Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 2)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hutaki Unaacha, Jan 9, 2012.

 1. Hutaki Unaacha

  Hutaki Unaacha Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Previously: JK, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa historia (Part 1)

  Karume na Jussa ni wamoja na wanafahamiana vizuri sana kuliko wewe unavyofikiri. Kundi hili linao uwezo wa kuvunja Muungano muda wowote linaoutaka na kuanzisha serikali tatu na baada ya malengo kutimia likaanzisha serikali moja!. Ni vigumu kuelewa ni yapi majukumu ya Karume ndani ya hili kundi na nani kampa majukumu hayo na wapi kiburi cha Karume kimeegemea. Ni swala la historia ndefu sana ambayo nitaiunganisha vizuri baada ya kumchambua Rostam ambaye nitachukua muda mrefu kumchambua kuliko mwingine yeyote katika kundi hili.

  Nafikiri urafiki wako na Karume waweza kuwa umeingia doa kipindi cha 2007 hivi wakati umeletewa zile briefcase zilizojaa dola na kumhukumu Karume kabla hujaenda uarabuni!. Hivi zile dola zilienda wapi Mh Rais?. Zilikuwa nyingi kwelikweli. Hata hivyo Karume anaweza kweli kusahau mchezo mliotaka kumfanyia wewe na Nahodha kuhusiana na mwafaka kabla ya kipindi chake kuisha na kupelekea kumtishia Nahodha nafasi yake ya Waziri Kiongozi? Nahodha akabaki analia wakati wewe umemruka tayari baada ya kuona umezidiwa nguvu?.

  Mr President, unawafahamu waliokuwa nyuma ya mchezo huu? Basi hao hao kwa miaka mingi wangekwishakumaliza lakini Edward alionekana "kukupenda'" zaidi na yeye amekuwa akiwawekea ngumu yaani kukulinda lakini kwa bahati mbaya sana, amewakubalia hivyo kufanya "game'' kuwa kali. Edward anaweza kukulinda baadaye. Lakini hutaweza kufanya biashara yeyote ile na waweza kubaki na "njaa" kali sana baada ya kustaafu. "Game'' hii ni hatari kwasababu lazima imuweke Karume kwenye nafasi za juu za uongozi wa taifa hili 2015. Mh Rais naomba umuulize Mama Maria Nyerere akwambie vitisho alivyopewa na Karume na Mkapa kuhusiana na mwanaye makongoro wakati wewe unaendesha kikao cha NEC. Hata hivyo ni vizuri ukajiuliza swali la kitoto kama hili: Je ni kwanini Karume na wenzake walikushinikiza sana umteue Tom Apson kuwa mbunge wao wakikudanganya kwamba Tom amefanya kazi nzuri ya kuiba siri za Apson na malecela na wengine? Think twice Jakaya!.

  3. Rostam ni nani?


  Licha ya kuwa rais wa nchi hii tena Kamanda mkuu wa vyombo vyote vya usalama, umeshindwa kumfahamu Rostam kwa undani zaidi. Nikiri kwamba, bado hujamfahamu Rostam vizuri na sidhani kama ‘'vijana'' wako wanamfahamu vizuri. Kabla sijamwelezea vizuri, naomba nikukumbushe kitu kimoja. Hivi ilikuwaje mwaka 1995 wakati kambi yako inaomboleza baada ya kushindwa urais, Rostam alionekana kwenye sherehe ya kumpongeza Mkapa tena akiwa na Mkapa na kwa mazungumzo marefu sana?. Je aliwasaliti nyie washirika wake?.

  Nikiri tena kuwa, Rostam aweza kuwa mtu hatari, mwenye akili ya haraka sana lakini mwenye kuzichezea kwa akili ya juu sana siasa za Tanzania kuliko mtu yeyote aliye hai niliyeweza kumfahamu hapa Tanzania. Huyu akiwa pale LSE UK, alijenga urafiki mkubwa sana na binti wa mkubwa mmoja na muhimu katika Tehran (siasa za Iran). Haikufahamika kwa haraka ni nini alichokuwa akikitafuta kwa huyo binti na nani alimtuma ajenge huo urafiki ghafla kiasi hicho. Hili ninalolisema kwa sasa hata Lowassa hawezi kulifahamu, si wewe peke yako.

  Ni vigumu kuamini kuwa, Serikali ya Marekani imegharamia masomo ya Rostam LSE (baada ya hii task) na hii serikali kupitia Prof mmoja anayefundisha chuo kikuu kimoja UK huku akiwa ni mfanyakazi wa CIA iliweza kufanikisha urafiki mkubwa wa Rostam na huyu binti huku yeye (Prof) akiwaachia maelekezo vijana wa CIA baadhi kum-monitor Rostam na hatimaye urafiki ukawa mkubwa sana kiasi kwamba ukaweza kumfanya Rostam akubalike na Tehran.

  Kwa udhamini na wito kutoka serikali ya US, Rostam akawa anakwenda mafunzo mahsusi ya ki-usalama marekani na huko alikutana na watu wengi sana muhimu wakiwemo wamiliki wa Symbion. Kwa kukudokezea tu, pesa za Kagoda ni msamaha wa deni lililofanikishwa na ushawishi wake pale Tehran. Kwa bahati mbaya sana hata Mariam (mke wa Rostam) hakuufahamu uhusiano ule akifikiri ni mapenzi mpaka pale alipojua vinginevyo (ingawa hawezi kujua behind the scene kuna nini). Malengo ya Marekani na huu urafiki (Rostam-Tehran) bado yako palepale na nilipokutana na rafiki yangu (huyu aliweza kufanya kazi nzuri sana na Shah Riza kule Middle East) wa siku nyingi sana pale Boston, akanihakikishia kuwa lengo lilipangwa kutimia 2018 au 2022 hivi!. Ni hatari sana na mtandao wa Rostam na wenzake unaweza kukufanyia lolote watakalo kama usipokuwa makini!. Kule Saudi Arabia na sehemu nyinginezo ameweza kutumiwa sana na hawa "mabosi'' wake kwenye masuala ya biashara.

  Rostam anafanya kazi kubwa na nyingi za kibiashara na kisiasa na CIA kama agent wao muhimu sana Afrika huku yeye akisaidiana na mtandao wa CIA kule South Africa na ku-control sehemu kubwa Afrika Mashariki na Kati na sehemu nyingine za afrika ambazo US itakuwa na maslahi nazo. Mambo machache aliyoweza kufanikisha ni pamoja na kumfikisha Raila hapo alipo, mikataba ya kimaslahi na Salva Kiir achilia mikono ya Rwanda na Uganda kule Congo, Madagascar, mwafaka wa Zanzibar, kujivua gamba though kosa mojawapo ni wewe kukosea implementation hivyo kum-cost na kupelekea US kumwambia ajiuzulu ubunge na "kuacha'' siasa kitu kinachomfanya afanye siasa mara kumi ya aliyokuwa akiifanya awali.

  Mr President, muulize Othman akueleze ukweli kwa kuwa hili alilifahamu ingawa hajui ni kwanini lilitokea. Kumbuka vizuri wakati Bush amekuja Tanzania. Kule Arusha, viongozi wa makampuni makubwa yanayomiliki migodi mikubwa ambayo Bush, US na CIA ina maslahi nayo kutoka karibu kila kona ya dunia walikusanyika na walielezea ni kwanini biashara haiendi vizuri. Hakuna mtanzania yeyote Yule hata Deo aliyehudhuria except Rostam. Nani alimwalika na alihudhuria akitokea wapi?! Pale waliazimia mambo makubwa na ya hatari sana. Rostam anajua vizuri what happened na maazimio yale yalilenga nini.

  US imeona wewe ni shida kwa kuwa nchi ni kama inakushinda vile na haioni tena mvuto wako kwa wananchi na hii ni hatari kwa maslahi yao hasa mafuta ya Zanzibar ambayo imeshayalia timing kwa maana ya kwamba imeshirki kikamilifu kucheza "game'' ya Rostam-Jussa-Karume-Shein kwa haraka sana. Nimekwambia kwamba, Muungano waweza kuvunjwa na baada ya muda ukarudi tena nakuwa serikali moja. Jiulize ni kwanini Mwamunyange anakudharau kiasi hicho?. Hicho kiburi anakitoa wapi?. Mr President, usikurupuke, cheza karata vizuri!

  WAPENDWA WANA JF, MNIVUMILIE KWA MPANGILIO MBOVU. NITAENDELEA NA ROSTAM KWA UPANA ZAIDI, THEN APSON, MKAPA, EDWARD NA OTHMAN
   
 2. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mkuu Hutaki naona umerudi kama ulivyoahidi.Thanks mkuu,wacha tuchambue pumba na mchele!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Masimulizi yanaendelea....
   
 4. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mkuu ngoja nikopi haraka kabla hawajaiondoa.
   
 5. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  hutaki unaacha, ungetupa yote kwa pamoja
   
 6. t

  true JF-Expert Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Mhh mkuu!! Kumbe Rostam ni mtu hatari hivi?!!! Mungu wangu..,
   
 7. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu Hutaki Unaacha, umekosea sana. Ilitakiwa dossier ije kwa pamoja. Hali ilivyo hivi ni hatari sana.

  Mkuu hata mimi umeniacha hoi, maana kuna mambo mengi yame make sense kwa haraka. Haya tuone kama kweli JF ni jukwaa huru, Time will Tell, lakini kesho asubuhi corridor pale oysterbay zitakuwa busy mno.

  Chadema wanahangaika sana na kupeleka mambo ya ufisadi balozi za UK, US, Canada na zinginezo, lakini hawajui kuwa forces zinazocontrol natural resources zinataka mambo yawe kama TZ, na mafisadi ndio partners wa zile channel ambazo haziko kwenye official capacity, zenye nguvu kuliko hata congress. Kabila kashindwa Congo, watu wanataka UK, Canada, US wamforce out, SINCE WHEN?? Kwani Mobutu ilikuwa vipi??

  Democracy itatetewa kama nyie ni nchi ambayo hamna natural resources kama Ivory Coast, lakini TZ na hili balaa la mafuta ya off shore yaliyoko huku Zenj, ndio tumekwisha rasmi, ukiongeza na Gold, Diamond & Natural gas, Almighty God aliyotujalia.

  May God Bless TZ
   
 8. w

  watundawangu JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Duu!! Kwa maelezo hayo, idara ya usalama wa taifa ina kazi gani? Kama hii mijitu inajiingiza hapa nchini hakuna mtu wa kuwagusa... inaunda mitandao ndani ya ccm na serikali hakuwa wa kuwagusa... Sasa nchi hii inakuwaje chini ya nyang'au hawa ccm?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Acheni wasiwasi, hakuna ambacho kinasemwa hapa ambacho hakijulikani in the corridors of power za Tanzania. Na kwa wale wasomaji wa muda mrefu wa JF wanaweza kukumbuka mengi humu yameshasemwa hadi yamechosha. "Hutaki Unaacha" ameyaweka kwa mtiririko wake wa asili na kuunganisha. Mada hii itakuwepo na itaendelea kusoma JF is where "where we dare to talk openly"... just returning to our roots!

  Jukumu la mwenye akili ni kujua hesabu za MAGAZIJUTO!
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Ile ya RA kuwa ni mtanzania pekee kuhudhuria mkutano Arusha na Bush kama kweli ni hatari.
   
 11. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,868
  Trophy Points: 280
  NAFWAAAAAAA.!!!! Nilijua R.A ni simba Kumbe ni li dinosaur. Ee Mungu tusaidie wana wako :(
   
 12. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #12
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Rostam pia licha ya kuwa mbunge wa igunga ana uraia wa nchi mbili wakati ilo bado alitambuliki katika katiba ya nchi yetu sasa huo ubavu aliutowa wapi kama si kushikilia vyombo vya usalama na kupata support ya wanaomtumia kwa maslai yao binafsi?na pili lowasa kutokana na kujua rostam ni mtu hatari ndo maana anajua kwamba yeye ndo raisi ajae baada ya Jk.hapa ndipo nakuja kuamini cdm na nape wanacheza ngoma wasioijua.
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  Sasa kama chadema watachukua nchi 2015 hali itakuwaje? Hawa jamaa wataenda wapi?
   
 14. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  hii ni hatari ndo maana pinda alisema kuwa kuna kamtandao ka watu wachache wameamua kuziteka rasilimali zetu siku kakiguswa basi serikali yote inatetetereka
   
 15. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Huu mtandao una mwisho, lakini kipindi hicho watakuwa wameiacha Tanganyika ikiwa taabani. Kizazi kijacho kitabidi kianze kujenga nchi upya.
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CDM haiwezi kuchukua hii nchi. Hizo ni story za JF tu!
  Na huo mtandao haujakaa kihivyo ...... ni mchina ndiye atayemweka rais 2015.
  Haya maongezi yataisha baada ya uchaguzi wa CCM.
   
 17. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  taratibu naanza kuelewa kuwa kumbe TZ tuna Mafia wa kisiasa! We are in tough time mbele, nasubiri mtiririko kamili, Mr Hutaki Unaacha keep on bringing the goods!
   
 18. c

  cicy Member

  #18
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  huyu ndio rostam bwana tutaona na kusikia mengi juu yake. ila mungu yupo huu mtandao wake na hao usa una mwisho. time will tell
   
 19. c

  cicy Member

  #19
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  umeeona ee mkuu hii kitu ni hatari sana najiuliza kwa nini hawa watu hawakufikiria na kujiuliza nana kamuurika rostam na kwa nini yupo peke yake mtanzania
   
 20. Mr. Bigman

  Mr. Bigman JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,855
  Likes Received: 629
  Trophy Points: 280
  Rostam! CIA agent? can't believe this. This man is terribly dangerous. Really
   
Loading...