maendeleo makubwa katika kusifiwa na kupewa chapuo kama kiongozi bora na wa kuigwa hapa kwetu na Afrika Mashariki. Nina dukuduku na maswali lukuki kuhusu yanayoendelea kutendeeka hapa nchini bila ya wewe kuonesha kukerwa ama kuchukizwa hata basi kukemea wahusika maana iinaonesha kuwachukulia hatua hao wanaoyatenda ni vigumu sana kwako kwa sababu whusika ndiyo wanaowachukulia hatua wale wote wasaiokubaliana na udhaifu wako kiutendaji.

  1. Tumekupa katiba UILINDE lakini inaendelea kuchezewa hasa kwa serikali yako kupoka haki za raia kikatiba kama vile Uhuru wa kutoa maoni na kupata habari mbapo wateule wako wamekuwa wakifanya maamuzi yanayokinzana na dhana ya Natural Justice huku wakitumia sheria kandamizi ambazo wamekimbilia Bungeni kutaka ziwe na meno makali zaidi. Ikumbukwe kwamba pamoja na uwepo wa sheria kandamizi ya Magazeti nchini, imetaja kuwepo na kiwango cha muda cha kufungia gazeti ama chapisho linalokwenda kinyume na ukandamizi huo. Hiyo kulifungia Mwanahalisi kwa Muda usiofahamika ni kukiuka hata sheria yenyewe kandamizi. Rais haujaonesha wala kuchukua hatua
  2. Imefikia sassa viongozi wameanza kuonja machungu ya Mob Justice baada ya wananchi kuchoshwa na mfumo wa utoaji haki na hata kuchoshwa na namna viongozi chini ya utawala wako wanavyojitwalia mamlaka yaa uungu dhidi ya raia. Rais haujaonesha kukerwa wala kukemea.
  3. Vyombo vyako vya dola hususani jeshi la polisi limejikita kuwashughulikia watanzania badala ya kuwasaidia kama Katiba inavyoamrisha. Tumeshuhudia Mwangosi akiuawa mbele y RPC tena wauaji wakiwa ni polisi wenyewe na hadi sasa hujawahi kusema lolote ama kukerwa na tukio lile, Morogoro polisi waliua raia kwa risassi za moto wakidhibiti wanasiasa wanaofanya shughuli zao kwa mujibu wa Katiba lakini haukuonesha kukerwa wala kukemea. Polisi wameendelea kutumika dhidi ya wanasiasa walio na fikra tofauti na za chama chako na kuwadhalilisha badala ya kutimiza jukumu lao la kikatiba na hata mwenye macho anajiuliza ukokotozi wa idadi ya wnausalama wanaopaswa kulinda makusanyiko inavyozidiwa kwa mbali na idadi ya wanausalama wanaotumika kufanya mashambulizi hatimaye mauaji kwenye makusanyiko halali kikatiba.
  4. Ongezeko la UHALIFU nchini limekuwa kubwa hadi kupelekea raia kukosa imani na serikali yako hususani vyombo va kutoa na kusimamia haki.
  5. Mawaziri wako ni mzigo kwa nchi yetu kutokana na kukosa weledi na tija. wengi wana Uholela wa maamuzi, Kejeli na dharau kwa wananchi, wizi wa mali ya umma na hata wakuu wa mikoa, wilaya , wakurugenzi na wengine kwenye kada hiyo wamekosa uhalali wa kuaminiwa utumishi wa umma kutokana na kukosa usimamizi imara na thabiti kutoka juu. Hilo haujawah kuoneshwa umekerwa na haujawahi kujibu malalamiko ya wananchi kwenye maeneo tajwa
  6. URITHI WA TAIFA, hapa naongelea maliasili, nishati na madini ambavyo vilipaswa kuwa mkono wa kulia wa uchumi wetu na vingeweza kusaidia Watanzania kutoka ktk lindi la umaskini na kuishi kwenye nchi yenye uchumi unaokua wa viwango maridhawa. Tumeshuhudia IIdadi kubwa ya Tembo wanaouawa na pembe zao kutoroshwa, na hata zinazokamatwa kuna kulegalega kuwachukulia hatua wahusika wanaotajwa moja kwa moja kuhusika na kashfa hizo. Wewe na serikali yako tena mkizingatia HASARA kubwa Taifa iliyoipata kupitia mikataba mibovu tena yenye usiri mkubwa ya madini na makampuni ya nje, mmedhamii kutumia njia ile ile ktk kuuza nishati ya Gesi na Mafuta tena zikitumika njia za kibabe kuwaengua Watanzania wenye uwezo wa sekta hiyo kuwekeza. Kejeli za watendaji wako, kebehi zao hata ubabe wao HAUJAWAHI KUKUKERWA rais wetu. Tunakuangalia machoni unaonesha kutoguswa kabisa na madudu yaa wasaiddizi wako.
  7. STAHIKI ZA WAFANYAKAZI, kada nyingi ndani ya serikali yako zinanyanyasika kutokana na mapunjjo, unyanyasaji na hata makato ya ajabu kupitia mishahara yao. Tunakumbuka tulivyopoteza wapendwa wetu kupitia migomo ya Madaktari ambapo hata kwa njia ya mgomo serikali yako iliziba masikio na kutumia nguvu kubwa kuhadaa jamii kwamba madaktari wale waligoma kwa sababu ya mishahara na si uboreshwaji wa mazingira ya utoaji huduma na upatikananji wa tiba sahihi. Tunakumbuka migomo ya waalimu ambapo tumevuna kiwango kikubwa cha wanaofeli kila uchao kutokana na serikali yako kuwapuuza na kushusha ari ya waalimu ktk kutoa elimu bora kwa wenentu. Bado tnakumbuka ile kauli yako maarufu mbele ya wazee waDsm kuwa kama Wafanyakazi wataendelea kugoma basi wengine watalazimishwa kufika kenye meza ya mazungumzo wakiwa na ngeu na bandeji na pia hata kura zao huzitaki, Uliliongea hili mbele ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Hili hukuwahi kulikana wala kurekebisha kauli yako

Kuna mengi sana ambayo yanagusa utendaji wako na hukuwahi kuonesha hata nia ya kuyaweka sawa, machache ni.
  • Ukiritimba wa TANeSCO na namna wanasiasa wanavyoliingilia shirika kiutendaji,
  • Ripoti za CAG kutotumika kuondoa viongozi na watendaji wabovu badala yake wanalindwa
  • Sheria za mipango miji kutkelezwa bila kushirikisha kikamilifu whau wote husika ambapo hupelekea displacement ya raia wako ndani yya nchi yao.
  • Ukiritimba wa TRA kwenye ukusanyaji w kodi na hasa Ushuru wa Forodha ambapo nchi inakosa kipato kikubwa kwa sababu ya umungu wa mamlaka hii kwenye eneo hilo.
  • Wakulima wamekuwa wakiburuzwa kuanzia kwenye kupanga bei na soko la bidhaa zao huku wakikatwa makato lukuki seuse kutolipwa kwa wakati.
  • Mauaji ya kimya kimya yanayoendelea nchini dhidi ya watu wanaoonesha kutokuwa na imani ya utendaji wa serikali.
  • Utekaji nyara, kuwapiga na kuwadhibiti wale wote wanaoipinga serikali kana kwamba ni maadui wa nchi.
  • Wageni wengi kuingia nchini kinyemelaa na kushika nafasi ambazo Watanzania wana uwezo wa kuzishika.
  • Uhamiaji kuhusika kuwaingiza wageni wasio halali.
  • Polisi kulinda whalifu
  • Mahakama kuingiliwwa ktk maamuzi yake
  • Bunge kutumika kama fimbo na mhuri wa watawala dhidi ya matumaini ya raia.

Tunasikitika kumpoteza kipenzi chetu na wengi Mandela, na tunashukuru kwa namna ulivyotuwakilisha kwenye maziko yake. Lakini haiyumkiniki kufanya safari mbili kwa msiba mmoja labda utuambie kwamba HAZINA haikuhusika na gharama za kukupeleka na ujumbe ulioambatana nao safari zote mbili. IIlitosha kwa taasisi yako kuhudhuria tukio moja la mazishi yale ili kuoko gharama za walipa kodi.

Ni mengi mno, naamini wanaJF wenzangu wana orodha ya mambo ambayo yanakupa uhalali wa wewe kujiuzulu.

Kwa nini Rais ASIJIUZULU?
 
Akili za gongo hizi kutoka Bavicha.

Wewe rais wako si ndo Slaa? kama unaona mambo hayakupendezi ondoka Tanzania.
Kwa namna mlivyopost majibu kwa haraka ni wazi mlisoma heading tu na kuamua kujibu thread nzima.
Hii post haihusiani na CHADEMA wala kundi lolote, inahusiana na Maongozi ya nchi na udhaifu wa mamlaka ktk kutimiza wajibu wake.

Leteni hoja KWANINI ASIJIUZULU?
 
Kauli nzito hii lakini sio ajabu ikawa na mashiko. Hii ni kwa sababu Katibu mkuu na mwenezi wake walipotaja mawaziri mizigo wote wanakana kuwa sio mizigo hivyo kututia mashakani sisi wananchi wa kawaida kujua ni wapi 'mzigo' umekaa. Pia kauli ya mbunge mmoja bungeni kusema kuwa timu ikifanya vibaya basi kocha ndio atimuliwe na sio wachezaji. Ngoja waje wajuzi wa mambo watueleze lakini.
 
Kauli nzito hii lakini sio ajabu ikawa na mashiko. Hii ni kwa sababu Katibu mkuu na mwenezi wake walipotaja mawaziri mizigo wote wanakana kuwa sio mizigo hivyo kututia mashakani sisi wananchi wa kawaida kujua ni wapi 'mzigo' umekaa. Pia kauli ya mbunge mmoja bungeni kusema kuwa timu ikifanya vibaya basi kocha ndio atimuliwe na sio wachezaji. Ngoja waje wajuzi wa mambo watueleze lakini.

Ni vema tuanze na mbowe aliyechakachua katiba ili atawale milele chadema.
 
Msanii Mambo uliyoyaeleza yanaweza kuondolewa kwa kurekebisha utendaji na si rais kujiuzulu. Mshauri awabane watendaji wake badala ya kumtaka akimbie majukumu.
 
Last edited by a moderator:
Yaani bavicha wamekalia kulia lia tuuuu utafikiri akili zao zipo kibandamaiti. Hivi ni Rais gani anayemtaka ajiuzulu? Ni huyu wanayemuita Rais, Babu Slaa?
 
Kwa namna mlivyopost majibu kwa haraka ni wazi mlisoma heading tu na kuamua kujibu thread nzima.
Hii post haihusiani na CHADEMA wala kundi lolote, inahusiana na Maongozi ya nchi na udhaifu wa mamlaka ktk kutimiza wajibu wake.

Leteni hoja KWANINI ASIJIUZULU?

kwa tarifa yako watu wanajibu kwa umakini mkubwa wanajua mpaka unachowaza usishangae kujibiwa mpaka unayowaza ndani ya moyo wako.
 
Mambo uliyoyaeleza yanaweza kuondolewa kwa kurekebisha utendaji na si rais kujiuzulu. Mshauri awabane watendaji wake badala ya kumtaka akimbie majukumu.
Mkuu, babu yake Slaa alivyoona kuwa hawezi kuishi maisha ya ndoa, suluhisho ni kuishi na mahawara kila kukicha akiwaita eti ni wachumba. Ndo akili za bavicha hizo
 
Vitu vingi ulivyobainisha ni vepesi vyote vinaisha kwa kwa kurekebisha kidogo tu kwenye utendaji na uwajibikaji wala humgusi rais lakini kwa vile wewe unachuki na rais ndiyo maana umeenda kumdandia rais,
 
Mambo uliyoyaeleza yanaweza kuondolewa kwa kurekebisha utendaji na si rais kujiuzulu. Mshauri awabane watendaji wake badala ya kumtaka akimbie majukumu.
Kujiuzulu si kukimbia majukumu bali ni KUWAJIBIKA.

Kukubali nchi kuenenda kama hain kichwa ni sawa na kupeleka mifugo machungoni bila mwangalizi. Ni nani anamchagulia wasaidizi wake? Tuanzie hapo
 
Naunga mkono hoja, atakayepinga hii hoja lazima atakuwa na upungufu wa akili au anafaidika moja kwa moja na uvinjifu huu wa katiba na matumizi yasiyoyalizima ya kikwete
 
Naunga mkono hoja, atakayepinga hii hoja lazima atakuwa na upungufu wa akili au anafaidika moja kwa moja na uvinjifu huu wa katiba na matumizi yasiyoyalizima ya kikwete
Mkuu, hivi ile hoja ya nchi isitawalike imeishia wapi? Na ule mkakati wenu wa kumng'oa JK kabla ya 2015 umeishia wapi?
 
Back
Top Bottom