vilaza mpo wengi! huna hata uwezo wa ku-argue
Leo katika hotuba yake ya siku ya kuzaliwa CCM, kuna kauli nyingi za kikwete ambozo kama rais hakustahili kuzisema, mojawapo ya ,ni kauli yake ya kwamba pamoja na kumsifu sana Nyerere lakini alishindwa kutatua changamoto nyingi katika utawala wake na hivyo hivyo kwa marais wengine waliomtangulia, sembuse mimi (Kikwete). Alisema hayo akijitetea kwamba yeye sio wa kwanza kushindwa kuondoa matatizo ya watanzania.
Mimi nimeichukulia kauli hii kama simple/cheap excuse ya kikwete kwa jinsi alivyoshindwa kutatua matatizo ya watanzania. Sio tu kikwete ameshindwa kutatua matatizo bali ameyaongeza na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu zaidi. Anaweza kutuambia yeye kama rais am-achiave nini, wenzake wote wana vitu vya kujivunia.
Nyerere alijenga umoja wa kitaifa na kufanya watanzania kuwa wamoja na kuwepo kwa amani ambayo kikwete anajivunia leo, lakini pia mzee huyu alijenga uwajibikaji kwa watumishi wa umma kitu ambacho kikwete ameshindwa.
Mzee Ruksa aliruhusu uchumi wa soko ambao ulisaidi kufanya upatikanaji wa bidhaa muhimu ambazo mwanzo zilionekana kama anasa.
Mzee Mkapa akajitahidi kujenga uchumi imara bila kusahau miundo mbinu na kurudisha heshima ya wafanyakazi.
Pamoja na mapungufu yao viongozi waliopita wanayo ya kujivunia.
Akaja kikwete
1) akaharibu kabisa umoja wa kitaifa kwa kuanza na makundi ndani ya CCM (kwa kuanzisha mtandao wake uliowavuruga wengine) na baadae kuharibu umoja taifa zima kwa kuchochea ajenda zake za udini na ukabila.
2) Akabomoa kabisa uchumi alioujenga mzee Mkapa kwa kuendekeza anasa, matumizi makubwa serikalini, kusafiri kwenda kubembea na kuendekeza ununuaji wa magari ya kifahari yasiyo na tija, gharama za maisha zimepanda mno, thamani ya shilingi imeshuka sana, mfumuko wa bei hauelezeki.
3) Ametengeneza mitandao ya wizi kwa kuwatumia marafiki zake kama RA, ED kwa kutaja wachache.
4) Akaharibu kabisa mfumo wa elimu kwa kuanzisha kisiasa shule za kata zisizo na walimu wala vifaa, ukiangalia wanafunzi wanaofeli ni heri hata tungebaki na shule chache bora,maana waliofeli wanabaki kuwa darasa la saba hawawezi kusema wana elimu ya form IV.
Ni mengi jamani yanayoonyesha tofauti ya utendaji kazi wa kikwete na watangulizi wake, naomba niishie hapa.
Lakini Kikwete please dont look for cheap excuses, just admit that ur the most failure president we ever had.
najuta kuwa kwenye utawala wa jk!!!
hakuna hoja ya maana,zaidi ya chuki ndo imewatawala. Nyinyi mkisema maneno ya hovyo ok,sisi no. Tatizo JF imeingia ushabiki wa dini na vyama. Nasi twaenda kwa style iliyopo. Kwahiyo tuvumiliane