BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,009
Mimi siku hizi ninashangaa sana ninaposikia watu wengi wakimuorodhesha Muungwana kama mpambanaji dhidi ya mafisadi!! Jakaya ni fisadi nambari wani kwahiyo kwake si rahisi kuwatosa wakina RA na EL akifanya hivyo atakuwa anacommit suicide; the most he does ni kujifanya akiwa jukwaani kuwa anapinga ufisadi kumbe nyuma yake anaukumbatia; kudhihilisha ninayosema nyie ngojeni maadam amepitia Dubai akirudi tu, utasikia serikali imeamua kununua mitambo ya Dowans!! Msijekushangaa huyo ndio mnamuita mpambanaji wenu!!
Naam huyo ni fisadi Nambari one nakubaliana na wewe katika hili. Sakata lote hili la Richmond/Dowans likiendelea yeye kaamua kukaa kimya kabisa bila kutoa kauli yoyote. Mkurugenzi wa TANESCO anatutisha Watanzania eti nchi ikiingia kizani basi TANESCO isiilaumiwe, bado tu Rais wa nchi yuko kimyaaaa halafu yule comical Salva anasema Rais hahusiki kabisa na swala la Richmond/Dowans. Halafu hii njemba inataka kugombea tena 2010!!!! Kazi kweli kweli!!!! I hope watatokea watu ndani ya CCM kumpinga maana kama tungekuwa na katiba yenye kuweka maslahi ya nchi mbele huyu asingemaliza hata awamu yake ya miaka mitano. Angekuwa ameshaondolewa madarakani siku nyingi sana.