Kikwete Hongera kwa Ujenzi wa barabara! Ongeza zaidi Kasi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete Hongera kwa Ujenzi wa barabara! Ongeza zaidi Kasi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mlengo wa Kati, May 31, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Leo Rais Jakaya Kikwete ameonekana mwenye furaha zaidi na kusema wanaobeza utekelezaji wa Serikali kuwaletea Watanzania Maendeleo wana agenda zao za Siri na wana macho lakini hawataki kuona kinachoendelea! Akifungua baarabara ya Lami ya Somanga amewataka wananchi waitumie barabara hiyo kwa kurahisi shughuli zao na kuinua uchumi wao. Barabara ya somanga ni mwnendelezo wa ujenzi wa barabara nchini kama ule wa babati singida ambao umeanza baada ya babati minjiku kukamilika na kufunguliwa!
  My take: Nakupongeza sana Kikwete kwa kufanikisha ujenzi wa barabara zinazo endelea nchini hata wale wanao fanya maandamano imekuwa rahisi kwao kusafiri upande mmoja kwenda upande mwingine kwa barabara za lami na wakifika huko hujitoa fahamu kuwa hakuna unalofanya! Endelea na ujenzi wa barabara na mambo mengine kwa kuwaletea watanzania maendeleo!
   
 2. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna chama cha siasa kimekariri kuwa kuwa upinzani ni kupinga kila kitu ili Nchi isitawalike! Ni ushamba wa kisiasa! Binafsi natambua jitihada za kimaendeleo zinazofanyika hasa barabara! Kwa sasa unaweza safiri kutoka sirari hadi Mtwara kwa lami! Hongera kikwete wapuuze wanasiasa vipande vipande!
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Tunampongeza sana tu kwa kufungua hii miradi ya barabara ambazo nyingi zilianza kujengwa katika awamu ya tatu au upembuzi yakinifu ulikuwa ni katika awamu ya tatu!
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hizo ni pesa za Bush ambazo hazisimamiwi na serikali!!!. Serikali ya marekani haiamini serikali yetu ya mafisadi hivyo hawajafanya kitu kuanzia kutoa pesa hadi usimamizi!!. Unaweza kumpa hongera tu ili ujisikie vizuri lakini ukweli ni kwamba barabara nyingi sana hazitengenezwi na serikali wala serikali haisimamii.
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,108
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hadi kipande cha Dar mwenge mpaka pale wako ni serikali ya Japan imetoa pesa na Kikwete ataenda kufungua lakini hata kampuni ni ya Japan. Tutampa hongera badaya ya kuwapa Japan hongera kutusaidia wakati nchi yao iko kwenye janga ka tetemeko.
   
 6. G

  Galula Jr Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Unampongeza kwa kujenga barabara wakati zinatumika pesa zetu, kama ungekuwa msaada sawa lakini tunampa kodi atuletee maendeleo na siyo kumwomba ni lazima afanye hivyo. Kwani rais wetu anatoa misaada ya hisani hiyo hadi apongezwe. THINK BIG!!!
   
 7. The sage

  The sage Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo furaha ya rais wako inaonekana kuwa ya gharama kubwa na inapatikana mara chache sana. Na isitoshe furaha hiyo anaipata kutokana na juhudi za waziri anayemwita mbabe!!
   
 8. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nawewe mmbeya tu, kwani lazima useme wanaoandamana tu? Kwani wewe hujui bila hao unaowaita wanaandamana ndiyo wanachangamsha serikali, na huoni kwamba wanamsaidia rais majukumu yake,
   
 9. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ujenzi wa miundo mbinu ni wajibu wa serikali, mtoto hawezi mpongeza baba yake kwa kuleta msosi nyumbani, bali atamshukuru kwa kumpa malezi mema na kumuwekea mazingira mazuri ya kujiendeleza kwenye dunia ya ushindani.

  Serikali itapongezwa kwa sera nzuri zitakazowawezeza wananchi wake kujiendeleza, sera si kujenga miundo mbinu wala si kutoa maji safi na nishati. Hivi vyote ni wajibu wa serikali.
   
 10. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  upinzani ni kupinga kila kitu.......! mwingine anaponda na kusema ni ya awamu ya tatu.....basi aipongeze serikali ya awamu ya tatu ya chamam cha......TLP
   
 11. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0


  John Marwa,
  Acha uongo ndugu yangu! Mimi ni mwenyeji wa Sirari na nimeshasafiri mpaka Mtwara. Kwamba unaweza safiri kutoka sirari hadi Mtwara kwa lami ni uongo. Sema unaweza safiri toka Sirari hadi Dar, then hadi Daraja la Mkapa. Baada ya hapo kuna kipande cha vumbi karibu Kilomita 100 hadi Nangurukuru (LINDI). Baada ya Nangurukuru kuna vipande vipande vya barabara ya Vumbi kama Kilomita 10 hivi. Ukishamaliza huo msoto ndo sasa unakamata mkeka wa lami hadi LINDI mjini hatimae MTWARA mjini.

  Hata ukisema upitie njia ya Sirari - Mwanza - Morogoro - Songea - Mtwara bado vumbi lipo. Kutoka Songea hadi Masasi ambapo utaikamata lami ili ikufikishe Mtwara ni Kilomita 470 za vumbi. Labda utuambie mwenzetu hiyo njia yako ya lami tupu kuanzia Sirari hadi Mtwara. Epuka ushabiki kwa Kikwete wa kijinga jinga.
   
 12. n

  nitasemaukweli Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unajua wanaoona hii barabara ni kitu cha ajabu na haikuwa haki yao na moja ya maelekezo yaliotakiwa kufanyika miaka ishirini iliyopita basi inaonekana jinsi gani makada wa ccm kweli wanaupungufu wa akili kichwani.

  Makada na empty head wa ccm, hizo trips za kikwete nje ya nchi zimeleta gharama kiasi gani tangu aingie ikulu? Mpaka leo hii kikwete katumia shilingi 200milioni na ubaya zaidi ni hapo anapotumia trips za serikali kufanya deals kama za Richmond na Dowans, barabara ngapi zingejengwa? Propagandas hazina nafasi tena onyo kwenu.
   
 13. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Sie wa Tabora mhh.. Hizo barabara tunazisikia kwenye bomba tu... Ingawa tunamawaziri wawili, na bunge lililopita tulikua na spika, bado haijasaidia kitu, hatuna hata barabara moja ya rami inayounganisha na mkoa mwingine.. Labda sie na Kigoma tuanze kudai uhuru wa kujitenga kama sudan kusini, hatujaona manufaa ya uhuru kwa miaka 50 sasa..
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  bongo bwana....
   
 15. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Sifa nyingi kazi kidogo,miaka 50 ya uhuru,taarifa habari ya leo magari karibia 50 yamekwama njia ya mtwara,hata ukimuuliza magufuli kati ya mkapa na jk nani ukifanya nae kazi unaipenda atakuambia mkapa,jk anamuagiza magufuli watu wafuate sheria ktk ujenzi wa barabara waziri akitekeleza jk na mizengo wake wanapambana nae aache so wanampa wakati mgumu sana waziri wao,pongezi pekee ni kwa magufuli kupambana na makandarasi wachwara,even jk anajuta awamu yake ya kwanza kumpeleka magufuli uvuvi angemuacha tangu awamu ya kwanza mi nadhani maeneo mengi yangepitika
   
 16. O

  Omr JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  magufuli,kikwete na mkapa ni chama gani?CDM? nyie lazima mtoe shukran kubwa sana kwa CCM lasivyo hata hizo taarifa za habari mgekua mnazisikia uhindini tu.
   
 17. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Ina maana ww ni ccm?mm nilichangia mada kama mtanzania ukiwa mtanzania unasheherekea miaka 50 ya uhuru huwezi pongeza maendeleo kiduchi ambayo hayalingani na rasilimali tulizo nazo,huwezi mpongeza mwanamke tukikuuliza unasababu gani za msingi unasema amenishauri ninunue jiko,kwani ww hujui umuhimu wa jiko?narudia tena,nampongeza magufuli kwa mapambano yake na makandarasi uchwara,jukumu la kumpeleka mtt shule ni la mzazi so ujenzi wa barabara ni la serikali nani ulitaka azijenge?
   
 18. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mkuu TBR ni vizuri uweke rekodi vizuri, umbali ambao unashida kwenye ile barabara ni kutoka daraja la Mkapa mpaka Somanga, pale si zaidi ya 60 km na kwa sasa eneo kubwa limejengwa tayari. nimepita mwaka juzi pale ukitoka Somanga na Nangurukuru hapakuwa na shida. waliopita hivi karibuni watujuze
   
Loading...