Kikwete hiyo ndiyo gharama ya ushindi wa mezani nchi inayumba!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wengi wetu tulisoma maandishi ukutani kuhusu hatma ya nchi hii ikiwa mikononi mwa kiongozi ambaye ushindi wake umeacha manung'uniko badala ya furaha kwa wananchi. Hali hii katika ulimwengu wa kiimani inamuacha kiongozi katika wakati mgumu kwani wananchi anawaongoza wanamheshimu kwa nje tu kwa sababu ya matakwa ya kikatiba lakini mioyoni mwao wanamtakia kila lililobaya.

Leo hii nchi yetu imefikia hali mbaya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Umaarufu wa kikwete siyo umeshuka tu bali umeporomoka na kinachomfanya atabasamu hadharani ni unafiki tu au waswahili wanasema anajibaraguza. Vinginevyo, lazima nafsi yake inamsuta kutokana na hali ya wananchi inavyozidi kuwa mbaya siku hadi siku. Mgao wa umeme ni aibu kubwa kwa taifa. Pamoja mgao huo, bei ya umeme ipo juu, vyakula muhimu bei juu, nauli za usafiri wa barabara juu, huduma ya maji hovyo, n.k. Kwa mwenendo huu nataka nimhakikishie kikwete kwamba hakuna siku wanayoisubiri watanzania kwa hamu kama siku atakayoacha madaraka na hiyo ndiyo gharama ya ushindi wa mezani.
 
Duhh! sidhani kama alipata ushindi wa mezani ila maisha magumu na mabovu ni moja ya sera zake. Anazitekeleza vyema. Bajeti ya mwaka huu tu inaupungufu wa bilioni 640 je atatekeleza ahadi alizotoa? Jumla ya ahadi ni trilioni 90. Bajeti ya 2011 ni trillioni 10 nazo awezi kuzipata. Ili atimize ahadi zake ni lazima awe na bajeti ya trilioni 20 kwa mwaka bila kuweka matumizi ya kawaida n.k Ilikuwa rahisi tu wananchi wenye uelewa mdogo wa kawaida kujua kuwa hawezi kutekeleza ahadi zake. Leo ni February katikati na hakuna mkoa wa Geita. unategemea nini kama ahadi ndogo hivyo ameshindwa kuitekeleza?
 
Back
Top Bottom