Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Ndugu yetu Hutaki Unaacha, kwanza asante kwa muendelezo huu, pili naweza kukubalia yote uliyoyasema kwa sababu mengi siyajui japo baadhi niliwahi kuyasoma katika zile dossier za Mzee Mwanakijiji ambazo alizitoa kwa subscription.

Ila hili la ubunge wa Tom hoja zako si za kweli. Ukweli kuhusu ubunge wa Tom ni juhudi binafsi za baba mtu kujaribu kuestablish his legacy baada ya yeye kuondoka ili angalau angalau jina lake lisi persish jumla kwenye power corridors kama Mwinyi, Karume, Kawawa etc.

Hivyo kabla ya uchaguzi alitumia fedha nyingi kuwekeza kwenye kilimo Mbeya huku akimgroom mwanaye kwenye politics huku akisaidiwa sana na vijana wa idara!.

Kusema ukweli lobbying ya hali ya juu ilifanyika ili kijana abebwe na vikao vya juu ila kwa vile Mpesya alisha cry foul ndipo aibu ikawashika na kuamua kumtosa mtoto wa Mzee jambo ambalo lilimsononesha sana baba.

Ndipo kwa kutumia utaratibu wa scrach my back and I'll scrach yours kwa huko walikotoka, then It was time to pay off kwa Mzee kumuomba muungwana ambebe kijana wake hata kwa mbeleko tuu ili kumsetiri aibu ya kushindwa!. Ndipo akamteua!.

Si kweli uteuzi ule ulikuwa ni asante kwa kuiba siri za kambi kwa sababu its obviously Waarabu wa Pemba hujuana kwa Vilemba with reference ya siasa za Mbeya, Baba na mwana walikuwa lazima wawe kambi moja ya mwenzao Prof. lakini ili kuua so, ilimbidi baba amtume mwana kule na yeye abaki kambi ya Jk hivyo hakuna cha wizi wa siri wala nini!.

Nasisitiza ubunge wa kijana yule sio ubunge wa shukrani kwa kazi yoyote nzuri bali ni ubunge wa hisani tuu!. Ungekuwa wa shukrani ungeandamana na uteuzi wa ujumbe wa bodi kwenye bodi zozote nono nono ili kijana ajilie vinono!.

Wanasema ukishikwa, shikamana na ukibebwa, bebeka!. Kijana mpaka kabebwa habebeki aingekuwa ni shukranisi angeendelea kuning'inizwa huko huko juu alikopandishwa?. Mbona sasa ameachwa akaporomoka?!. Sio shukrani ni hisani tuu!.
 
Mungu wangu! Nchi inaendeshwa na CIA huku tukijinasibu kuna TISS? Hakika cku tukifunga ndio hapo Natural Resources zetu zitakua zimeisha kabisa,Rostam mtu hatari sana huyu kwa mustakabali wa Taifa letu.
 
Acheni wasiwasi, hakuna ambacho kinasemwa hapa ambacho hakijulikani in the corridors of power za Tanzania. Na kwa wale wasomaji wa muda mrefu wa JF wanaweza kukumbuka mengi humu yameshasemwa hadi yamechosha. "Hutaki Unaacha" ameyaweka kwa mtiririko wake wa asili na kuunganisha. Mada hii itakuwepo na itaendelea kusoma JF is where "where we dare to talk openly"... just returning to our roots!

Jukumu la mwenye akili ni kujua hesabu za MAGAZIJUTO!
Mzee Mwanakijiji sio siri mwanzo nilifikiri huyu jamaa ni wewe umeamua kutoka kivingine nikikumbuka zile enzi za zile secret dossiers!. Ukijumlisha na ukimya wako wa kutochangia chochote kwenye ile sehemu ya kwanza, nika reach conclusion ni wewe!. Kumbe I was wrong!. Welcome on this!.

Kuna mambo Rev. Mtikika aliwahi kuyasema kumhusu huyu jamaa na double personalities tulimuona Mtikila kama amechanganyikiwa!. With this revelations sasa naanza kuelewa kidogo kidogo the source of powers behind the so called King Maker and why the hell he is just so poweful!.
 
Mzee Mwanakijiji sio siri mwanzo nilifikiri huyu jamaa ni wewe umeamua kutoka kivingine nikikumbuka zile enzi za zile secret dossiers!. Ukijumlisha na ukimya wako wa kutochangia chochote kwenye ile sehemu ya kwanza, nika reach conclusion ni wewe!. Kumbe I was wrong!. Welcome on this!.

Kuna mambo Rev. Mtikika aliwahi kuyasema kumhusu huyu jamaa na double personalities tulimuona Mtikila kama amechanganyikiwa!. With this revelations sasa naanza kuelewa kidogo kidogo the source of powers behind the so called King Maker and why the hell he is just so poweful!.
Pamoja na kushtushwa na taarifa hizi lakini bandugu na Adm nzima ya JF,hapa tunaanza kugusa na maslahi ya Marekani na for sure lazima watafuatilia effect ya taarifa hizi! Ninavyofahamu wanaweza kujaribu hata kuingilia mtandao huu kwa maslahi yao! Naamini JF imekomaa sasa wataweza kudetect any threat! Umakini uongezeke kidogo maana haya ni kwa maslahi ya taifa hili na kumsaidia Rais wetu ajue hali ilivyo kwa mapana yake.
 
Wow!

Ni Lowassa pekee ndie atakayemsaidia JK akimaliza term yake. Ndugu yangu Pasco haulali?

2015 ni Lowassa!
Mkuu FP, ki ukweli hakuna kulala!.

Baada ya kusoma hii, sasa ndio nimeanza ku connect the dots za source of powers za huyu jamaa RA!. Kama haya ni kweli, na kama mtu wa RA ni EL, na kama mambo yenyewe ni haya, kwa jinsi nchi yetu ilivyo masikini, nashauri 2015 tusipoteze muda na fedha kufanya uchaguzi wa rais!. Jee tumfungulie tuu njia awe mgombea pekee atangazwe moja kwa moja is kuzuia wastage of time and money?.
 
Mkuu mwaga data zake zote na hata ushahidi wowote ambao utawaacha hawa mafisadi uchi maana watu washasema sana kuwa tunaishi na majambazi na majasusi ya ki mataifa lakini serikali inajifanya kichaa na kwa kifupi ni kwamba serikali ina taarifa karibu zote za hujuma ya nchi yetu lakini inajifanya kichaa na haioni kwa sababu tu wana masilahi binafsi na familia zao.
 
kushindwa vibaya kwa Intelligence system ya nchi hii! Pengine hawamuamini hata Rais kama ataweza kuchukua maamuzi magumu kuinusuru nchi
 
Hutaki Unaacha, naomba nijibu swali hili: Ni nani alimteua Mwamunyange na je ni nani anaweza kusitisha uteuzi wake?
Aspen,

Mbona unauliza majibu? Anayeteua ni rais. Akishateua hawezi kunuondoa mpaka muda wake utimie. Swali ni jee jina la Mwamunyange aliletewa na nani?. Sambamba na RO alipewa jina na nani? So do Said Mwema jina alipewa na nani sambamba na jaji mkuu jina alipewa na nani?. Ukiachia nafasi hizo za uteuzi najua inajua Spika Makinda jina lilitoka wapi? The King Maker is for real!.
 
kushindwa vibaya kwa Intelligence system ya nchi hii! Pengine hawamuamini hata Rais kama ataweza kuchukua maamuzi magumu kuinusuru nchi
Mtizamo, rais yupi?, aliyewekwa na nani?. Inteligensia ipi na maamuzi magumu yepi? kwa uwezo gani? kuinusuri niniiliyokwisha teketea?!.
 
Kama CIA wanahusika ktk politics za tanzania na endapo hizi taarifa zina ukweli , basi hii nchi haitakuwa "kisiwa cha amani " time will tell. tumeona yaliyotokea sierra leone , congo na hivi sasa yanayoendelea ktk nchi za kiarabu.
 
Back
Top Bottom